Apartment ya Kupanga: Maswali ya kuuliza

  | 4 min read
0
Comments
563

Ikija kwenye swala la kutafuta apartment au nyumba, epuka na kupenda sehemu mara moja. Tatizo ni kwamba ukipapenda ghafla hutaweza kuona mapungufu yake. Ndio, kuona na mtazamo mzuri ni vizuri ila, ikija kwenye maswala sehemu utakayoishi, kuwa na mtazamo mzuri tu unaweza ukaingiza pabaya.

Kwa mfano, tuseme umepata apartment safi Upanga ya vyumba viwili na ipo kwenye bajeti yako na karibu na migahawa yote unazozipenda. Ila, unafanyakazi Tegeta, ambayo ina umbali wa 20km kutoka Upanga na hivyo, unaishia kutumia masaa matatu kwenye foleni kila siku. Iwapo apartment hii ni nzuri n ndani ya bajeti yako, safari ya kwenda kazini na kurudi itakuwa kero kubwa!

Bahati nzuri, ukiwa unafanya tathmini ya apartment za kukodi, kuna maswali kadhaa unayopaswa kumuuliza mwenye nyumba yatakayo kusaidia kuamua kama patakufaa:

1. Majirani wakoje?

Iwapo unahamia kwenye ghorofa la apartment au kwa ujirani mpya, kupatana na majirani itarahisisha maisha yako. Kwa hiyo ni muhimu kuelewa ni watu wa aina gani utakao ishi nao, na pia kuangalia kama maisha yao yanaendana na ya kwako.

Kwa mfano, kama wewe ni mtu wafanya sherehe nymbani mara kwa mara ila majirani wako ni watulivu, hapo sio pakuhamia.

2. Umeme, maji na gesi yanahesabiwa kwenye kodi?

Kwa kifupi, itabidi ujue kodi inalipia gharama zipi. Hii itakusaidia kujua kama una uwezo wakuishi hapo.

3. Mtandao wa simu na intaneti ukoje?

Ni muhimu kujua kama mtandao ina nguvu au ni dhaifu. Wengi wetu tunatumia simu zetu kuwasiliana na kufanya kazi kila siku. Kwa hiyo, mtandao mbovu itakuwa kero huku mbele.

4. Mkataba unasemaje?

Kitu cha kwanza kabla ya kutoa ofa ni mkataba. Hati hii inaeleza vigezo na masharti zamwenye nyumba.Itakuwa na maelezo kuhusu:

 • Kodi
 • Adhavu ya kuvunja mkataba
 • Kodi inalipia gharama zipi
 • Sera ya kupandisha kodi (atakujulisha miezi mingapi kabla)

5. Msimamo wako wa wanyama wa nyumbani ni nini?

Kwa kuwa watanzania wengi sio wapenzi wa wanayama wa nyumbani, wengi wanyama wa kinyumbani (ambao sio mifugo).

Kwa hiyo, kama unawanyama wa nyumbani unafikiri ungependa kuwa nao huko mbele, ni muhimu kujuwa kama utaruhisiwa.

6. Msimamo wako juu ya wageni ni nini?

Hii muhimu kwa watu wanaokodi apartment kwenye jengo la ghorofa. Iwapo, wenye nyumba wengi sio wakali kwenye swala hii, ni muhimu kuwa na uhakika.

7. Matengenezo ni jukumu la nani?

Inabidi ujue:

 • Kama wewe ndio mwenye jukumu la kufanya matengenezo yakihitajika (dokezo: kawaida jukumu hii sio ya kwako mradi sio wewe aliyevunja kinachohitajika kutengenezwa)
 • Kwa wastani, inachukua muda kufanya matengenezo?
 • Makubaliano ya malipo yanakuaje?

8. Maswala ya parking ni vipi?

Hakikisha unaulizia parking, hata kama huna gari. Ni vizuri kujua kwa ajili ya wageni.

Kama una nia ya kukodi nyumba, kawaida kutakuwa na nafasi ya gari moja. Ila, sehemu nyingi, haswa zikiwa na wapangaji wengi, zinaweza zikawa na nafasi barabarani tu. Ukikuta kwamba ni hivi, uliza kama walinzi wa magari wapo.

9. Kuna vitu vingine vinavyokuja na apartment?

Zaidi ya maji na umeme, mwenye nyumba anaweza akakupa faida zingine zitakazoweza kuchangia maamuzi yako. Kwa mfano fenicha, jenereta, bwawa la kuogelea, ulinzi n.k

Kwa hiyo, maswali kama:

 • Kuna jenereta?
 • Kuna fenicha kwenye apartment?
 • Kuna huduma za usafi?

10. Eneo ina usalama?

Ni muhimu kuwa na usalama nyumbani. Kwa hiyo, uliza maswali kuhusu usalama kwenye eneo hiyo, kama:

 • Matukio ya wizi yanatokea mara kwa mara?
 • Kuna walinzi/ulinzi kwenye jengo?
 • Kuna usalama kutembea usiku?

Aidha, kama wewe ni mwanamke asiye na gari, ni muhimu kujua kama kuna usalama kutembea usiku au kama unahitaji kuchukua tahadhari za usalama.

Dokezo: Zaidi ya kuongea na mwenye nyumba, tembea tembea kwenye eneo hiyo na uwaulize wenyeji kuhusu hiyo sehemu. Hapo ndio utajua ukweli.

Usiache hisia zako zichague apartment yako

Kutafuta apartment ni kazi kubwa na utafurahi sana ukiona sehemu unayopenda. Ila, kuwa mtulivu na hakikisha unafanya uchunguzi wa maana kwa vile ukishasaini mkataba, ni ngumu sana kujitoa.

Kuanza kutafuta apartment, pitia apartment zinazotangazwa ZoomTanzania.

Iman Lipumba
A digital storyteller, experienced in creating content that improves website visibility on search engines, enhances the user experience, and nurtures brand loyalty. With a background in the social sciences, an expert in researching complex ideas, and communicating them in engaging language to multiple audiences.