Siku ya Valentine: Namna 5 za Kufurahia bila Gharama Kubwa

  | 3 min read
0
Comments
2037
siku ya valentine siku ya wapendanao

Sikukuu ya Valentine imekaribia, ikimaanisha migahawa, wauza maua na karibu kila kitu kinachoweza kudhihirisha upendo kitapanda bei. Na kiukweli, kutokana na kugeuza siku hii kuwa kama biashara, inamaanisha watu wengi watatumia gharama nyingi sana kuliko kawaida kuonesha upendo.. Kama hujasikia, kuna hoteli Tanzania inatoza hadi shilingi Milioni 15 kwa usiku mmoja wa Valentine.

Lakini, ili ushiriki na umpendae katika siku hii ya wapendanao, si lazima umpe zawadi, au kumtoa mlo wa jioni wa gharama ya kutisha. Kuna vitu vingi mnaweza kufanya pamoja bila gharama kubwa na vikabaki kama kumbukumbu nzuri siku hii.

  1. Jumuikemi Kwenye Mlo wa Jioni Pamoja

siku ya valentine jumuikeni mlo wa pamoja jioni

Pamoja na kupeana zawadi, watu wengi hupenda sana kula mlo wa pamoja siku ya Valentine.. Baadhi ya migahawa inaweza kupandisha bei wakati huu, lakini mingi hubaki na bei ya wastani na unayoweza kumudu vyema katika siku hii. Lakini kama utaona gharama zimekuwa kubwa sana, kuna namna nyingi mnaweza kufurahia mlo wa jioni pamoja bila kutumia gharama kubwa, mfano:

  • Kufurahi na umpendao kwa chakula utakachokiandaa mwenye nyumbani.
  • Kuagiza takeaway (chakula cha kuagiza) kutoka kwenye mgawaha wa bei nafuu.
  1. Fanyeni Matembezi

Japo kutoka kwenye kula mlo wa jioni ni kawaida sana kwa siku hii ya wapendanao, lakini si lazima sana. Ukiwa mko katika bajeti, mnaweza kuamua kufanya matembezi ya pamoja jioni na kufanya shughuli za gharama rahisi kama:

  • Kutembelea nyumba za sanaa
  • Kwenda kufanya manunuzi ya zawadi jioni, mfano Mlimani City
  • Kutembea tu wakati wa Jioni kwenye sehemu tulivu yenye miti ama maua.
  1. Fanyeni Iwe  Siku ya Muvi

siku ya valentine fanyeni iwe siku ya muvi

Moja ya kitu kinachoweza kukamilisha siku ya wapenndanao ni kuangalia muvi itakayowaunganisha pamoja. Kama mna muda mzuri, mnaweza mkaenda kumbi za Sinema kama Mkuki au Mlimani City na mkaweka kumbukumbu nzuri. Lakini kama hamtakuwa na muda wa kutosha (hasa ukizingatia mwaka huu imeangukia siku ya kazi), basi hakuna kitakachoharibika. Nunua vitafunwa vichache vya jioni, bisi (popcorn), mvinyo kidogo kisha fanyeni siku hii kuwa ya kukumbuka kwa kuangalia muvi nyumbani.

  1. Rudieni Siku Yenu ya Kwanza Ilivyokuwa.

Mnakumbuka mlipoanzia? Kuna uwezekano mkubwa siku hii haikuwa ya gharama kubwa, lakini bado ni ya kuvutia sana. Ikiwa mlikula Samaki na Chipsi huku mkiangalia jua likizama, kwa nini msirudie tena siku hiyo? Hata kama mna watoto, mnaweza kuwachukua na kwenda nao – bado itabakia kuwa siku ya kipekee na watafurahi kujumuika na kukamilisha maana halisi ya siku ya wapendanao

  1. Ikiwa Ni Lazima kwenda Sehemu Nzuri, basi Chagueni Sehemu Nafuu

siku ya valentine chagua sehemu nafuu

Kweli. Mnaweza mkawa mlisubiri sana siku hii na mmetamani kwenda sehemu ya kuwavutia wote wawili. Kama mtaamua kweli kutoka basi anzeni kwa kuchagua hoteli zenye bei nafuu  . Mnaweza kupiga siku kwenye hoteli na kuulizia mapema na kufanya hifadhi (booking). Cha msingi hapa ni kutokuchagua sehemu moja tu na kulipia iyo iyo. Kuna sehemu nyingi na zinaweza zikawapa bei nzuri katika  siku hii ya wapendanao

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media