Baa 10 Bora za Mtaani

  | 4 min read
0
Comments
2993

Njia maarufu ya kujipumzisha Tanzania ni kwenda kwenye baa yako upendayo kukutana na maraafiki na kujipatia kinywaji baridiiiiiiiiiiiiiiii.

Sasa, Dar Es Salaam ina mamia ya baa na kuzitembelea zote itashindikana. Ila, kuna mengine ambayo ni  maarufu kuliko mengine ambazo unapaswa kwenda. 

Hizi ni:

Didis iko Masaki na inajulikana kwa kiti moto (nyama ya nguruwe) yake. Mandhari yake ni kati ya tulivu na fujofujo. Kunajaaga muda lanchi na wikiendi kuanzai saa tisa mchana.

Chakula ni cha kinyumbani na bei zake ni nzuri. Wateja wengi wanaonenda pale ni wenyeji.

Jua zaidi kuhusu Didis hapa.

Jackies inaangaliana na Didis. Inahistoria ya zaidi ya miaka 20 na itaendelea kuwepo.

Inajulikana kwa vyakula vyao vya Rump Steki na Makange pamoja na Vuruga. Bei za vinywaji ni nafuu na mandhari yake ni ya kitulivu zaidi. Pia, ni sehemu nzuri kuangalia mpira.

Jua zaidi kuhusu Jackies hapa

 • Lukas Bar & Restaurant, Masaki

Lukas ina hadhi ya juu zaidi ya Jackies na Didis, na ipo 400m kutoka baa hizo. Mandhari yake ni ya mgahawa wa nje zaidi. Ina ukubwa mara mbili ya Jackies na ina mapambo zaidi.

Pia, aina nyingi zaidi ya vinywaji, baa mbili, pool tebo, samaki, viti vingi zaidi na bendi inapiga kila ijumaa.

Jua zaidi kuhusu Lukas hapa

 • Kruzin, Mikocheni B

Ina vyakula vingi vya nyumbani (makange, mbuzi choma, ugali, mbavu za kiti moto n.k) na ni sehemu nzuri kupata mlo wa jioni na kukutana na washkaji. Kuna nafasi ya kutosha na mandhari yake ni ya kitulivu zaidi. Ila, kunachangamka kwenye wikiend.

Jua zaidi kuhusu Kruzin hapa

 • Rainbow Social Club, Mbezi Beach:

Rainbow ni baa nyingine ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 20. Iko Mbezi, ambayo ni kaskazini mwa Dar na ni baa inayotembelea na weneyeji wa huko hasahasa. Kihistoria, ni sehemu ya kwenda na familia. Ila siku hizi, inavutia vijana wengi zaidi kwa kuwa na DJ kwenye siku za ijumaa pamoja na Karaoke kila jumatano.

Zaidi ya hapo, chakula chake, hasa Kiti Moto spesho na Kiti Moto yenye asali ni balaaaa!

Jua zaidi kuhusu Rainbow hapa

 • Waungwana, Sinza

Si kitu cha kushangaza kuona watu wakipigana kwenye moja ya baa zilizo changamka zaidi Dar. Watu wanaenda Waungwana kulewa na kucheza muziki. Muziki unaopigwa ni ya kiafrika na za zamani. Wateja wengi wa pale ni wa kidha cha chini, ila kama unatafuta sehemu ya kufurahia na kujiachia, hapa ndio penyewe!

Jua zaidi kuhusu Waungwana hapa

 • Kona Baa, Sinza

Ni moja kati ya sehemu chache zilizopokea wateja kwa wakati wote. Ni kuku choma yao ni ya kipekee! Watu wengi wanafika hapa wakiwa wanatafuta chakula kabla ya kwenda nyumbani usiku wa manane. Hawapigi muziki yoyote ila iko jirani na klabu.

 • Nguruko, Makonde

Baa hii nayo ni ya miaka mingi sana. Umaarufu ni kutokana na mbuzi yake ya kipekee, pamoja na kuku na kiti moto chake.

Wateja wengi wa kila siku wanapita pale kila wikiendi wakiwa na marafiki na familia.

 • Hongera Bar, Bamaga-Sinza

Wateja wa baa hii ni watu wazima zaidi, wenye miaka 30 -50. Wanaenda pale kula Ugali na Mbuzi, na kuangalia taarifa ya habari.Ila, vijana nao wanafika siku hizi.

Jua zaidi kuhusu Hongera Baa hapa

 • East 24, Mikocheni

Kati kati ya wiki, East 24 ni sehemu iliyotulia na watu huenda pale kuangalia mpira au kupata kinywaji kitulivu. Ila, wikiendi ikifika inakuwa sehemu ya kucheza muziki wa bendi (ijumaa) au nyimbo kali za 1990 – 2000s (jumamosi).

Jua zaidi kuhusu East 24 hapa

Baa Nyongeza

 • Break Point, Kinondoni

Kwa kifupi, ni Hongera Bar ya hadhi ya juu.

 • Hunters Kinondoni

Hii ni baa inayonyesha mpira kwenye wikiendi. Pia, wanapiga muziki kwa ndani kwenye usiku wa wikiendi.

Jua zaidi kuhusu Hunters hapa

 • Rudys, Bahari Beach

Rudys ni sehemu ya kula zaidi ya baa na wanajulikana kwa nyama yao ya kuchoma (soseji, mbavu za kiti moto, kuku, t-boni). Pia, vinywaji vyao sio bei mbaya. Ni maarufu kwa familia, vijana na watu wazima. Mandhari yake ni ya kitulivu zaidi.

Jua zaidi kuhusu Rudys hapa

Baa haziishi

Kama kuna kitu ambacho Dar na Tanzania kwa ujumla zinazo kwa wingi, ni baa. Kwa hiyo ukitaka kutafuta sehemu zingine bora, pitia orodha ya biashara ya ZoomTanzania.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.