Jinsi ya kula vya kula vya afya ukiwa umekosa muda

  | 3 min read
0
Comments
2389

Vyakula vingi vya Tanzania vina wanga nyingi na nyama. Mboga za majani huwa zinawekwa pembeni.

Hii inaleta changamoto kwa wale wanaotaka kula kiafya zaidi. Pengi wengi wetu ambao tungependa kula vyakula vyenye afya zaidi ila hatuna muda wa kuzipika.

Ila, haimaanishi kwamba kula kiafya kinashindikana kabisa.  Vifuatayo ni vidokezo  7 za kula kiafya zaidi Tanzania:

1. Badilisha mtazamo yako juu ya chakula cha kiafya

Kula kwa afya haimaanishia kwamba inabidi uachane na nyama kabisa na vitu vingine vitamu.

Kula kwa afya inamaanisha kwamba unakula chakula bora yenye virutubisho vya kutosha. Virutubisho hivi vinapatikana kwenye mayai, kuku, nyama, maharage, parachichi, karanga na mengineyo.

Pia, mboga za majani, viazi vitamu wali wa brauni na vyakula vingine vyenye ‘wanga nzuri’ zinahitajika.

Aidha, mapishi ya chakula chako yanchangia kwenye maswala ya afya. Jiulize:

  • Unatumia mafuta mengi ukipika?
  • Vyakula vyako vingi ni vya kukaanga?
  • Unaongeza chumvi au mchuzi kwa kiasi gani?

Kingine cha kufikiria ni ukubwa wa kiasi chakula unalokula.

2. Uandaaji wa mlo

Tenga siku au mchana mmoja wa wikiendi kupika chakula cha wiki, ziweke kwenye makontena alafu uzihifadhi kwenye jokofu ukiwa unazitoa kadri ya unavyozila.

  • Siku nzuri ya kufanya hivi ni Jumapili
  • Hatua ya kwanza ni kuweka orodha ya vyakula vyote utakavyohitaji na kuzinunua
  • Baada ya hapo utaweza kupanga milo wako wa kila siku

Ukiamua na kuanza kufanya hivi, utakuta kwamba sio kitu kigumu cha kuendeleza.

3. Vitafunio ni muhimu

Vitafunio kama matunda, maziwa ya mgando na karanga zitakusaidia ukiwa na njaa. Kuna rasilimali nyingi kwenye intaneti zitakazo kusaidi na risipi.

4. Chagua migahawa vyenye chakula cha kiafya zaidi

Bahati nzuri, ZoomTanzania ina taarifa na menu za migahawa zenye vyakula vingi vya kiafya. Kumbuka, milo ya kiafya zina wanga, protini, mboga za majani na matunda.

5. Kifungua kinywa ni lazima

Kufungua kinywa ni muhimu sana. Na, ukifanya hivyo kiafya zaidi, itakusaidia:

  • Kuwa na motisha kuendelea kula kiafya
  • Kukuridhisha na hivyo hutakula chochote kile kitakacho kuja mbele yako

6. Fanya mazoezi na rafiki yako

Mazoezi ni muhimu kwa maisha yako.

Kwa hiyo, kufanya uwajibike zaidi, fanya mazoezi na rafiki yako. Pia, ukifanya mazoezi na rafiki yako inaifanya iwe kama njia nyingine ya kukutana kwenu badala ya kitu cha kulazimisha au adhabu.

7. Kuwa mkweli

Siku zingine hutajisikia kula kiafya, inatokea.

Kwa siku kama hiyo, unaweza kula unavyo taka ila kwa kutumia akili. Kula baga ila usiweke mayonaizi, kula kipande cha keki au slesi ya pizza.

Hii sio utaratibu maalum wa kula tu, ni maisha

Kula kiafya ni tabia ya maisha na inahitaji muda kuiweza. Ila, mwili na akili yako zitatoa shukrani zao.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.