Jinsi Ya Kuvaa Kwa Ajili Ya Interview Ya Kazi

  | 4 min read
0
Comments
5329

Sisi sote tunajua kwamba maishani, pale unapokutana na mtu yoyote kwa mara ya kwanza inachangia kwa kiasi kikubwa mtazamo wa huyo mtu juu yako wewe. Kwa Tanzania, nchi ambayo watu wanjali na kuheshimu itifaki, hii ina ukweli haswa.

Sasa, ukiwa unatafuta kazi muajiri anaweza akawa na mtazamo juu yako baada ya sekunde 30 za kukutana na wewe. Mtazamo huo utakuwa umefikiwa hasa kwa jinsi ulivyovaa.

Sababu ya kufanya hivyo ni kwamba muajiri wako anajaribu kupata picha ya haraka kama utaweza kujaza nafasi unayowania. Ila, ingawa inabidi uvae vizuri kwa ajili ya Interview, haimaanishi kwamba lazima uvae suti. Kumbuka, mavazi yako ya interview lazima yaendane na mazingira ya kazi ya muajiri.

Kwa hiyo, mavazi yako yasipoendana na muajiri, unmuonyesha muajiri kwamba uelewa wako wa kazi unayomba ni ya chini kidogo. Hii inaweza ikafanya ukose kazi kabisa kabisa.

Kwa bahati nzuri, kuna baadhi ya vitu amabavyo unaweza ukazifanya kuhakikisha kwamba mavazi yako kwenye interview ni sahihi.

 1. Fanya utafiti wa utamaduni wa kampuni/shirika unaloomba kazi

Lengo la vazi lako kwenye interview ni kumwezesha muajiri kuona kwa kiurahisi wewe ukifanya kazi hapo.

Kwa hiyo, itabidi ufanye utafiti wa utamaduni wa kampuni ili ujue mavazi yao ya kazini yakoje. Namna ya kufanya hivi ni:

 • Kwa kupitia ukurasa zao za mitandao ya kijamii kuona ni jinsi gani wafanyakazi wa hapo wanavaa.
 • Kwa kufanya utafiti wa mavazi ya kazini ya sekta hiyo kampuni ilipo.

Ukijikuta kwamba baada ya kufanya utafiti bado huna hakika kuhusu mavazi ya muajiri huyo, wapigie simu alafu omba kuongea na afisa rasilimali watu.

 1. Onyesha utu wako ila kumbuka kwamba umekuja kikazi

Ni muhimu sana kuvaa nguo zinazokuweka katika hali nzuri pamoja na kufaa kanuni ya mavazi ya ofisini. Kwa mfano, kama kanuni ya mavazi ya kampuni ni zinaruhusu mavazi ya kawaida kidogo, sketi ya kitenge kwa mwanamke inafaa. Ila, hakikisha kwamba inashuka chini ya magoti, haishiki mwili na mavazi yako mengine yawe ya kawaida.

 1. Kuwa msafi

Hakikisha kwamba:

 • Umechana nywele na umweziweka sawa
 • Hakuna harufu mbaya yoyote inayotoka kwako. Pig mswaki na usile chochote yenye harufu kali.
 • Kucha zimekatwa na ni safi
 • Punguza ndevu ama zitoe kabisa (kwa wanaume)
 1. Usiwe na manukato au mengineyo mengi

Kama utatumia manukato, hereni, pete n.k hakikisha kwamba ni chache na ni za kawaida. Hutaki muonekano wako ifanye muajiri wako asisikilize majibu yako.

 1. Jiandae vyakutosha

Chagua vazi lako siku kadhaa kabla ya interview kuhakikisha kwa linafaa na linakufaa. Pia, jaribu kujibu maswali ya interview ukiwa umeivaa.

Kanunui za Mavazi

Hatakama unajua kanuni ya mavazi ya muajiri, unaweza ukakuta kwamba bado hujaelewa vizuri maana yake. Kukusaidia na hilo, zifuatayo ni aina 4 kuu za mavazi ofisini:

 1. Mavazi yenye hadhi rasmi ya Kiofisi

Kama unaomba kazi kwa wansheria, benki n.k vaa hivi:

Kwa wanaume:

 • Suti ya rangi moja (nyeusi, kijivu au bluu nzito)
 • Shati nyeupe yenye vifungo
 • Viatu vya kazini (nyeusi au brauni)
 • Tai ya kawaida

 

Kwa wanawake:

 • Suti ya suruali au sketi
 • Viatu vya kazini
 • Vipodozi na hereni/pete/bangili vya kawaida.
 1. Mavazi yenye hadhi ya Biashara ya kitaalamu

Hapa, mavazi yanafanana na yale ya biashari rasmi, ila unaweza ukavaa:

 • Rangi zaidi ya nyeupe, nyeusi, kijivu na bluu nzito
 • Vifaa vya nguo vinaruhusiwa zaidi
 1. Mavazi ya kibiashara yasiyo na hadhi rasmi

Hii ni aina mavazi ya ofisini utakayokutana nayo kwa wingi zaidi. Unaweza ukavaa:

Kwa wanaume:

 • Mashati, t-shirt (mradi uivae na koti la suti) kwa rangi yoyote
 • Tai zenye rangi mbali mbali
 • Suruali nyeusi, za brauni hata jinzi za rangi nzito.
 • Saa ya mkononi
 • Viatu vya buti, vya ofisni, vya rangi tofauti.

 

Kwa wanawake:

 • Sketi au gauni zinazofikia magoti, suruali au jinzi za rangi nzito
 • Mashati ya rangi mbalimbali
 • Bangili, mkufu, hereni
 • Viatu vyovyote mradi sio sandals
 1. Mavazi ya kawaida

Ukibahatika kuitwa kwenye interview kwenye ofisi inayoruhusu mavazi ya kawaida, bora uvae mavazi ya kibiashara yasiyo na hadhi rasmi. Bora kufanya hivi kuliko kuvaa mavazi ya kawaida sana.

Vaa kwa kutarajia mafanikio

Kuitwa kwenye interview ya kazi ni kitu kikubwa sana. Itasikitisha sana kama unakosa kazi kwa sababu ya jinsi ulivyo vaa.

Hatuajiriwi kwa kutegemea ujuzi wetu tu. Kili kitu kuanzia namna tunavyojieleza mpaka mavazi yanachangia. Kwa hiyo, kumbuka kwamba mtazamo muajiri atakayoupata kwa kukutana na wewe mara ya kwanza lazima iwe nzuri. Mavazi huchangia kwa kiasi kikubwa hili swala.

Tafuta duka la nguo yenye nguo bora.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.