Chapa kazi, cheza kwa bidii: Sababu 5 za kwenda Likizo

  | 4 min read
0
Comments
1719

Iwapo unamiliki biashara ndogo, ni mzazi, mwanafunzi au mfanyakazi wa kawaida – inabidi ujiwekee muda wa kupumzika.

Kwenda likizo inatusaidia kujisikia vizuri pamoja na kuwa wafanyakazi bora zaidi. Ingawa imani maarufu ni kwamba ukichapa kazi zaidi utafanikiwa zaidi, ukweli ni kwamba unaweza kuchapa kazi na kupumzika. Sana sana utafanikiwa zaidi kwa kufanya hivyo.

Kwa bahati nzuri, tunaishi kwenye nchi iliyojaa urembo na yenye sehemu nyingi za kwenda likizo. Pia, kama umeajiriwa, unapata siku 28 za kwenda likizo.

Ila, kabla ya kuanza kuwa na ndoto ya sehemu utayokwenda ukichukua likizo yako, zifuatayo ni sababu 5 za kwenda likizo.

1. Kupunguza Mkazo

Wengi tunafikiri kwamba kuwa na mkazo ni dalili ya kuchapa kazi. Ila, ukiwa na mkazo kali sana inachangia magonjwa sita zenye uwezo wakuua: ugonjwa wa moyo, kansa, magonjwa ya mapafu, ajali, cirrhosis ya ini na kujiua.

Kwa bahati mbaya, wengi wetu hatuwezi kuepukana na mikazo maishani. Ingawa unaweza kuzipunguza kwa kwenda gym na kula vizuri, kama unaishi kwenye mji kama Dar es Salaam ikiwa na foleni, gharama kubwa za kuishi na vitu vingine vya vitakavyo kukera kila siku, lazima utazidiwa.

Kwenda likizo, likizo ya ukweli ambayo unajitoa katika maisha yako ya kila siku na kupumzisha akili yako, inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana.

Kiukweli, badala ya kuchukua likizo ndefu mara moja kwa mwaka ni bora uende kwenye likizo fupi ya siku 3 au 4 mara kwa mara kwa mwaka. Hii itakuwezesha kupunguza mkazo kwa mfululizo ndani ya mwaka. .

Sehemu ya kwenda: Kama unaishi mjini, tuseme Dar es Salaam, kuna hoteli nyingi zilizopo ufukweni unazoweza kutembelea. Ila, kama unataka kutoka nje ya nchi kabisa, nenda Zanzibar au Bagamoyo.

Kama huna pesa nyingi ya kutumia, baki nyumbani alafu tembea mara kwa mara au nenda kwenye fukwe ya umma.

2. Panua mtazamo wako

Kwa kuwa tunaweka umakini kwenye maisha yetu ya kila siku, ni ngumu kuona matatizo ndani ya maisha haya na ni ngumu zaidi kutafuta suluhisho.

Ukienda likizo, hasa kama unasafiri kwenda mkoa, mji au nchi nyingine, unajitoa katika maisha yako ya kila siku na unajiingiza kwenye nafasi iliyotofauti na unachokijua. Hii itakusaidia kutafakari vitu mbalimbali katika maisha yako ya kazini na kibinafsi na kuona nini cha kubadilisha na nini cha kubakisha. Pia, kwenda likizo itakusaidia kufanya hivi vilevile.

Kama unaendesha biashara, nenda likizo ili ujue kama biashara inaweza kujiendesha yenyewe. Kama haiwezi, gazeti la Inc inasema kwamba “inabidi uongeza muda wa kuwawezesha wengine, kuweka mifumo bora zaidi na kuongeza uwajibikaji”.

Sehemu ya kwenda:  Kuna wakala wa usafiri wazuri sana watakaoweza kukusaidia kutafuta sehemu nzuri ya kwenda likizo, iliyo ndani ya bajeti yako.

Tunarudia tena, kama hutaki kutumia pesa nyingi, unaweza ukaenda kwenye likizo iliyotofauti kidogo na ukajitolea. Au, tembelea mkoa ambao hujawahi kufika.

3. Ongeza Ubunifu

Wengi wetu tumeona jinsi gani mfanyakazi mwenzetu amerudi kutoka likizo akiwa amebadilika kabisa na jinsi alivyokuwa kabla ya kwenda likizo. Badala ya kuwa na uchovu na kutokuwa na motisha, amepata msisimko na ana mawazo mazuri ya kuboresha kampuni.

Ukweli ni kwaba, ubongo ukipumzika ina pokea taarifa kwa ukamilifu zaidi na inaweka malengo kufanya mazoezi kupata ujuzi zaidi, pamoja na kutatua matatizo (bila wewe kujua). Matokeo yake ni kwamba unaboresha mawazo na ujuzi wako; unaishia kufanya kazi vizuri zaidi na pia, unakuwa mtu mzuri zaidi wa kuwa naye.

Sehemu ya kwenda: Kuongeza ubunifu, tembelea sehemu za sanaa na utamaduni kwa muda wako.

4. Ongeza Furaha

Wafanyakazi wenya furaha wanaongeza faida. Jua kwa nini hapa.

Sayansi inahusika hapa. Ukiwa likizo, mwili wako inatoa hormoni ya furaha ya serotonin. Hii ina pumzisha viwango vya cortisol (hormone ya mkazo). Mwisho wa siku, horomoni nzuri zinalazishwa ndani ya mwili wako na hii ina changia mtazamo wako wa kimaisha.

Sehemu ya kwenda: Sio lazima likizo iwe ya ghara kubwa au kwa muda mrefu ili iwe na faida. Bora uende kwenye likizo ya wikiendi kwenda sehemu isiyo na gharama kubwa badala ya kutokwenda kabisa. Lengo ni kujitoa kabisa na maisha yako ya kila siku.

5. Utendaji Bora

Utafiti uliofanyiwa na Florida State University ulionyesha kwamba watu wanaoenda likizo wanafanya kazi zaidi na wana nafasi kubwa zaidi ya kupandishwa cheo na kufanikiwa kuliko watu wasioenda likizo.

Hii inathibitisha kwamba ukijipatia muda wa kupumzika baada ya kuchapa kazi kwa muda, utaboresha utendaji kazi wako.

Lazima likizo lipewe kipaumbele

Kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba ukipumzika, utendaji kazi wako ni bora na kwa kasi zaidi.

Kujipumzisha si fadhili, ni lazima. Na kwa kuwa tumekuonyesha umuhimu wa kwenda likizo na faida yako kwa afya yako ya kimwili na kiakili, pamoja na kwenye utendaji kazi, weka kipaumbele kwenye kuomba likizo.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.