Gari Iliyotumika – Namna ya Kuinunua

  | 4 min read
0
Comments
4988

Magari yaliyotumika yanatusaidia kumiliki magari ambayo kwa kawaida, tusingeweza kununua. KWa mfano, Rav4 mpya inaweza ikawa TZS 15m ila iliyotumika inaweza ikauzwa kwa TZS 10m – 12m. Pia, ukinunua gari iliyotumika, unaweza ukainunua hapahapa Tanzania na kuepukana gharama za uzafirishaji kutoke nje.

Ila, magari yaliyotumika yanakuja na msuala mengine. Yanaweza yakahitaji matengenezo mengin kutegemeana na mmiliki wa kabla.

Ila, hii isikukatishe tamaa.  Inabidi uwe makini sana ukiwa unatafuta gari iliyotumika. Hatua zifuatayo zitakusaidia na hilo:

1. Una bajeti ya kiasi gani?

Zaidi ya bei ya kununua gari, kuna gharama zingine zinazokuja kwa kunmiliki gari. Kwa hiyo, kabla ya kununua gari jiuliza, ‘je, bajeti yangu inaniruhusu kumiliki gari?’

Andika orodha ya gharama zinazokuja na kumiliki gari alafu jibu swali hilo. Gharama zitakazokuwepo ni:

 • BIma
 • Utengenezaji wa hapa na pale
 • Spea
 • Servisi
 • Mafuta

2. Jua bei ya wastani

Watu wengine waamua kununua aina ya gari kutokana na maoni ya familia, marafiki na wafanyakazi wenzao. Tatizo ni kwamba kwa kufanya hivi, unaweza ukakosa aina zingine za gari amabazo zingekufaa.

Kwahiyo, ukiwa unaafuta gari anza kufanye utafiti wa awali kujua vitu maalum, kama:

 • Ukubwa wa gari
 • Upatikanaji wa spea
 • Inauwezo wa kubeba watu wangapi?
 • Rangi

Tovuti za matangazo kama ZoomTanzani na Cheki ni sehemu nzuria sana kutafuta magari kwa kuwa unaweza ukatafuta gari kwa bei, aina na mengineyo. Ukishajua gari gani unayoitaka, fanya utafiti wa gari hiyo.

Mwisho wa siku, inabidi ujue:

 • Kari gani itakufaa kwa mahitaji yako
 • Bei ya wastani ya gari hiyo ni ngapi?

3. Aina gani ya gari?

Bajeti yako ndio kitakacho amua aina ya gari utakayo nunua. Na kumbuka, kwenye bajeti hiyo kuna bei ya kununua gari pamoja na gharama zingine za kumiliki gari.

Kwa hiyo, kabla ya kununua gari jiulize:

 • Spea zinapatikana nchini?
 • Inaendana na maisha yako ya sasa?
 • Gharama zake za mafuta unayaweza?
 • Unafikiri kwamba utaimiliki kwa zaidi ya miaka 3?

4. Tafuta gari kwa njia ya kuaminika

Iwapo utamaduni wa Tanzania ina vitu vingi visivyorasmi, ni bora kutumia tovuti zinazoaminika kama ZoomTanzania na Cheki kutafuta gari yako. Pia, unaweza ukatembelea wauzaji wa magari kama hawa. Utajiepusha na watapeli kwa kutumi njia hizi.

5. Uliza maswali

Huwezi kujua kama kutapa taarifa sahihi kutoka kwa muuzaji, ila kuna njia maelezo utakayohitaji.

Kwa hiyo, ukiona gari unayopenda, hakikisha unamuuliza muuzaji maswali ya kutosha kabla ya chochote kile.

Kama huna uzoefu na magari na hujui maswali ya kuuliza, pata ushauri kutoka kwa fundi au mtu mwenye uzoefu zaidi ya magari. Pia, zingatia namna gani muuzaji anajibu maswali yako.

6. Fanya uchunguzi

Baada ya kuridhika na majibu ya muuzaji, muda wa kufanya uchunguzi utakuwa umefika. Kabla ya kupata ushauri wa fundi, kuna baadhi ya vitu unavyoweza kuchunguza mwenyewe:

Umbo la gari:

 • Angalia kama imekwaruzika, imebonyea, inakutu n.k
 • Rangi ya gar nzima inabidi iwe sawa kote
 • Fungua kila mlango alafu ziacha zikiwa wazi. Pia hakikisha zinafunga vizuri
 • Hakikisha paa iko katika hali nzuri.

Glass/Vioo:

 • Hakikisha vioo vyote havijavunjika

Suspension/Saspensheni:

Ingia kwenye gari alafu anaza kudunda ukiwa umekaa. Angalia kama:

 • Ina chezacheza kwa muda au inatulia haraka.

Shuka kwenye gari alafu shikilia kila tairi ya mbele kwa juu, ukizisogeza mbele na nyuma.

Taa:

Hakikisha taa zote zinafanyakazi na hazija vunjika.

Matairi:

 • Hakikisha matairi yote ni ya kampuni moja
 • Kama matairi sio orijino, uliza ni kwa nini
 • Angalia kwenye makali kama kumebonyea, kuna nyufa n.k
 • Hakikisha tairi akiba iko katika hali nzuri

Interior:

 • Viti au kapeti vinamadoa au vimeraruka?
 • Gari ina harufu mbaya?
 • Buti iko katika hali nzuri?
 • Kompartmenti ziko katika hali nzuri?

Breki:

 • Zinafanya kazi?
 • Zimekaza au zimejiachia?

Vifaa vingine:

 • Ukiwasha gari ishara zote nyuma ya steering (idadi ya mafuta kwenye gari, hali ya injini, hali ya joto la injini n.k) zinaonekana?
 • AC inafanya kazi?
 • Redio inafanya kazi?

7. Tembelea Fundi

Kama umeridhika na vyote mpaka hapo umefikia makubaliano ya bei au matengenezo, ipeleke gari kwa fundi ichunguzwe kwa kiundani zaidi.

Hata kama muuzaji anaripoti kutoka kwa fundi mwingine, inapendekezwa kwamba unaipeleka kwa fundi wako. Muuzaji akikataa, usinunue hiyo gari.

8. Makubaliano ya Bei

Baada ya uchunguzi wote kufanyika na fundi wako kuridhika pia, muda wa kukubaliana bei umefika. Wauzaji wengi wanaongeza bei kwa 10% – 25% juu ya bei waliyotayari kukubali.

Kwa mfano, kama gari ni TZS 15m, toa ofa ambayo ni TZS 3m chini ya hiyo bei. Tumia matatizo yoyote uliyokuta kama sababu ya kutoa bei hiyo.

9. Kamilisha kila kitu

Kabla ya kufurahia gari yako mpya, hakikisha zifuatayo yamekamilika:

 • Hati zote za gari na umiliki wake
 • Umetuma pesa kwa kupitia benki na muuzaji amezipokea (usitumie check wala keshi)
 • Bima

Uko tayari kutafuta gari yako?

Sasa, kwa kuwa umepewa vidokezo vya kununua gari iliyotumika, ni muda muafaka kuanza kutafuta. Unasubiri nini? Anza kutafuta gari yako sasa hivi!

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.