Hatua 6 za Kudumisha Betri Yako

  | 2 min read
0
Comments
5422

Kama una gari, kudumu kwa betri yako ni muhimu.

Wengi wetu hatuangalii hali ya betri mara kwa mari. Huwa tunasubiria servisi ya gari au mpaka inapokufa kabisa.

Ila, unaweza kuitunza na kuidumisha kwa kujenga tabia ya kuiangalia mara kwa mara. Aidha, kuna muda ambao ni vyema kutumia fundi wako kwa hili swala, mara nyingine unaweza kuiangalia we mwenyewe.

Kufanya hivyo, fuata maelekezo yafuatayo:

  1. Kama hujui  muonekano wake kabisa, ni sanduku kubwa yenye plastic kwa juu, kwenye boneti.
  2. Kutegemeana na aina ya betri, chunguzi maji ya betri kwa kufungua vifuniko vyake. Maji yake yanatakiwa yawe yanagusa shimo la kujaza maji. Uwe unaangalia maji kila baada miezi 2 au 3.
  3. Toa viunganishi vya betri kutoka kwa termino zake na zisugue na burashi wa waya ikichanganywa na maji kuzisafisha. Inapendekezwa kufanya hivi kila baadaya ya miezi 6 au 8.
  4. Paka girisi ya kutosha kwenye betri kuilinda na kutu.
  5. Kila unapopeleka gari yako servisi, mwombe fundi wako aangalie kiwango cha nguvu (volti) cha betri yako. Betri iliyo na chaji kamili itakuwa na volti 12.5 – 12.6
  6. Ipeleke gari yako servisi mara kwa mara.

Kuanza na betri nzuri ndio mwanzo bora

Iwapo kudumisha gari yako ni muhimu, kuhakikisha kwamba betri yako ni nzuri kwa kuanzia, ni bora. Juhudi zako zote za kuitunza hayata kuwa na mafanikio yoyote kama betri yako iko chini ya kiwango. Kwa hiyo, ni muhimu kununua betri bora kwa bajeti ulionayo. Kumbuka, betri ya gari ni moyo ya gari.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.