Jinsi Ya Kuandika Maelezo Ya Kazi: Wavutie Wafanyakazi Wa Hali Ya Juu

  | 4 min read
0
Comments
2596

Wafanyakazi wazuri watachangia mafanikio na ukuaji wa biashara yako. Hivyo, inabidi ujitahidi kuwavutia wafanyakazi bora. Ila, waajiri wengi Tanzania hawazingatii namna maelezo ya kazi yanavyochangia kuwavutia wafanyakazi bora.  Ni lazima kwamba kampuni/biashara/shirika ilete picha nzuri na maelezi mazuri ya kazi ni njia mojawapo ya kufanya hivyo.

Maelezo ya kazi ndio yatatoa mtazamo wa kwanza juu ya kampuni yako kwa watu wanaotafuta kazi. Kwa hiyo, lazima iwe sahihi, ilete picha ya kufanyakazi hapo na imfanye mtu apate msisimko wa kufanya kazi na kampuni yako.

Sasa, hii ndiyo namna ya kuandika maelezo ya kazi mazuri:

Kwanza: Jina la Kazi

Jina la kazi lazima ivutie na ionyeshe umuhimu wa hiyo kazi

 • Tumia vielezi: Jina la kazi linabidi lieleze ni kazi gani haswa itakayofanyika ndani ya nafasi hiyo. Kwa mfano, badala ya kuita nafasi ya kazi ‘secretary’, iipe jina la ‘mtendaji msaidizi’.

Pili: Maelezo ya kazi

Hapa, unatoa maelezo ya hiyo kazi kwa ufupi, pamoja na majukumu ya atakayechukua nafasi hiyo.

 • Maneno muhimu: Tumia maneno yakumvutia mtu atakyekuwa anatafuta kazi ya aina hiyo. Pia, tumia maneno yatakayo gusia maarifa, ujuzi na utu utakayohitajika kwa ajili ya nafasi hiyo.
 • Elezea vizuri: Eleza ni kazi zipi haswa mwajiriwa atakuwa anafanya siku kwa siku ndani ya nafasi hiyo. Kwa mfano, ‘Kama Mhariri Mkuu, 75% utakuwa unatumika kuwaongoza wafanyakazi chini yako juu ya mada ya wiki, kila wiki’.
 • Historia ya Kampuni: Toa historia ya kampuni kwa ufupi, ikiwemo mafanikio, muelekeo na utamaduni wa kampuni. Pia, eleza ni jinsi gani mwajiriwa ata toa mchango wake kwenye kampuni. Wafanyakazi wanapenda kujisikia kwamba wanatoa mchango wa maana.
 • Maelezo maalumu:  Kumbuka kuweka maelezo muhimu kama jina na mkuu wa idara, aina ya kazi, mahali ya kazi n.k
 • Mshaara na mengineyo: Usitaje mshaara kabisa kabisa ila, onyesha kwamba mtu atalipwa kulingana na ujuzi wake wa kazi pamoja na kazi yenyewe. Pia, kama kuna maslahi mengine au faida nyingine ya hiyo kazi, zitaje.
 • Kuwa mchangamfu: Hata kama unaadika maelezo ya kazi ya mtu wa chini kabisa, lazima uonekane kwamba umechangamka na utamchangamkia atakayepata kazi hiyo. Kumbuka, hakuna kazi ndogo. Kila mtu ana nafasi ya kuchangia mafanikio ya kampuni yako.
 • Usomaji: Hakikisha maelezo ya kazi yako yanasomeka vizuri. Hivyo, usiandike sentensi ndefu sana na ukiweza, toa maelezo kwenye staili ya orodha. Pia, acha nafasi kati ya vifungu tofauti.

Tatu: Ujuzi uanotakiwa

Hii ndio sehemu ngumu ya kuandika kwenye maelezo ya kazi. Ukiweka masharti mengi hapa unaweza mno au usipoweka masharti ya kutosha unaweza kukosa mwajiriwa mzuri.

 • Elimu: Umuhimu wa kuweka kiwango cha elimu kinachohitajika inategemeana na kazi yenyewe. Kama unaajiri Mkuu wa Masoko, basi digrii ya Masoko unaweza ukahitajika. Ila, kama unamuajiri Mwandishi wa Habari, digrii yoyote inaweza  ikakufaa
 • Ujuzi: Kama ni kazi ya chini, ujuzi haina umuhimu sana. Ila, kama kazi ni ya meneja kwa mfano, basi miaka kadhaa ya ujuzi ni muhimu.
 • Character: Mtu mwenye utu wa aina gani ndiyo atakayeifaa hii kazi? Jaribu kutoa maelezo mafupi yatakayo weza kugusia hili. Kwa mfano, ‘je, unaweza kufanya kazi kukiwa na mahitaji mengi kwa wakati mmoja?
 • Utamaduni wa ofisi: Elezea mazingira ya kikazi ya ofisi kwa usahihi. Hii itawasaidia wanaotafuta kazi kuamua kama hiyo kampuni itawafaa.

Nne: Kumalizia

 • Vitu wanavyohitaji kumailisha maombi: Taja wazi unachohitaji kutoka kwa wagombea nafasi, zikiwemo:
 1. CV
 2. Barua inayoeleza kwa nini upewe nafasi hiyo
 3. Mifano ya ujuzi wako wakuandika
 4. Mtihani
 • Mawasiliano: Toa jinsi ya kuwasiliana nanyi pamoja na jina na kazi ya la mtu wa kuwasiliana nao. Pia, eleza kwamba kama wanamaswali yoyote wayafikishe kwa huyo mtu.
 • Wito: Malizia kwa kutoa wito kwa wote wanaona kwamba kazi hiyo inawafaa.

Maelezo mazuri ya kazi yatawavutia wagombea bora

Waajiri wa kitanzania huwa hulalamika kwamba hakuna wagombea wazuri wa kazi kwenye soko la nyumbani. Wanacho shindwa kujua ni kwamba wao pia wanachangia  kuwavutia wafanya kazi bora kwa hiyo nafasi waliyotangaza.

Lazima mwajiri ajitahidi kuhakikisha maelezo ya kazi anayotanganza yanamlenga aina ya mfanyakazi anayemtaka. Pia, maelezo hayo yanabidi yampe mfanyakazi hamu yakufanya kazi nao.

Uko tayari kutafuta wafanyakazi bora?

Tangaza nafasi za kazi na zoomtanzania.com

 

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.