Sifa 7 za Mwanamke Mpambanaji

  | 3 min read
0
Comments
9202
mwanamke mpambanaji

Dunia ingekuwa wapi leo bila mwanamke? Wanawake wana  nafasi kubwa katika jamii yetu ya Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla. Mwanamuziki Beyoncé wa marekani aliwahi kuimba akisema wanawake wanakimbiza/wanaongoza dunia (Runs the World (Girls)

Ingawa baadhi ya wanawake wengi hawajapata ujasiri wa kuishi kufuatana na  matakwa yao, wapo wengine wanaoishi na kutimiza ndoto zao katika maisha yao kila siku.

Katika kuisheherekea  siku ya wawanawake duniani tarehe 8 Machi 2019, Zoom Tanzania ikiamini nguvu ya mwanamke katika jamii ingependa kuchukua nafasi hii kutambua ujasiri na upambanaji wao katika jamii. Katika karne hii, mwanamke amepewa kipaumbele  na kuwezeshwa katika jamii, jambo lililosababisha wanawake wengi kujitambua na kufanya mambo makubwa zaidi kuliko hapo awali.

Mwanamke mpambanaji ni mwanamke imara na anayeijua nguvu iliyo ndani yake ya kupambana na kukabiliana na changamoto katika nyanja mbalimbali za  maisha ili kutimiza malengo yake. Hizi ni sifa za mwanamke mpambanaji:

  1. Jasiri

jasiri mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ni jasiri anaona nafasi za kujiendeleza na kuzinyakua haraka. Mwanamke jasiri haogopi kushindwa na  changamoto zilizo mbele yake, siku zote huchagua kuzikabili. Wanawake wengi majasiri wamefanikiwa kuinua uchumi wao na kuzisimamia familia zao, wakati mwingine bila hata ya msaada wa mwanaume. Ni wajasiriamali. Ni wanawake wenye nyadhifa za uongozi wakifanya kazi na kuleta  maendeleo kwa bidii.

  1. Hufanya Maamuzi Sahihi

Mwanamke mpambanaji haogopi kufanya maamuzi sahihi juu ya maisha yake na kufuatilia mipango yake. Hupokea maoni chanya  na kuamua pia kupuuzia maoni ya watu wengine yasiyo na tija ama ambayo hayamsaidii kwenda mbele na kutimiza ndoto zake. Kutokana ma mapito yake, mwanamke mpambanaji hufanya mamuzi sahihi juu ya jinsi gani ya kubadili mwenendo wa maisha yake ili  kujiboresha siku zote.

  1. Ana Ndoto

ana ndoto mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji ana ndoto za kuwa mtu fulani ama kufikia malengo fulani. Haogopi kuwa tofauti na mategemeo ya wengine. Pia anajua ni njia gani za kufuata ili  kutimiza ndoto zake. Anajua umuhimu wa kuwa makini na kila nafasi inayopita mbele yake inayoahidi mafanikio. Ndoto zake ni muhimu kwake na huzipa kipaumbele.

  1. Mbunifu

Mwanamke mpambanaji ni mbunifu kila wakati. Wanawake wamebarikiwa uwezo wa kufanya mambo mengi katika  muda mchache. Hivyo basi, mwanamke mpambanaji anajua jinsi ya kujigawa katika kazi, kuongeza ujuzi na kujaribu mambo mbalimabli ili apate matokeo sahihi katka mambo anayoyafanya.

  1. Anajitegemea

Mwanamke mpambanaji anajua kujisimamia katika mambo mbalimbali maishani. Hii haimaanishi mpambanaji  hahitaji msaada kwa wengine bali anajua msaada peke yake hautoshi. Anafahamu kuwa lazima ajiongeze maana kuna mambo mengi anayohitaji kutimiza. Hivyo basi, anaelewa nafasi yake katika maendeleo yake na hata ya familia yake.

  1. Hujitoa

hujitoa mwanamke mpambanaji

Mwanamke mpambanaji anatambua mchango wake katika jamii inayomzunguka. ujitoa kwasababu ni jambo sahihi na si kwa ajili  ya kupata umaarufu ama cheo. Mwanamke mpambanaji pia anajua thamani ya kuwainua wengine na kuwatia moyo wale wanaomwangalia. Siku zote, anajitambua na kutambua mchango wake katika jamii yake.

  1. Anatia Hamasa

Mwanamke mpambanaji huhamasisha jamii yake kuwa bora zaidi  kupitia juhudi zake na mafinikio yake huhamasisha watu wengine kuongeza jitihada katika shughuli na mambo  mbalimbali. Mpambanaji sio mchoyo wa maarifa, na hupenda kuona wengine wakifanikiwa kupitia yeye.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media