Fundi wa Gari – Jinsi ya kupata Fundi Bora

  | 2 min read
0
Comments
1332

Fundi mzuri ni kama daktari mzuri. Ila wengi wetu hatuwi waangalifu wakutosha tukiwa tunamtafuta ‘daktari’ huyu. BAdala yake, tunamtumie yule alliyependekezwa na familia au marafiki. Tatizo ni kwamba huwa hawawi makini na gari zetu kama jinsi walivyo makini na gari za wateja wao wa zamani.

Pia, fundi wengi si waaminifu na wala si wataalam wakuthibitishwa.

Kwa hiyo, tumia maswali yafuatayo kumtafuta ‘daktari’ bora wa gari yako:

1. Wanautaalam na magari ya kampuni ya gari yako?

Gereji nyingi Tanzania zinautaalam na magari ya Toyota, Nissan na Honda. Kama una gari tofauti kama Mini Cooper, Jeep au mengineyo, ni muhimu kumtafuta fundi mwenye ujuzi wa magari hayo.

2. Wana sera ya uthibitisho?

Kabla ya kukubali kumwachia fundi gari yako, muulize kama gari haijatengenezeka au baada ya siku mbili tatizo inajirudia, inakuwaje? Fundi mwenye hakika na kazi yake atakurudishia pesa yako au ataifanyia kazi gari yako bure kama haijakamilika baada ya yeye kuifanyia kazi mara ya kwanza.

3. Tumia intaneti

Tumia rasilimali kama orodha ya biashara ya ZoomTanzania kutafuta fundi muaminigu kwenye mji wako. Pia, fundi anayejitangaza kupitia ZoomTanzania, Facebook, Instagram n.k anajitangaza kupata biashara na pia kuonyesha kwamba anaaminika.

4. Inapatikana/wanapatikana wapi?

Watu wengi wanasahau kufikiria hili swala wakimchagua fundi. Eneo ya fundi wako ni muhimu sana, hasa kwa mji mkubwa kama Dar ambapo akiwa mbali na malazi yako, ni rahisi kupata uvivu wakupeleka gari yako kwako. Pia, gari yako ikipata matatizo makubwa na hata kuwaka hai waki, kuisafirisha kwenda kwa fundi wako inaweza ikawa gharama kubwa sana. Kwa hiyo, zingatia hii ukiwa unamchagua fundi.

5. Pata ushauri kutoka kwa marafiki na familia

Iwapo ni muhimu kufanya utafiti, kupata mapendekezo kutoka kwa mtu unaye muamini ni mwanzo mzuri. Pia, ukimtumia fundi wa familia/marafiki na ukamwambia ‘fulani alipendekeza nije kwako’ hawataka kumpoteza mteja huo

Pia, ni muhimu kupata mapendekezo kutoka kwa watu wenye gari kama ya kwako.

6. Mjaribishe kabla ya kumpa kazi nzima

Ukishamchagua fundi wako, wajaribishe na tatizo ndogo alafu tathmini uzoefu wao. Mawasiliano yao yakoje? Wanamaliza kazi kwa muda uliokubaliwa? Kama unaridhika na kazi yao, basi fundi wako kapatikana!

Sasa, unasubiri nini? Anza kumtafuta fundi wako sasa hivi!

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.