Je ni bora kununua gari kutoka Japan?

  | 2 min read
0
Comments
3587

Watu wanonunua gari kutoka nje wanaongezeka. Wengi wao wananunua kutoka Japan, kwa kuwa Toyota ndio gari maarufu Tanzania. Ila, kabla yaw ewe kujiunga na kundi hii, fikiria faida na gharama zifuatayo utakazokutana nazo:

Uaminifu

Faida kubwa ya kununua gari kutoka Japan ni uaminifu wa kwamba utakuwa unapata gari nzuri. Serikali, ya Japan imelazimisha kwamba magari yote yanayoingizwa Tanzania lazima zifanyiwe uchunguzi wa hali ya juu kabla ya kusafirishwa. Magari yanayofanikiwa yanapata cheti cha Japan Automobile Appraisal Institute (JAAI).

Chaguo nyingi

Kwa kuamua kununua gari kutoka Japan utakuwa na chagua ya magari mengi zaidi ya soko la ndani. Ila, ni muhimu kuhakikisha spea zipo na fundi wao wa gari utakaloamua kununua lasivyo, utajikuta na gharama za juu za utunzaji wa gari yako.

Muda

Kwa wastani, inachukuwa muda wa wiki 6 kuingiza gari kutoka Japan. Pia, kuna fomu nyingi na ufuatiliaji bandarini utakaohitajika kwa sana kuhakikisha gari lako linafika na linatoka kwa usalama. Kwa hiyo, inabidi uwe na muda na subira.

Gharama

Ingawa gharama ya kununua gari yenyewe itakuwa chini ya kuinunua nyumbani, gharama za ziada za kodi za kuingiza na malipo mengine yataongeza gharama yake kwa ujumla sana. Pia, gari za zamani zaidi zina kodi zaidi.  Kwa hiyo, unaweza ukaamua kununua gari ya zamani kwa kuwa ni gharama nafuu ila kodi yake itakuwa ya juu zaidi. Ukitaka kujua zaidi kuhusu kodi, pata taarifa kutoka kwa Beforward.

Fikiria kununua gari kutoka nyumbani

Ukiamua unataka kununua gari, fikiria kuinunua Tanzania kwanza. Kama huna muda na pesa ya kununa gari kutoka Japan (au nchi nyingine yoyote), kuna wauzaji wengi wa magari pamoja na watu binafsi wanaouza magari.

Ila, kama huoni gari yoyote itakayokufaa Tanzania, kampuni kama Beforward na Car Junction zinaweza zikakusaidia kuingiza gari kutoka Japana.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.