Jinsi ya kuhamia Dar Es Salaam

  | 3 min read
0
Comments
542

Iwapo unahamia Dar au unarudi Dar kutoka mji mweingine, kuna vitu vya kujua kuhusu mji huu kukusaidia uhamiaji.

1. Kodi ni kubwa sana

Ingawa Dar sio New York, ina kodi za nyumba za juu kweli kweli, kutegemea na eneo utakalopenda kuishi. Pia, utalazimika kulipa kodi ya miezi 6 au mwaka.

Kwa kama unampango wa kukodi nyumba, fikiria bajeti yako.

Uko tayari kuanza kutafuta malazi? Tuna apartment na nyumba zinzaopangshwa hapa.

2. Fanya utafiti wako kabla ya kwenda hospitalini

Mtoa huduma wa bima yako ataamua hospitali gani utakazoweza kutumia. Ila hospitali zinatofautiana kwa ubora wa huduma.

Baadhi za hospitali zitatambua ugonjwa wako kwa haraka na kupa dawa nyingi, bila sababu. Kwa hiyo, kabla ya kuchagua hospitali uliza watu unawajua wanatibiwa wapi.

Pitia baadhi ya hospitali hapa.

3. Nunua gari yenye matumizi mazuri ya foleni

Dar ina foleni nyingi na unaweza ukawa na , lakini kuwa na gari isiyotumia mafuta mengi ni suluhisho bora.

4. Mavazi yako (kwa wanawake)

Mavazi yako inabidi yaendano na mazingira yako.

Kwa mfano, kama unatumia usafiri wa umma, vaa nguo zisizoonyesha umbo wa mwili wako sana. Ila kama uko kwenye gari yako au unaenda kazini au kwenye baa unaweza uka vaa skirt/gauni inayofikia magoti yako au juu kidogo.

Tumia akili yako ya kawaida.

5. Kuna sehemu nyingi za kujiburudisha

Utaishia kupata sehemu 2 au 3 utakazozipenda sana. Ila, zitakuja kukuboa ukiwa unaenda huko tu. Kwa, jaribu sehemu nyingine mbalimbali.

Kuna baa na migahawa mingi mizuri kwenye mji huu. Jaribu hizi kwa kuanzia.

6. Kuwa na msaidizi wa nyumba ni kitu cha kawaida

Familia nyingi zina msaidizi wa nyumbani.

Wengi wao wanawaajiri kwa njia isiyo rasmi (kama mapendekezo ya rafiki au mwanafamilia). Ila,ukitaka mchakato uliorasmi zaidi, kuna kampuni nyingi za kuaminika zinazoweza kukusaidia na hili swala.

7. Jifunze Swahili

Watanzania wengi hawaonge kiingereza kizuri, kwa hiyo kuweza kuongea Kiswahili, hata kidogo, ni muhimu.

Tafuta darasa yako ya kwanza hapa.

8. Kujadiliana kuhusu bei ndio maisha ya hapa

Mradi hauko kwenye duka ambayo bei za bidhaa zimekamilika, unaweza kujadiliana kuhusu bei za bidhaa nyingi.

9. Usafiri wa umma

Kuna aina 4 kuu za usafiri wa umma:

  • Dalala
  • Bajaji
  • Taxi
  • Bodaboda

Daladala ndio zinazotumika kuliko zote na nizenye bei nafuu kuliko zote. Ila, zinajaa sana na madereva huwa si wamakini.

Matokeo yake, watumiaji wa bajaj na bodaboda wanaongezeka na wanaweka makubaliano maalum ya usafiri na dereva.

Pia, kuna Mabasi ya Mwendokasi yalioanzishwa mwaka huu.

10. Muda

Watanzania wengi wanachelewa kote pale wanapotakiwa. Kwa hiyo, utahitaji subira au panga mambo yako lisaa limoja kabla ya muda unaotakiwa – ili watu wawahi.

Utapapenda

Ingawa kuna michakato mengi ya kuhamia Dar, fukwe zake, watu wake nautulivu wa maisha yatakufanya upapende na kutojutia kuhamia huku.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.