Dondoo 5 za Kuandaa Pendekezo Zuri La Biashara

  | 2 min read
0
Comments
5457
pendekezo la biashara business proposal

Wakati wa kuandika pendekezo (proposal) la biashara, inatakiwa ufahamu kitu kimoja kwamba, muundo wa pendekezo  hilo si muhimu kuliko kilichoandikwa ndani. Hivyo kuwa makini kwa kuandika pendekezo lisiyochanganya, linalomvutia msomaji na lililo rahisi kueleweka.

Japokuwa pendekezo  la biashara lililopangiliwa vizuri ni muhimu ili uweze kuungwa mkono utakapoiwasilisha, kumbuka kutilia maanani vipengele vitatu: Muhtasari, Bajeti na Timu nzima ya biahsra unayoipendekeza. Vipengele hivi ndivyo vitakavyowafanya wasikilizaji watatie umakini kwenye pendekezo  lako.

Hizi ni dondoo muhimu zinazoweza kukusaidia  kuandika pendekezo zuri la biashara.

  1. Elezea Wazo Lako Vizuri

elezea wazo lako vizuri idea of business proposal

Wakati wa kuandaa pendekezo  la biashara unalotaka mtu awekeze, ni lazima ueleze wazo la biashara hiyo kwa uwazi. Ikiwa ni biashara ya kutatua tatizo fulani, basi elezea tatizo hilo na namna ambavyo wazo hilo  litalitatua tatizo hilo. Elezea jinsi wazo hilo lilivyotokea ili kuweza kugusu nyoyo za wasomaji, huku ukizingatia vitu vinavyogusa hisia. Jaribio la kujua kama wazo lako liko wazi ni kuwauliza walio karibu nawe ama marafiki kama wanalielewa.  

2. Elezea Malengo (Vision) ya Pendekezo  Lako

Kila pendekezo lina malengo fulani. . Elezea malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu ya pendekezo hilo.  . Ni muhimu sana kuelezea hili kwa kuwa wawekezaji watataka kujua malengo ya ya biashara yako na wanachoweza kutegemea kutoka katika uwekezaji wao.

3. Onyesha kwa Takwimu

onyesha takwimu use statististics pendekezo la biashara

Pendekezo  lako la biashara pia linatakiwa lielezee faida gani zinazoweza kupimika ambazo mwekezaji atapata. Hii ni sehemu ya kuvutia sana, wawekezaji ndipo hufanya maamuzi muhimu. Hivyo hakikisha takwimu za makadirio ziko sahihi, zenye uhalisia na zinazoeleweka kirahisi.

4. Elezea Kigezo cha Mafanikio

Vigezo utakavyotumia kuonesha   mafanikio ni muhimu, na ni mhimili mkuu wa wazo la biashara yako. Elezea ni vitu gani vikifikiwa mafanikio yatakuwa yamepatikana. Angalia viwango vya faida, ukuwaji wa timu ya wafanyakazi, ukubwa wa soko, nakadhalika. Vigezo vizuri humvutia mwekezaji kuangalia pendekezo la biashara yake.  

5.  Bajeti

bajeti muda wa mwisho pendekezo la biashara

Mwisho, ongelea bajeti yako. Unahitaji kiasi gani ili uweze kufanya biashara yako ifanikiwe kwa kipindi maalum kilichoelezewa? Kumbuka kulinganisha thamani ya mtaji  dhidi ya ukubwa wa matarajio ya mradi au biashara unayoipendekeza. Matokeo ya mradi au biashara unayoipendekeza hutokana na uwekezaji.

Kwa dondoo hizo apo juu, sasa unaweza kuunda pendekezo  lako la biashara na kulifanya livutie kusoma, na kuongeza nafasi ya kukubaliwa na wawekezaji . Ikiwa unaona unatoa maelezo mengi sana yanayoweza kuwa na kurasa nyingi sana, jaribu kuweka pointi muhimu katika muhtasari mkuu kwa ufupi, na kwa namna hiyo itaeleweka kirahisi zaidi.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media