Krismasi na Familia: Dondoo 5 za Kufurahia Msimu Huu

  | 3 min read
0
Comments
905
sheherekea sikukuu familia

Sikukuu ya Krismasi Na Mwaka Mpya huwaunganisha wanafamilia baada ya mihangaiko ya mwaka mzima. Maisha yamebadilika. Watu wanafanya kazi sehemu mbalimbali Tanzania na hawapati muda wa kukutana.  Hivyo ni ngumu kwa familia kuwa eneo moja kwa mwaka mzima. Ndio sababu, Wachaga wanasifika Tanzania nzima kwa safari zao za kwenda Kilimanjaro kusheherekea Krismasi na Mwaka Mpya na familia na wengine wakiwatania kuwa wanaenda kuhesabiwa. Sio wachaga tu bali watu wa makabila mengi hufanya hivi. Kumbukumbu nyingi huzaliwa msimu huu. Hivyo, kama unajiandaa kukutanisha familia yako msimu huu, fikiria namna ambazo zitawafurahisha na kutengeneza kumbukumbu zisizosahaulika. Hizi ni baadhi ya namna unazoweza kutumia:

1. Panga Sehemu ya Kukutanisha Familia

krismasi na familia

Mara nyingi, muunganiko wa familia msimu wa sikukuu hufanyika nyumbani. Kiutamaduni, huwa hakuna haja ya kutuma kadi ya mwaliko, bali simu hupigwa kuwaalika ndugu na jamaa wa karibu kujumuika pamoja. Anza kwa kufikiria kuhusu idadi ya watu watakaokuja na nani hasa anakuja. Watafikanye? Watalala wapi? Na watarudi vipi makwao  . Na kama ukiamua kuandaa sherehe ndogo njee ya nyumbani, basi chagua mapema mgahawa au ukumbi ambao unadhani kila mmoja ataupenda. Kumbuka tu kwamba, babu, wajomba, shangazi, watoto n.k wakifika kwako watahitaji sehemu nzuri ya kuseherekea mwisho wa mwaka.

2. Fikiria Kuhusu Chakula

Sio kwamba ukiwaaliwa wanafamilia kujumuika nawe msimu huu wa sikukuu basi inatakiwa uandae vyakula vyenye hadhi ya kimataifa ili wafurahi, hapana. Unahitaji kuwa na chakula kizuri ambacho kitawafurahisha. Uliza watu wanapenda nini ili upate maoni yao. Kama kuna wanafamilia wenye magonjwa kama ya kisukari ama ya msukumo wa damu, hakikisha unaanda chakula chao tofauti. Kumbuka watu wengi wanakosa kula vyakula vya kiasili kwa sababu ya kuishi mijini. Je unaweza kuandaa mtori? Je unaweza kupika mlenda? Vyakula hivi vinaweza kuwakumbusha enzi za zamani wakubwa na kuwafundisha tamaduni wadogo.

3. Usisahau Watoto

krismasi na familia usiwasahau watoto

Ni wazi kabisa watoto watahudhuria. Shangazi atakuja na watoto wake na Mama Mdogo atakuja na wa kwake.  Hivyo ni bora ukajiandaa ili na wao waweze kukumbuka msimu huu. Michezo kadhaa na zawadi za watoto zitafanya msimu wa sikukuu kuwa wenye kumbukumbu ya muda mrefu. Fikiria kutenga bajeti ya vitu kama:

  • Midoli na magari ya kuchezea
  • Madaftari na vifaa vidogo vya shule
  • Vyakula vitamu kama keki
  • Katuni na michezo mingine ya watoto

4. Fanya Watu wa Rika Zote Wafurahie

Je unapata changamoto ya kufanya kila mtu afurahie mijumuiko hii? Andaa , baadhi ya shughuli ama michezo itakayowafanya watu wa rika zote kufurahia. Mnaweza  kuimba nyimbo za zamani au za kiutamaduni pamoja wakati wa jioni. Babu na bibi wanaweza kusimulia hadithi mkiwa mnaota moto. Kama inawezekana angalieni filamu kwa pamoja ama ata chezeni michezo ya karata. Watoto wanaweza kupamba mti wa Krismasi. Pigeni picha za pamoja na kuziweka katika fremu ama tengenezeni “family tree” ili kuwasaidia watoto kufahamiana.

5. Ambianeni Mipango Ya Mwaka Mpya

krismasi na familia mipango ya mwaka mpya

Kuwa mbunifu katika hili. Mnaweza mkiwa mmekaa mkizunguka moto, kila mmoja akasema ni kitu gani anataka kufanya mwaka kesho. Ongeleeni mipango ya mwaka unaoishi na changamoto mlizozipata. Tengeneza mazingira salama yatakayoweza kusaidia wanafamilia kunena mamoja na kupanga mipango itakayowainua kwa mwaka ujao.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media