Jinsi ya Kutafuta Nyumba ya Kupanga

  | 5 min read
0
Comments
3326

Kutafuta sehemu ya kuishi ni kazi kweli kweli, hasa ukiwa Dar es Salaam kwa kuwa  ni gharama kubwa. Pia, sheria za nyumba zinampendelea mwenye mali na huwa unalazimishwa kulipia miezi 6 au mwaka mmoja  kabla ya kuhamia. Kwa hiyo wengi wanakubali kwamba, ikija kwenye swala la kukodi nyumba Dar, ni shida!

Ila, ingawa kuna changamoto, utafiti uliofanyiwa na Shelter Afrique ilithibitisha kwam 80% ya watu wanaoishi Dar es Salaam wamepangisha. Watu wanapangisha kwa sababu:

  • Walihamia Dar kutoka mikoa mingine kwenda chuo au kwa ajili ya kazi
  • Wanataka kuondoka nyumbani na kujitegemea
  • Kuwa karibu na ofisi

Kwa sababu yoyote ile, watu wengi Dar wanapangisha. Hii ni ukweli kwenye miji mingine Tanzania pia. Kwa hiyo, iwe mara ya kwanza kutafuta nyumba ya kupanga au kama una uzoefu, videkezo 10 vifuatayo vitakusaidia:

1. Weka Bajeti

Kitu cha kwanza cha kujiuliza ni, je bajeti yako inakuruhusu kukodi?

Ni rahisi sana kuwaza tutakavyo pamba nyumba yetu na sherehe tutakazozifanya hapo. Ila, inabidi ujipe bajeti alafu uifikie.

Kumbuka, kulazimika kulipa kodi ya miezi 6 kabla ya kuhamia ni kitu cha kawaida. Pia, zingatia gharama za kuhamia, fenicha za kununua, bili za maji na umeme n.k

2. Amua ni nini ambacho ni muhimu kwako

Kabla ya kuwaza rangi ya kupaka ukutani, anza kufikiria vitu ambavyo ni muhimu kwako.

Kabla ya kuanza kutafuta nyumba, andika orodha ya vitu muhimu utakavyo vihitaji. Kwa mfano:

  • Vyumba viwili vya kulala
  • Bafu moja chumbani na nyingine ya wageni
  • Jiko yenye tanuri inayofanya kazi
  • Sebule
  • Nafasi ya kupaki gari
  • Maji na taa
  • Eneo liwe karibu na supermarket.

Ukishajua vitu muhimu vitakavyo kupa faraja nyumbani, vitakusaidia kuwa na malengo ukiwa unatafuta nyumba.

3. Chagua maeneo

Bajeti lako litaamua utakapoishi.

Inawezekana kwamba tayari unafikra zako za kibinafsi kuhusu maeneo mbalimbali, ila miji mikubwa kama Dar es Salaam zina maeneo ambayo utakuta yanakufaa bila wewe kutegemea. Mara nyingi, watu wanaishia kulipia zaidi ili waishi kwenye eneo maarufu, ila wanaishia kuishi maisha yaleyale ambayo wangeishi kwenye eneo isiiyo maarufu sana.

Kwa hiyo, tumia tovuti za matangazo kama kipengele cha Nyumba na Malazi ya ZoomTanzania ili ufahamu bei za nyumba kwenye maeneo tofauti.

4. Tafuta Wakala wa Nyumba na Malazi

Ingawa watu wengi wanaamua kutafuta nyumba kivyao, kuna faida nyingi za kutumia wakala wa nyumba na malazi.

Kwanza, wanamaarifa zaidi kuhusu bei za soko hiyo na wanaweza wakakuonyesha maeneo tofauti, mengine ambayo ulikuwa huzijui.

Pia, wataokoa muda wako kwa kuwa ni kazi ya kutafuta na kukadiria nyumba – ili wewe usiwe na haja ya kufanya hivyo.

Pitia wakala wazuri wa nyumba na malazi hapa.

5. Jiandae kwa chochote

Kuna uwezekano mkubwa kwamba utakutana na changamoto mbalimbali.

Labda wakala wako wa nyumba na malazi amepata nyumba iliyo na 74% ya vitu unavyotaka. Je, utataka kuiangalia?

Au wamepata nyumba yenye kila kitu unachotaka ila kodi ni kubwa zaidi ya ulivyotegemea. Je, utaweza kuigharamia?

Au mara nyingine unakuta kwamba kwa bajeti yako, hutapata vitu vyote unavyohitaji kwa nyumba. Ila, ukihamia na mtu mwingine, itawezekana. Je, utaweza kuishi na mtu mwingine?

Jiandaa kufanya maamuzi usiyoyategemea na jiandae na chochote ila zingatia vile vitu ambavyo ni muhimu kwako.

6. Jitume

Hata kama unatumia wakala wa nyumba na malazi, usiache kutafuta nyumba kabisa kabisa.

Kwa mfano, ZoomTanzania inakuwezesha kupata tahadhari zitakazo kuja kwa barua pepe kukutaarifu kwamba nyumba (au apartment) mpya imetangazwa.

Pia, mapendekezo ya watu ni njia nyingine ya kutafuta nyumba. Waambie marafiki na wanafamilia kwamba unatafuta nyumba. Pia, waambie wenzako kupitia mitandao ya kijamii.

7. Uliza maswali kwa simu

Ukianza kuona baadhi ya nyumba zinazonekana nzuri, kabla ya kufunga safari ya kwenda kuziona, ongea na mwenye nyumba kwa simu. Kwa kufanya hivi, utaweza kujua kama ni mkweli. Pia, unaweza kumuuliza maswali mengine ili ujua kama kuna vitu vya ziada unazohitaji kujua.

Pitia maswali ya kuuliza kabla ya kukodi nyumba au apartment.

8. Tembelea Nyumba/Apartment

Ukisharidhika na majibu ya mwenye nyumba baada ya kuongea naye kwa simu, panga muda wa kwenda kupaona. Nenda na wakala wako wa nyumba na malazi na rafiki yako. Usitegemee mapendekezo ya wakala wako kabisa kabisa. Kuwa na maona yako mwenyewe.

Uliza maswali mengi. Kwa mfano, uliza ‘majirani wakoje?’. Kwa vile, kama majirani ni watu wazima au wazee na wewe ni kijana aliyechangamka, labda hapatakufaa. Hutaki kuambiwa kwamba wewe ni msumbufu au ubadilishe maisha yako.

9. Makubaliano

Kama huhamii kwenye ghorofa la apartments zenye bei kamilifu, utakuta kwamba wenye nyumba wengi wanaweka kodi 10% juu ya walichotayari kupokea. Kwa hiyo, ongea na jaribu kushusha kodi. Kama unatumia wakala wa nyumba na malazi, waambie bei uliyotayari kulipa na waachie wafanye makubaliano.

10. Hakikisha una hati zote

Kwa kuwa utapeli ni jambo la kawaida Tanzania, hakikisha kwamba makubaliano yote yameandikwa, kuna nakala na zimesainiwa na wahusika wote. Usilipe kodi bila mkataba.

Kabla ya kusaini mkataba, isome vizuri. Ili kuwa makini kabisa, some sheria ya kukodi nyumba Tanzania kujua haki zako na hivyo, ujue ukubaliane na nini na usikubaliane na nini.

Faraja ndio cha muhimu

Mwisho wa siku, wote tunataka kuishi kwenye nyumba inayotuletea faraja. Zingatia hili ukiwa unatafuta nyumba (au apartment) ya kuisihi. Iwapo unakodi nyumba au apartment, utatumia muda wako mwingi hapo. Inaweza isiwe na kila kitu unachotaka, ila, ukifuaya vidokezi hivi itakuwa na kila kitu unachohitaji.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.