Vitu 5 vya Kukarabati Gari Kabla Ya Msimu wa Mvua Kuanza

  | 3 min read
0
Comments
5548
Msimu wa Mvua rekebisha gari

Hakuna haja sana ya kuelezea namna ambavyo mvua inaweza kuwa hatari kwa gari lako, na maisha yako pia. Msimu wa mvua umekaribia sana.. Hivyo ni bora ukajiandaa kwa lolote linaloweza kutokea. Kwa msaada wa wataalam, hizi ni baadhi ya sehemu muhimu za gari lako unazotakiwa kuzifanyia marekebisho mapema kabla msimu wa mvua haujaanza.

  1. Breki

msimu wa mvua breki za gari

Breki ni sehemu muhimu sana  linapokuja suala la uendeshaji gari msimu wa mvua. Lakini cha ajabu, watu wengi wanapuuzia kuzikagua na kuzibadilisha . Sababu? Wanatumia kila siku., inatakiwa uwe makini zaidi wa  breki zako wakati huu wa kuelekea msimu wa mvua kwa maana Wakati wa mvua brake zinaweza kusumbua kutokana na uwepo wa msuguano hafifu kwenye raba, ngoma na diski za breki. Hivyo ni vyema kuzikagua  mapema na kuzibadilisha kama kuna uhitaji kabla hali haijawa mbaya zaidi msimu wa mvua ukianza.

  1. Ball Jointi na Tire Rod Ends

Hivi ni viungo muhimu sana na vinapatikana katika magari mengi. Ni beringi za uviringo, na zinafanya kazi kama ilivyo katika muunganiko wa mwisho wa goti la  binadamu. Zinafanya kazi muhimu sana ya kuunganisha ustelingi wa gari na mikono ya matairi ya gari. Zote kwa pamoja zinaathiri uwezo wako wa kuamua gari liende uelekeo gani. Kwa ufupi, hizi zikivunjika, basi unakuwa huwezi kuliongoza gari na linaweza kwenda uelekeo wowote. Hivyo ni muhimu sana kuzibadilisha mapema, hasa kabla msimu wa mvua haujaanza. Wataalam wanashauri kuwa, kusikiliza dalili za mapema za kuchoka kwa Ball Jointi na ‘Tire rod ends’ kama vile:

  • Sauti za Kugonga gonga kutoka kwenye tairi za mbele
  • Mtetemo (vibration) iliyopitiliza kutoka kwenye suspension ya mbele
  • Ustelingi wa gari kuvutia upande mmoja (Kulia au kushoto)

Ukiona dalili kama hizi, na hata kama si zote zimejitokeza, basi ni bora kujiandaa mapema kabla majanga hayajakufika.

  1. Kagua Matairi Mapema

msimu wa mvua kagua matairi ya gari

Hili sio la kufikiria mara mbili. Tredi zinazowekwa kwenye matairi ya gari si kwa ajili ya mapambo. Zimetegenezwa maalum kabisa kwa ajili ya kuondoa maji na unyevu unaoweza kukaa baina ya mpira wa tairi lako na barabara hivyo kusababisha gari kuteleza. Tairi zikichakaa sana, hubaki vipara. Ukiwa katika barabara yenye maji, husababisha mwelekeo wa gari kuwa rahisi kuathiriwa kutokana na kutokua na mshikamano thabiti baina ya tairi na barabara. Inaweza kupeleka ajali na hata madhara makubwa kama kifo. Hivyo kabla hatujafika msimu wa mvua na tairi za gari lako zina kipara, huu ni muda sahihi wa kuwaza kuhusu tairi mpya.

  1. Angalia Betri na Mfumo wa Umeme Mapema

Kwa kawaida, betri za gari zimetengenezwa kudumu kati ya miaka minne mpaka sita . mvua inaweza  kuathiri ubora wa betru yako. Maji maji na unyevu vinaweza kusababisha kutu na shoti katika sehemu tofauti za gari lako (mfano kama kuna nyaya zilizochubuka) na hivyo kuua betri ndani ya muda mchache. Katika kuelekea msimu wa mvua, ni bora kulifanyika kazi hili mapema. Kama gari linaonyehsa dalili yeyote ya kusumbua katika mfumo wa umeme au betri kusumbua wakati wa uwashaji  gari ni bora kuingia gharama mapema. Ni afadhali kutumia pesa sasa hivi kuliko kulala barabarani ndani ya gari lililozimika usiku wakati wa mvua.

  1. Kagua Mfumo wa ‘Suspension’

nsimu wa mvua kagua suspensheni

Huwezi kusahau kabisa mfumo wa ‘Suspension’ wakati wa msimu wa mvua. Maji husifika kwa uharibifu wake hasa katika sehemu za vyuma. Katika mfumo wa uendeshaji, sehemu kubwa ya ‘Suspension’ imefunikwa kwa mipira na plastiki ili kuzuia maji yasiingie. Lakini wakati mwingi, mipira hii huzidiwa na joto na hivyo kupasuka. Hivyo, hakikisha mapema sana, kabla msimu wa mvua haujafika unapeleka  gari lako kukaguliwa hasa sehemu hizi zinazohitaji kufunikwa na mipira bado ziko imara. Vinginevyo, gharama za kurekebisha zinakuwa kubwa zaidi wakati wa kubadilisha vifaa vya chuma badala ya mipira midogo midogo.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media