Jinsi Ya Kufanya Manunuzi Kupitia Mtandao wa ZoomTanzania

  | 3 min read
0
Comments
2153
nunua zoomtanzania

Teknolojia imerahisisha mambo mengi. Kwa mfano, biashara zimerahisishwa kiasi kwamba mtu unaweza kuuza na kununua bidhaa  na huduma tofauti bila kunyanyua mguu. Mtandao wa Zoom Tanzania unaunganisha vyema dhima hii. Unafanya mchakato wa kutangaza biashara ya muuzaji na upatikanaji wa bidhaa kwa wanunuzi uwe wa  rahisi sana. Mtandao wa Zoom Tanzania umekuwa ukiwaunganisha wanunuzi na wauzaji toka mwaka 2009.

Nunua Kwa usalama na ZoomTanzania

Zoom Tanzania ina waunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa na huduma kupitia mtando huu kwa kuzingatia usalama wa pande zote mbili. Bidhaa zote zinakaguliwakwa umakini mkubwa na wataalam wa bidhaa waliopo ZoomTanzania ili kuhakikisha wanunuzi wanapata bidhaa na huduma zenye salama.

Jinsi ya kununua na ZoomTanzania

1. Tembelea Tovuti ya ZoomTanzania.Com

nunua zoomtanzania

Hatua ya kwanza kabisa ya kufanya manunuzi katika mtandao huu ni kutembelea www.zoomtanzania.com. Unaweza ukatumia kompyuta ya mezani, kompyuta mpakato ama hata unaweza kuingia kwa kutumia simu yako.  Zoom Tanzania pia ina App ambayo itaendelea kufanyiwa maboresho. Ukifika kwenye page ya kwanza, utaona vipengele tofauti vyenye makundi ya bidhaa tofauti.. Ukifika, unaweza kuachagua kipengele  cha bidaa unachotaka au kutafuta jina halisi la kile unachotaka, mfano IST, Nyumba Magomeni, Kiatu, na kadhalika. Unashauriwa uchukue muda kwenye tovuti ili uweze kulinganisha bidhaa tofauti ukiangalia be, ubora, modeli, rangu, na kadhalika.

2. Chagua Bidhaa/Huduma 

Mtandao wa Zoom Tanzania umefanywa kuwa rafiki kwa watumiaji wote. Kuna watu ambao wanajua kabisa wanachotaka, hivyo akiingia anatafuta na kuchagua bidhaa anayotaka. Lakini kuna  wengine huamua kuangalia kwa muda kwanza ili kulinganisha bei, aina, uwezo wa bidhaa n.k. Vyote hivi vimewezeshwa kirahisi kwani ukiingia ZoomTanzania, unaweza ukachagua bidhaa moja moja au kuingia katika bidhaa zilizowekwa katika vipengele (categories). Utakachokipenda, bofya picha yake ili kukifungua.

3. Soma maelekezo ya bidhaa/ Huduma

zoomtanzania

Baada ya kufunga bidhaa unayotaka, utapelekwa katika kurasa yenye maelezo zaidi kuhusu bidhaa hiyo. Mfano, kama ni simu uliipenda, basi ukiifungua utapelekwa kwenye ukurasa unaoonyesha ukubwa, uwezo, picha zaidi, bei na namba za simu za muuzaji. Pia kuna maelezo mengine mengi mfano hali ya simu (ni mpya au iliyotumika?) sehemu inapouzwa, kama muuzaji anasafirisha ama la  na kadhalika. Ukiridhika na maelezo hayo , unaweza kuamua kununua au kuendelea kutafuta

4. Wasiliana na Wauzaji

Baada ya uchaguzi wa bidhaa na kusoma taarifaza bidhaa/ huduma, unaweza kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja. Kwa kawaida, mtandao wa Zoom Tanzania unaweka namba ya simu upande wa kulia wa tangazo,   ikiwa kwenye batoni ya blue. Unaweza kumtumia ujumbe wa WhatsApp, kumtumia meseji ya kawaida, na hata kumpigia simu . Pia unaweza kumtumia barua pepe kumuuliza maswali kuhusu bidhaa yake. Kumbuka, hauhitaji kupiga simu kwenye ofisi za Zoom Tanzania kwa maana sio wauzaji bali ni wamiliki wa platform inayotumiwa na wauzaji kutangaza bidhaa yako. Unachotakiwa kufanya ni kuongea na muuzaji moja kwa moja.

5. Kuwa Makini

zoomtanzania

Lengo kuu la mtandao wa Zoom Tanzania ni kukutanisha Wauzaji na Wanunuzi. Lakini, kama ilivyo katika masoko mengine, kuna wauzaji wema na wauzaji waovu. Na kuna wanunuzu wema na matapeli. Kuwa makini wakati wa kuwasiliana na wauzaji na kufanya malipo. Zoom Tanzania inafanya kazi vizuri sana kuhakikisha inadhibiti matapeli na wezi wa mitandao kwa kukagua bidhaa na wauzaji kabla ya kuhakiki matangazo yao katika mtandao. Lakini ikiwa unapata mashaka, mfano muuzaji anakulazimisha kulipia bidhaa kabla ya kuiona, kuwa makini. Hakikisha unamuona muuzaji, unakagua bidhaa unayoitaka na unafanya malipo ukiwa sehemu salama ukiwa umeshapata bidhaa. Kama unanua bidhaa ukiwa mkoani, hakikisha unatafuta ndugu, rafiki ama mtu unayemuamini ili aweze kuikagua bidhaa hiyo.  Ukiona unapata tabu, wasiliana na watoa huduma wetu moja kwa moja na watakushauri nini cha kufanya.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media