Faida 5 za kuajiri kwa kupitia Shirika La Ajira

  | 4 min read
0
Comments
979

Wafanyakazi wabaya ni gharama kwa kampuni. Ila, kumpata mfanyakazi mzuri ni ngumu duniani, hasa Tanzania ambapo unaweza kukuta:

 • Maombi ya kazi mengi kutoka kwa watu wasiyo na sifa ya kazi hiyo
 • CV zimejaa na udanganyifu
 • Kazi zinazo hitaji interview tu zinawependelea watu wanaojiamini lakini huenda wakakosa ujuzi
 • Sheria za kuajiri zinafanya iwe ngumu na gharama kubwa kumfukuza kazi mtu anayeshindwa kazi.

Sasa, biashara zilizopo Tanzania zita suluhisha matatizo ya kuajiri kivipi?

Shirika za kuajiri zina uwezo wa kutafuta watu wenye vipaji vilivyohitimu na vya kipekee.

Kuajiri ni nini hasa?

Kuajiri unaweza kuelezwa kama kutafuta na kusaka mgombea bora aliyetiimu kwa ajili ya kujaza nafasi ya kazi, ndani au nje ya kampuni.

Lengo ni kuajiri kwa gharama nafuu na kwa wakati. Mchakato wa kuajiri ni pamoja na kuchambua mahitaji ya kazi, kuwavutia wafanyakazi kwa kazi hiyo, kuchunguza waombaji pamoja na kuwachagua.

Kwa mfano, kampuni kubwa kama Vodacom inaweza ika ajiri ndani au nje ya kampuni, kwa kutegemea mahitaji ya nafasi ya kazi iliyopo. Vodacom inaweza ikajaza hiyo nafasi kwa kupitia idara yao ya rasilimali watu au kwa kutumia shirika la kuajiri. Kawaida, shirika la kuajiri itajaza hiyo nafasi kwa kasi na ufanisi zaidi.

Zifuatayo ni sababu 5 kuu za kutumia shirika la kuajiri kutafuta wafanyakazi:

Kazi yao kuu ni kutafuta wafanyakazi bora

Shirika za ajira zina utaalamu.

Matokeo yake ni kwamba shirika za kuajiri zina mitandao mikubwa  zinazowawezesha kuwafikia watu wengi zaidi watakao faa nafasi ya kazi iliyotangazwa, kuliko idara ya rasilimali watu.

Pia, kwa kuwa nafasi za kazi ni chache, nafasi zikitangazwa watu wengi sana wanatuma maombi. Hii inaweza ikafanya idara ya rasilimali izidiwe. Kwa kuzidiwa, idara hiyo inaweza ikakosa wafanyakazi wazuri kwa vile hawakuwa nauwezo wa kupitia maombi yote.  Tatizo hili halipo kwa shirika za kuajiri kwa kuwa wanategemea hili kutokea na wameshajipanga na kujua mbinu za kupambana hili swala.

Shirika za kuajiri nzuri zina utaalamu kwenye sekta maalum na zinajua maendeleo ya sekta hiyo. Wanajua:

 • Wafanyakazi na makampuni muhimu.
 • Mishaara ya nafasi ya kazi mbalimbali ndani ya sekta hiyo.
 • Ukuwaaji wa wafanyakazi ndani ya sekta hiyo
 • Ujuzi na utu bora kwa kazi iliyotangazwa.

Kwa hiyo, kama biashara yako haina muda wa kufanya utafiti juu ya sekta maalum, shirika la kufanya kazi huenda ikawa masikio na macho yako kuhakikisha kwamba unapata mfanyakazi anayeiweza kazi uliyotangaza.

Upatikaniaji wa wafanyakazi bora

Biashara nyingi Tanzania zinalalamika kwamba hakuna waombaji kazi wa kutosha wenye sifa za kujazi nafasi za kazi.

Ila, mara nyingine tatizo si ukosefu wa waombaji kazi wenye sifa bali ni kwamba hawa hawaombi kazi kupitia njia za kawaida (matangazo magazetini, kupitia tovuti ya kampuni n.k)

Shirirka za kuajiri zina mitandao mikubwa na zina hifadhi CV za mamia ya waombaji kazi weneye sifa nzuri. Baada ya kujua mahitaji ya nafasi ya kazi, shirika hizi zinakupatia waombaji wenye sifa zinazofaa hiyo kazi.

Kwa hiyo, kwa kutmia shirika la kuajiri matokeo yake inabidi iwe kwamba waombaji wamesha chaguliwa kuwa na sifa zote zinazohitajika na hivyo, kustahili interview.

Kwa kufanya hivi, kampuni inokoa muda wa kutafuta, chambua na kuajiri waombaji.

Gharama nafuu

Kuajiri wafanyakazi ni gharama kubwa na gharama huongezeka kama ukikosea kuajiri.

Utafiti unaonyesha kwamba wafanyakazi hovyo wanachukua asilimia 17 ya muda wa meneja. Pia, hapa Tanzania shirika za ajira zimefanya kumfukuza mtu kazi iwe ngumu.

Na hata kama mfanyakazi mwenyewe anaamua kuondoka, atakayekuja kujaza nafasi yake itabidi apewe mafundisho na meneja.

Yote haya hayana faida na yanachukua muda mwingi kwa kampuni yako. Kwa hiyo, biashara yako inaweza isitake kutumia pesa kwa ajili ya kuajiri, ila inabidi uzingatie muda utakaokosa kuongeza mapato ukiamua kuajiri mwenyewe bila kupitia shirika la kuajiri.

Inaokoa muda

Shirika la kuajiri ina fanya zile kazi zote zinazochosha na kuchukua muda kwenye mchakato wa kuajiri. Kuna:

 • Kufanya ukakuzi na kuwasiliana
 • Kufanya majaribio ya ujuzi
 • Kuandaa interview

Kwa hiyo, huna haja ya kutumia muda wako wa kuongeza mapato mpaka umeletewa orodha ya waombaji kazi bora.

Haina mashaka

Shirika za kuajiri ambazo ni bora zaidi zinajiamini kwa kiasi kikubwa kwamba watakutafutia mfanyakazi mwingine kama chaguo lao la kwanza alishindwa kazi.

Shirika za kuajiri kaka ZoomTalent zitafanya utafiti wa baada ya kuajiri kuhakikisha  mfanyakazi uliyemwajiri anafanya vizuri.

Wafanyakazi bora wanakusubiri wewe!

Kufanya kazi na shirika la kuajiri itabadilisha mtazamo wako wa waombaji kazi Tanzania. Ingawa tunaamini kwamba Tanzania haina wafanyakazi wazuri wa kutosha, kuna wafanyakazi wengi Tanzania wenye motisha na uwezo wanaosubiri nafasi ya kukuonyesha uwezo wao.

Hutuamini?

Wasiliana na shirika letu la kuajiri: recruitment@zoomtanzania.com

* Shirika letu la kuajiri inatumia miaka mingi ya kufahamu changamoto za waajiri, shirika za kuajiri na washauri wa rasilimali watu kuitafutia biashara yako wafanyakazi waliyohitimu na waliyo bora.

 

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.