Jinsi ya Kuchagua Wakala wa Nyumba na Malazi

  | 4 min read
0
Comments
424

Wote tumewahi kuambiwa kuhusu mtu aliyenunua kiwanja na kukuta kwamba kiwanja hicho ilishauzwa.  Au, wenye nyumba kupandisha kodi ghafla na kufukuza wapangaji.

Hapa Tanzania, tuna utamaduni wa kukubaliana vitu kwam mdomo, bila hati yoyote au chochote kuandikwa. Hii ni tatizo kwenye maswala ya nyumba na malazi.

Matokeo yake ni kwamba inbidi uwe na busara wa hali ya juu ukiwa unatufuta nyumba na pia, ukiwa unaingia kwenye makubaliano. Hii inafanya shughuli nzima iwe ndegu zaidi na kuchukua muda wako mwingi.

Kwa hiyo, iwapo unatafuta apartment ya kupanga au unajaribu kuuza nyumba yako, unaweza ukafaidika kwa kutumia wakala wa nyumba na malazi.

Mwisho wa siku, bora umtumie mtu au kampuni yenye ujuzi, uzoefu na maarifa kuhusu soko la nyumba pamoja na mikataba kuhakikisha kwamba hutapeliwa. Ila, watanzania tuna tabia ya kwenda kwa mtu tunayemjua. Iwapo kumwomba ndugu au rafiki yakoakusaidie kutafuta nyumba, ni vyema kufanya utafiti kidogo na kuuliza maswali mengi kabla ya kumchagua wakala wako.

1. Umefanya biashara hii kwa muda gani?

Uzoefu ni muhimu sana.

Kama unajaribu kutafuta apartment au kununua nyumba, wakala mwenye ujuzi atajua vitu vyakufikiria wakata mnachunguza nyumba, watajiamini wakiwa wanafikia makubaliano ya beina waakuwa na ujuzi wakukupatia vitu vingine vya ziada.

Ila, wakala amabaye ni ‘mpya’ aliyeingia kwenye biashara hii hivi karibuni ataweza kukushauri juu ya mwenendo za kisasa kwenye soko la nyumba. Pia, watataka kuthibitisha kwamba wanaweza kwa wataweka juhudi kali.

Vilevile, mantiki hii inatumika ukiwa unataka kuuza nyumba. Wakala mwenye uzoefu atakuwa na fomula ya kuuza.

Pia, kumbuka kwamba kama unajaribu kuuza mali, uzoefu sio tu miaka ambazo wakala huyu amekuwa akifanya biashara hii. Pia, ni idadi ya mauzo waliofanya.

2. Una utaalamu kwenye aina gani na maeneo yapi ya nyumba/apartment

Kwa wanunuzi au wapangaji, bajeti ndio kitakacho amua utakapoishi. Kwa hiyo, ukipata waka mwenye ujuzi wa eneo unayotaka kuishi au aina ya nyumba/apartment unayotaka itakurahisishia kazi.

Aidha, kanuni za viwanja vinatofautiana eneo kwa eneo. Hutaki kununua nyumba leo alafu uambiwe kesho kutwa kwamba liko kwenye eneo la baraba kwa hiyo ‘bomoa bomoa’ wako njiani.

Aidha, zaidi ya hayo, watu wanaweza wakataka kutafuta nafasi ya ofisi, nyumba ya likizo, majengo ya viwanda n.k Ni muhimu kwamba wakala wako ana uzoefu na mahitaji yako, kwa kuwa zitahitaji uchunguzi, kanuni na mikataba tofauti.

3. Unawasiliana vizuri na watu?

Wakala wako anabidi aweze kuwasiliana kwa kasi.

Unaweza ukakosa dili safi kwa kuwa alichelewa kukutaarifu. Kwa hiyo, hakikisha wanapatikana kwa barua pepe, simu na mitandao ya kijamii.

Aidha, kama unataka kuuza, wakala wengine wanatabia ya ‘kuongeza chumvi’ kuhusu mali yako iliwauze. Kuwa makini na wakala wa aina hii kwa kuwa wanaweza wakuingiza katika matatizo mengi kwa kuahadi vitu ambavyo huna nia ya kutekeleza.

Jiulze, vitendo vya wakala wangu zinaendana na wanachoongea?

4. Kuna watu ninaoweza kuongea nao kuhusus utendaji kazi wako?

Wengi wetu tunajikuta tukitafuta huduma mbalimbali kupitia mapendekezo. Utafutaji wa wakala wa nyumba na malazi nayo inabidi iwe hivi. Waambie wakupatie orodha ya wateja wao ili uweze kuongea nao na kujua zaidi kuhusu utendaji kazi wa wakala huyo na kama wateja wake wameridhika na huduma.

Kumbuka, utamlipa wakala huyu kwa huduma yake kwa ni muhimu kujua kama wanastahili kuchukua pesa yako.

5. Huduma yako ni shilling ngapi?

Unaweza ukafikiri kwamba gharama ya wakala ndio kitu cha muhimu cha kuzingatia ukiwa unachagua wakala wa nyumba na malazi. Ila, kuna mengine. Kwa mfano, wakala wengine wanaweza wakawa na gharama ya chini zaidi ila unaweza ukakuta kwamba hawana uwezo wakutangaza mali yako kama wakala wa bei ghali zaidi.

Pia, wakala wa bei ghali anaweza akawa ana Featured Business Lisiting (FBL) kwenye tovuti ya ZoomTanzania na kuweka picha na maelezo ya nyumba yako kwenye kurasa yao. Ukiwa na FBL biashara yako inaonekana zaidi na hivyo kuvutia wanunuzi zaidi.

Kama unataka kununua nyumba/apartment, wakala wengine wanaweza wakawa na gharama zaidi ila watuhakikishia kwamba watakutafutia nyumba ndani ya wiki mbili. Wengine watakuwa na gharama nafuu zaidi ili wanaweza wakachukua muda zaidi.

Iwapo unauza au unanunua, ukiwa una fanya tathmini ya gharama za wakala wa nyumba na malazi, zingatia unachopata na unachokosa. Pia, usizidi bajeti yako.

Rahisisha maisha yako

Zamani, kuuza au kununua kiwanja au nyumba ulikuwa unawaambia ndugu na marafika kwamba una nia na wao wangekuelekeza kwa watu wanaowafahamu kukusaidia. Leo hii, mapendekezo kama haya bado yanasaidia ila, kutafuta na kununua mali bado inahitaji mtaalamu atakayeweza kukusaidia kuepukana na utapeli, bei zilizongezwa na mikataba.

Sasa, uko tayari kuanza?

Wakala wengi wa nyumba na malazi wanajitangaza kupitia ZoomTanzania na wako tayari kukusaidia kutafuta nyumba itakayokufaa kabisa.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.