Jiografia na Hali ya Hewa: Hali ya hewa ikoje Tanzania?

  | 3 min read
0
Comments
3040

Tanzania sio nchi ndogo, kijiografia. Kuna takriban nchi 196 duniani na Tanzania ni namba 31 kwa ukubwa. Ni nchi kubwa Afrika Mashariki na ina mipaka na nchi 6 zingine – Kaskazini, Kenya & Uganda; Magharibi, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; na Kusini, Msumbiji, Zambia na Malawi.

Ikiwa na umaarufu kutokana na mchanganyiko wa nyika zake kubwa na visiwa vya kitropiki, jiografia ya Tanzania ni ya kipekee duniani.

Mikoa ya Kaskazini

Milima Kilimanjaro (mlima mrefu kuliko zote Afrika) na Meru, ambayo ilikuwa hai miaka ya nyuma, zote ziko kaskazini. Miteremko yao zimeweka misingi ya miji ya Arusha na Moshi. Urembo asili wa milima haya, hasa Kilimanjaro, zinavutia watilii wengi kila mwaka. Aidha, zote zinafurahiwa na wapandaji milima duniani.

Pia kuna mabonde makubwa, moja ambayo inafika Kenya. Jina lake? Serengeti, ikijulikana kwa wanyampori na uhamiaji wa wanyama, ilipata jina lake kutokana na neno la kimaasai la ‘Serengit’ inayomaanisha ‘mabonde yasiyo na mwisho’.

161km kutoka Serengeti ni Eneo la hifadhi Ngorongoro . Ikiwa na ukubwa wa 8,982sqm, ni moja kati maeneo mazuri yenye urembo nchini. Pia, ni nyumbani kwa Ngorongoro Crater. Zaidi ya hapo, utakuta wanyama 5 kuu hapa wakitumia ardhi nzuri ya Ngorongoro ipasavyo.

Mashariki (Mikoa ya Pwani)

Kuna mikoa mitatu mashariki mwa Tanzania – Pwani, Tanga na mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam.

Zote ziko jirani na Bahari la India na zinafanana kijiografia. Ziko kwenye ardhi bapa, zikiwa na mabonde machache. Pwani ndio kubwa kuliko zote. Ikiwa na ukubwa wa 32,000sqm, Dar pamoja na Tanga zinatosha ndani yake.

Visiwa vya Pemba na Unguja, ambazo ni visiwa vya Zanzibar, zipo mashariki mwa bara kwenye bahari la India.

Mikoa ya Kusini

Lindi, Mtwara na Ruvuma ndio ziko kwa chini kabisa Tanzania. Mtwara ndio ndogo kuliko zote. Ruvuma, ikiwa na 60,000sqm ndio kubwa.

Ilikubwa sio kila kitu na Mtwara ni mfano. Mtwara iko kusini mashariki na jirani yake naye ni bahari la India. Na hivyo, bandari yake ni ya tatu kwa ukubwa Tanzania. Uendelezaji wa bandari itachangia uboresha wa mkoa kwa ujumla, hasa baada ya kugundulika kwa mafuta na gesi. Maendeleo haya ya kiuchumi zinaonekana kwa kuangalia idadi ya watu, ambao ni nyingi sana kuliko Lindi na Ruvuma.

Mikoa ya Magharibi

Kigoma, Mbeya na Rukwa ndio mikoa yaliyo magharibi zaidi. Yote ni makubwa na yako mpakani na nchi kadhaa.

Kigoma iko mpakani na Burundi na Ziwa Tanganyika.  Kwa kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ipo karibu pia, Kigoma ni muhimu sana kwa usalama. Mbeya iko mpakani na Zambia, na ruti maarufu ya treni ya Tanzania Zambia Railway line (TAZARA) inapita huko. Ruti hii inaunganisha Dar es Salaam na Zambia. Ikiwa katikati ya Mbeya na Kigoma, Rukwa iko mpakani na Zambia na Ziwa Tanganyika. Ndani yake ni Rukwa Rift Valley ambayo ina upana wa 48km na urefu wa 200 maili.

Hali ya hewa

Tanzania ina misimu miwili kuu kila mwaka; Kiangazi na Masika. Kiangazi ni kati ya Juni na Septemba alafu huwa hamna mvua kabisa. Nyuzi za joto ziko kati ya 20C na 30C, wakati joto likipunguwa kadri mwinuko linavyoongezeka. Masika ni kati ya Novemba – Mei, wakati wastani wa nyuzi za joto zikiwa katikati au kidogo zaidi ya 30C kabla la jua kuzama na chini kidogo ya 30C baada. Unyevu nao unaongezeka sana msimu huu.

Kuna vipindi vitatu katika masika:

  • Novemba na Desemba – mvua  za muda mfupi
  • Januari na Febuari – Mvua inapungua maeneo ya pwani kwa miezi hizi.
  • Machi, Aprili na Mei – Mvua kwa muda mrefu

Jua linawaka kila siku Tanzania

Kwa ujumla, mchanganyiko wa hali ya hewa ya Tanzania na vutio asili iliyo barikiwa nayo inapafanya sehemu nzuri ya kuishi na ya likizo.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.