Njia 5 Nzuri za Kusherekea Sikukuu ya Pasaka na Uwapendao

  | 3 min read
0
Comments
1493
sikukuu ya pasaka

Moja ya vitu vizuri kuhusiana na sikukuu nyingi, ni jinsi zinavyotengeneza  kumbukumbu na furaha zinazobaki kwa muda mrefu katika maisha. Na moja ya sikukuu ambazo zinabeba tamaduni za kipekee ni Pasaka. Ni sikukuu inayofuata baada ya mfungo wa waumini wa dini ya Kikristu na ni siku ya mapumziko kwa watu wa dini zote.

Kuna mengi ya kufurahia na uwapendao  katika msimu huu wa sikukuu. Ikiwa unafikiria namna ambavyo utasherehekea na uwapendao , nini cha kufanya, maandalizi na zawadi za kutoa, basi hizi ni namna chache unavyoweza kusheherekea.

1. Andaa Chakula cha Pamoja

sikukuu ya pasaka andaa mlo wa familia pamoja

Katika kujumuika na uwapendao  msimu wa sikukuu hii, andaa chakula cha pamoja  kinachopendwa zaidi na watu wote. Pilau? Labda, lakini unaweza kufanya kitu cha tofauti msimu huu. Nyama choma na ndizi ama viazi, ama na mchanganyiko wa chakula kingine unaweza  kuwa kiburudisho kizuri kwa ajili ya Pasaka hii. Wakati wakubwa wakiandaliwa nyama choma na vinywaji, unaweza kuwaandalia watoto chakula laini zaidi kama ndizi rosti na pilau kidogo. Kwetu uswahilini sherehe hainogi  bila pilau.

2. Andaa Mchezo Utakao Waleta Karibu

Siku kama hizi za shehere ni vizuri kuweka majukumu mengine mazito pembeni  na ku-enjoi pamoja na uwapendao. . Yapo mengi yanayoweza kuwleta watu karibu, michezo, filamu ama mazungumzo yaa furaha/ucheshi. Michezo kama mtu kati, kuchagua mtu na kumuuliza maswali magumu ni mchezo mzuri unaochangamsha. Kuangalia  filamu nzuri za vichekesho ama muvi ya mateso ya Yesu Kristu kama ukumbusho wa sababu ya siku ya Pasaka kunaweza kuwa kitu cha kufanya na uwapendao. Katika kuchagua muvi ni vizuri kuzingatia muvi yenye maadili na mafunzo inayoweza kuangaliwa na watu wa rika lote.

3. Toa Zawadi na Pongezi

sikukuu ya pasaka toa zawadi

Fanya Pasaka hii ya kukumbwa na kila mtu kwa kutoa pongezi na zawadi. Hakikisha umeandaa kitu cha kukumbukwa na wana familia yako. Zawadi inaweza kuwa kitu chochote kitachobeba kumbukumbu kwa mpokeaji na mtoaji. Unaweza kuandaa vifaa vya shule kwa watoto na kuwapatia siku ya Pasaka kama zawadi. Mama anaweza kupewa doti ya vitenge, na baba anaweza kuzawadiwa saa ya mkononi.  Kwa zawadi za mavazi tembelea zoomtanzania na fanya chaguo lako kua rahisi kutoka kwenye bidhaa nyingi zilizopo.

Sio zawadi za vitu tu. Hata maneno mazuri ya pongezi na shukrani kwa uwapendao  yanaweza kuwa zawadi tosha. Andaa neno la shukran kutoka moyoni.i. Pia unaweza kuandaa neno ama tafakari nzuri itayoweza kumgusa kila mtu na kufanya siku hii kuwa ya pekee na chachu ya mabadiliko katika maisha yake.

4. Andaa Michezo ya Watoto

Pasaka na familia haitakua ya furaha kama watoto hawapata mahali pa kucheza. . Unaweza kupata vifaa vya michezo ya watoto kutoka ZoomTanzania , mipira ya kuchezea, nk. Unaweza pia kuwafundisha watoto michezo kama ngonjera na ngoma, michezo ya kitamaduni nk. Pia, unaweza kutambulisha michezo mipya ya watoto, mfano tamaduni ya kuficha mayai yenye zawadi katika moja ya sehemu ya nyumba na kuwaacha watafute (Easter Egg Hunt). Hii ni nafasi ya kufurahi na kujifunza mambo mapya  wakati wa Pasaka.

5. Pumzika — Usisahau Kupiga Picha

sikukuu ya pasaka pumzika piga picha

Hakikisha unapata muda wa kupumzika baada ya maandalizi yote ya kuisherehekea Pasaka. Jumuika na familia na marafiki katika maongezi na mapumziko baada ya chakula cha mchana. Muda huu watu wanaweza kuwa huru kupumzika na kubadilishana mawazo huku wakiendelea kupata vinywaji nk. Wakati huu pia usisahau kutengeneza kumbukumbu nzuri. Picha hutunza kumbukumbu. Hakikisha pasaka hii haikosi picha. Kumbuka muda si mrefu utarudi  ofisini kuendelea na majukumu ya kazi, hivyo picha zitakufanya utabasamu ukikumbuka jinsi ulivyosheherekea Pasaka yako.

 

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media