Njia 5 za Kuwa Mwenye Afya na Nguvu Wakati wa Ramadhan

  | 3 min read
0
Comments
1858
ramadan ramadhan

Wakati mwa mwezi wa Ramadhan — Waislam wote ulimwenguni huungana kutimiza ibada ya mwezi wa 9 katika kalenda ya Kiislam, kama mwezi wa kufunga. Ni muhimu kwa watu wote wanaoshiriki kufunga mwezi huu, kuzingatia na kudumisha afya na lishe wakati wa kutekeleza ibada hii. Hizi ni baadhi ya dondoo zitakazokuwezesha kuwa na nguvu na afya bora wakati wa mwezi huu mtukufu

1. Usiruke Daku wakati wa Ramadhan

usiruke mlo wa daku suhur ramadhan ramadan

Kama kifungua kinywa chochote kilivyo na umuhimu katika sehemu ya mlo wa siku, Daku (chakula kinacholiwa kabla ya kupambazuka) ni mlo muhimu sana wakati wa mwezi huu. Husaidia sana mwili wako kubakia kuwa na maji, nguvu na virutubisho muhimu kwa siku nzima mpaka wakati wa futari. Pia chakula hiki kitakuepusha na kula kupita kiasi wakati wa kufungua swaumu yako jioni. Chakula kizuri cha daku kinaweza kujumuisha — Vyakula vyenye wanga, Vyakula vyenye asili ya nyuzi nyuzi mfano viazi, tende, viazi, mboga mboga n.k, na vyakula vyenye protini mfano mayai, jibini, nyama au samaki — vyote hivi ni kwa ajili ya kuupa mwili nguvu na maji wakati wa mchana

2. Punguza Sukari na Vyakula Vya Viwandani

Epuka sana vyakula vya viwandani, vinavyotengenezwa kwa haraka (fast food) ambavyo vinatengenezwa kwa mafuta mengi, sukari na wanga. Vyakula hivi vina virutubisho kidogo sana. Pia epuka vyakula vya kukaanda na vile vinavyoandaliwa kwa mafuta mengi. Ikiwa vyakula hivi haviepukiki, basi unaweza kujaribu kupunguza ujazo wa mafuta unayoyatumia.

3. Jumuisha Matunda na Mboga Kwenye Mlo

matunda na mboga mboga ramadhan ramadan

Matunda na mboga ni muhimu  wakati wa kula, na ni mbadala mzuri  wa vitu vitamu vitamu vinavyoliwa wakati wa mwezi wa Ramadhan. Baadhi ya matunda na mboga yana maji mengi, mfano matango, machungwa namatikiti maji, na. Ukila matunda haya wakati au baada ya kufuturu yanaweza kukufanya uwe na maji ya kutosha mwilini hadi kesho yake wakati wa futari.

4. Kula Futari Polepole na Usizidishe Chakula

Japo inashawishi kula mpaka uchoke wakati wa kufturu kutokana na kushinda njaa siku nzima, kumbuka kuwa unatakiwa uanze pole pole. Unaweza ukaanza na tende au maji kidogo kabla ya kula mlo kamili. Tende zinasifika kwa uwezo wake wa kuleta nguvu mwilini na pia kuandaa mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwa mlo unaofuata. Baada ya hapo, unaweza ukafuata na kitu cha moto — mfano uji, maziwa, chai au supu. Kumbuka unatakiwa ule polepole ili kuupa mwili muda wa kumeng’enya chakula.

5. Zingatia Maji na Epuka Vinywaji Vyenye Kafeni

epuka vinywaji vyenye kafeni ramadan ramadhan

Japo unaweza ukahisi tumbo kujaa sana katika kipindi cha kati ya mlo wa ftari na Daku, usipuuzie kunywa  maji maana yana umuhimu wake. Kunywa angalau glasi 4-8 za maji kwa siku. Tumia vimiminika au vyakula vyenye maji maji kwa kipindi cha kati ya futari na daku. Kuwa makini na epuka vyakula vyenye sukari nyingi na kafeni — vina vichocheo vinavyopelekea uhitaji mwingi wa maji mwilini. Ni vyema kuacha au kutumia kidogo tu vinywaji kama chai, kahawa, soda n.k  

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media