Njia 6 Rahisi za Kupunguza Matumizi Makubwa Ya Umeme

  | 4 min read
0
Comments
7602
punguza gharama za umeme

Siku hizi matumizi mengi ya nyumbani yanahusika sana na umeme. Taa, feni, mashine za kufulia, viyoyozi, friji, majiko ya umeme vyote vinafanya maisha kuwa rahisi zaidi. Lakini matumizi makubwa ya vifaa hivyo vinavyotumia nishati ya umeme vinakuja na gharama kubwa. Kila mtumiaji wa umeme angependa kujua ni kifaa gani kinatumia umeme sana nyumbani, ili aweze kujua ni njia gani mbadala anaweza kutumia ili  kupunguza gharama.

Kila unapopunguza matumizi ya nishati ya umeme nyumbani, unapunguza gharama na unaweza kutunza fedha kwa matumizi mengine. Matumizi madogo ya umeme pia ni njia ya kutunza mazingira. Kuna njia nyingi za kupunguza matumizi ya umeme nyumbani na kufurahia zaidi maisha na kupunguza gharama.

1. Tumia Vifaa Vinavyotumia Umeme Mdogo

punguza gharama za umeme

Kuna vifaa vingi vya umeme vilivyo katika kiwango na ubora mzuri vinavyotumia umeme mdogo. Punguza gharama za matumizi ya umeme kwa kuchagua vifaa vinavyotumia umeme mdogo. Kwa teknolojia inapoelekea, vifaa vingi kama taa, feni, friji n.k. vinatengenezwa kwa mfumo unaowezesha kutumia umeme mdogo hivyo kuokoa gharama kubwa. Ikiwa unapendelea kutumia majiko na oven ya umeme, unaweza kuchagua kama Toster zenye Oven ambazo zinasifika kwa uwezo mzuri wa kupikia lakini kwa matumizi madogo ya umeme.Ingia Zoom Tanzania ujionee zaidi bidhaa za umeme zenye matumizi madogo ya umeme.

2. Usiache Plagi Ikiwa Imechomekwa kwenye Umeme.

Umeme hutumika wakati vyombo vya umeme vimeunganishwa na kuwashwa kutoka kwenye soketi. Baadhi ya vifaa mfano pasi, huhitaji kuwa vimechomekwa kwenye umeme wakati wa matumizi yake. Wakati mwingi, vifaa kama hivi vikiachwa katika umeme, huweza kusababia mtitririko wa umeme kuendelea kuwepo hata kama vifaa hivi vimezimwa. Hakikisha unachomoa kabisa plagi kutoka kwenye soketia. Hakikisha pia unazima umeme kwenye kila chumba ambacho hakitumiki kwa wakati huo. Watu wengi husahau kuzima feni majumbani au kuacha vifaa kama hita, taa, n.k vikiwa katika soketi za umeme.  Ni muhimu kuwa mwangalifu na kufuatilia vitu hivi.

3. Tumia Feni Zaidi Kuliko Viyoyozi Kupunguza Joto

punguza gharama za umeme

Ingawa viyoyozi vinapendelewa na wengi, ikiwa una mpango wa kupunguza matumizi ya umeme, basi ni muhimu kuchangua matumizi ya feni kuliko ya viyoyozi. Viyoyozi vinasifika kwa kutumia umeme mwingi, hasa kwa kuzingatia vinafanya kazi kubwa ya kupooza joto . Ili kuokoa gharama kubwa, unaweza kuwasha kiyoyozi kwa muda mchache mpaka hali ya joto itakapopoa, kisha kuendelea na matumizi ya feni ya kawaida. Hii itasaidia kupunguza muda mrefu wa kiyoyozi kutumika hivyo kuokoa gharama za umeme.. Baadhi ya viyoyozi vya kisasa vinakuja na mfumo unaokiwezesha kiyoyozi chenyewe kujizima baada ya muda fulani utakaoupendelea, na kujiwasha pale joto linapoongezeka.

4. Pendelea Madirisha Makubwa Nyumbani.

Madirisha ni moja ya sehemu muhimu ya  nyumba. Mpangilio na ukubwa wa madirisha unaweza kuruhusu upitishaji mzuri wa hewa ndani ya nyumba. Ikiwa uko kwenye hatua za ujenzi au umefikiria kufanya maboresho ya nyumba yako, fikiria kuongeza ukubwa wa madirisha ili kupata  hewa ya asili na kuachana na feni au viyoyozi. Kama madirisha yanapitisha hewa vizuri, matumizi ya umeme yatapungua kwa kiasi kikubwa.

5. Tumia Nishati za Umeme Mbadala

punguza gharama za umeme

Vifaa vya umeme wa sola vinaweza pia kuwa jibu la tatizo la matumizi makubwa ya umeme nyumbani. Maendeleo ya teknolojia yanaongeza uwepo wa vifaa vingi vinavyotumia mfumo wa jua kama vile Balbu za nyumbani, feni za sola n.k vinaweze  kupunguza sana gharama za umeme. Japokuwa matumizi yake yanaweza kuwa na mipaka kwa kiasi fulani, lakini gharama zake ni bora sana kuliko gharama za malipo ya umeme wa kawaida. Pia, ni rahisi kutumia katika baadhi ya maeneo, mfano vijijini ambapo gharama za kujiunganishia umeme wa Tanesco ni kubwa sana.

6. Panda Miti

Kupanda miti si tu njia nzuri ya kutunza mazingira, bali pia ni sehemu muhimu ya kuokoa gharama kubwa za umeme. Miti inasaidia upatikanaji wa hewa nzuri na mzunguko mzuri wa hewa na vivuli. Wakati ukiwa nyumbani, badala ya kufikiria kuwasha kiyoyozi au feni, badala yake vivuli vya miti na hewa yake vinaweza kuwa mbadala tosha. Jijengee utaratibu wa kupanda miti mapema nyumbani na kumbuka ni tegemeo la muda mrefu sana la kupunguza gharama za umeme kwa miaka mingi mbele.

Zipo njia nyingine nyingi za kupunguza matumizi makubwa ya umeme nyumbani, la kuzingatia ni kutumi njia salama na rahisi za kufanikisha hilo. Njia mbadala za nishati ya umeme, mazingira safi na vifaa vyenye ubora ni suluhisho lako katika kupunguza matumizi makubwa ya umeme

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media