Kujenga Nyumba au Kununua Nyumba – Namna ya Kuamua

  | 3 min read
0
Comments
2201

Ukibahatika kuweza kumiliki nyumba, swali la kwanza kujiuliza ni, ni nunue nyumba au ni jenge nyumba?

Kuna nyumba nyingi nzuri za kunua Tanzania, na kununua nyumba itaondoa mchakato ndefu ya kujenga.

Ila, labda hutaona nyumba inayokufaa na hivyo, ukataka kujenga.

Sasa, kama hujui uchague ipi kati ya zote mbili, maswali yafuatayo yatakusaidia kufanya maamuzi:

1. Utafurahia mchakato wa kujenga nyumba?

Mchakato wa kujenga si ndogo. Itabidi:

  • Ununue kiwanja pamoja na kuichunguza kabla
  • Utafute muasisi mzuri wa kufanyanae kazi
  • Jiwekee muda maalum wa kutafuta rasilimali za kujenga, ulinganishe bei, utembelee eneo hilo mara kwa mara n.k

Mwisho wa siku, kujenga nyumba ni kazi kubwa na ili ufanikiwe inabidi kweli uwe na nia ya kujenga.

Kama huna nia hiyo, bora umtafute wakala wa nyumba na malazi atakayeweza kukutafutia nyumba.

2. Gharama yake ni kiasi gani?

Wengi si mamilionea wa Dola wenye uwezo wa kununua nyumba bila bajeti. Ila, badala ya kumuliza ndugu au rafiki gharama ya kujenga alafu uweke gharama yao kama bajeti yako, ata ushauri kutoka kwa wakala wa nyumba na malazi na mtaalam wa ujenzi ili kujua gharama ya kujenga.

Wakala wako ataweza kukupa bei za wastani za viwanja kwenye maeneo unayofikiria kujenga. Vile vile, wataweza kukupa bei za nyumba. Wakati huo huo, mtaalam wa ujenzi atakupa gharama ya wastani ya ujenzi wa nyumba yako.

3. Unataka kuishi wapi?

Sehemu unayotaka kuishi inawaza ikachangia maamuzi yako ya kununua au kujenga kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mfano, kama unataka kuishi kwenye maeneo karibu na mjini kama Upanga, kupata kiwanja itakuwa ngumu na ghali.

Ila, kama uko tayari kuhamia sehemu nje ya mjini kama Pugu au Bunju, kiwanja kiakuwa bei rahisi zaidi na hivyo, bora ujenge.

Ila, bei ya kiwanja kinaweza kikawa nzuri, lakini zingatia maisha yako ya kila siku. Kama unafanya kazi mjini, uko tayari kutumia zaidi ya lisaa limoja kwenda ofisini na lisaa limoja kurudi nyumbani kila siku? Je, maduka, migahawa, baa n.k yapo kwenye eneo hiyo?

4. Uko tayari kusubiri?

Watu wengi hawajenga mara moja. Inaweza ikachukua miaka kumaliza. Kwa hiyo kama una muda huyo na huna pesa yakutosha kununua nyumba, basi kujenga kunaweza kikakufaa.

Ila, kama tayari unapesa ya kutosha, fikiria kununua nyumba. Wakala wa nyumba na malazi mwenye ujuzi anaweza akakupatia punguzo la bei. Pia, ukinununa nyumba unaweza kuhamia mara moja. Ndio, inaweza ikahitaji matengenezo, lakini uzuri ni kwamba tayari utakuwa nyumbani.

5. Je, tayari umeshawaza nyumba yako itakuaje?

Wengi wetu tumeshafikiria kwa kiundani nyumba yetu itakuaje. Kama wewe ni mtu wa aina hii, kujenga kutakufaa zaidi ya kununua.

Furahia mchakato mzima

Unaweza ukakumbwa na gharama, maswala ya kisheria na mengineyo, ila, usisahau kwa iwe kwa kununua au kwa kujenga, nyumba yako itakuwa sehemu ambayo we na familia yako mtafurahia kwa muda mrefu sana. Kwa hiyo, muda wako na gharama zako hazitaenda bure.

Ila, hatutaki upate shida sana! ZoomTanzania ina wataalam wa ujenzi na mawakala wa nyumba na malazi watakaoweza kukusaidia kupata nyumba itakayokufaa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.