Majibu ya Maswali 10 Muhimu Zaidi Kuhusu ZoomTanzania

  | 5 min read
0
Comments
2068
maswali majibu zoomtanzania

ZoomTanzania ni mtandao mkubwa na wa kuaminika unaowakutanisha wauzaji na wanunuzi kutoka sehemu tofauti Tanzania. Haya ni baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakiulizwa zaidi na watumiaji wa mtandao huu. Tumeweka majibu yake ili kuwasaidia wateja wetu kufahamu ZoomTanzania. 

1. Ninauzaje Bidhaa ZoomTanzania?

uza zoomtanzaniaIli kuweza kuuza bidhaa ZoomTanzania, inahitaji ufungue akaunti ya bure kabisa katika mtandao huu. Baada ya hapo, bofya kitufe kilichoandikwa  Weka tangazo/Post Ad. Baada ya hapo, ingiza taarifa za tangazo lako.

Ili tangazo lako liwe zuri na bora, hakikisha lina kichwa chenye jina la bidhaa, maelezo rahisi na yanayoeleweka, bei na picha nzuri za bidhaa. Tangazo lako litaonekana mtandaoni baada tu ya timu ya ZoomTanzania kulihakiki.

2. Mchakato wa Kuhakiki Tangazo langu Unakuwaje?

Kama ukiweka tangazo lenye ubora unaotakiwa, basi tangazo lako litaonekana kwa haraka baada ya muhakiki kulipitia. . Ili hili litokee inabidia  jina la tangazo lionekane vizuri, maelezo ya tangazo lako yanajitosheleza, na bei na picha ziwe sawia. Lakini kama tangazo lako litakuwa lina shida, , basi timu yetu ya wahakiki watakushauri nini cha kufanya ili kuliboresha na baada ya marekebisho tangazo lako litaonekana kwa wanunuzi.  Tangazo lako litahakikiwa ndani ya masaa 2 kama utaliweka ndani ya masaa ya kawaida ya kazi. Kama ukiliweka ndani ya muda wa ziada wa kazi na siku za wikiendi, basi itachukua hadi masaa 8 kuhakikiwa. 

Baada ya tangazo kuruhusiwa, utapokea ujumbe kutoka ZoomTanzania kukutaarifu hili. Kama lilikataliwa, utapokea ujumbe wa barua pepe au kupigiwa simu kujulishwa nini tatizo. Hapo utaweza kulirekebisha na kuposti upya tangazo lako. Matangazo yako yote yatakuwa kwenye ubao wako wa matangazo. 

3. Nawasiliana vipi na Muuzaji?

nunua zoomtanzania

ZoomTanzania ni mtandao unaowakutanisha wauzaji na wanunuaji wa bidhaa. Lakini ZoomTanzania sio wauzaji wa bidhaa zinazoonekana kwenye tovuti. . Ili kununua kitu unachokipenda, unaweza kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja kwa namna tofauti. Kama unatumia WhatsApp, bonyeza kwenye kitufe chenye nembo ya Whatsap kwenye upande wa kulia wa tangazo la bidhaa unayotaka. Itafungua WhatsApp  moja kwa moja ikiwa na namba ya muuzaji. Kama utataka kumpigia moja kwa moja, basi tumia kitufe kilichoandikwa Onesha Namba (Show Number). Na pia unaweza kuwasiliana na muuzaji kupitia barua pepe. Tumia sehemu ya barua pepe kama uko tayari kufanya hivyo. 

4. Ninaripoti vipi Udanganyifu wa Wauzaji?

Kila tangazo lina sehemu ya Ripoti Tangazo Hili. Kama una mashaka ya aina yeyote na tangazo unaloliona, bonyeza sehemu hii mara moja na eleza sababu za kwa nini hasa unaliripoti tangazo hilo. Tutapokea ripoti yako na kuchukua hatua mara moja

Pia, unaweza kututumia ID ya tangazo kwenye page zetu za mitandao ya kijamii au kututumia email moja kwa moja kwenda info@zoomtanzania.com au kutumpigia kupitia namba 0655 140 602 iliyopo  chini kabisa ya tovuti yetu Tunawaomba wateja wetu wawiliane nasi kama wataona tatizo lolote. 

5. Kuna tofauti gani kati ya Wauzaji Binafsi na Wafanyabiashara?

tofauti kati ya wafanyabiashara na wauzaji binafsi zoomtanzania

Akaunti za Wauzaji Binafsi ni kwa ajili ya mauzo ya kawaida. Kama una kitu chochote nyumbani kwako unataka kukiuza na kupata fedha ya ziada ama kupata nafasi zaidi kwenye stoo yako, basi unaweza ukafungua akaunti ya binafsi na kuuza kirahisi. 

Wafanyabiashara kwa upande mwingine ni wale wanaonunua bidhaa kwa ajili za kuziuza tena. Mara nyingi wanauza bidhaa nyingi. Baada ya kufungua akaunti yako unaweza kujitambulisha kama muuzaji binafsi ama mfanyabiashara kwa kwenda kwenye profaili yako. Ama kama haujatambulisha akaunti yako, basi wakati wa kuweka tangazo lako, utaulizwa kama unauza kama muuzaji binafsi ama mfanyabiashara. 

6. Ninafanya Vipi Tangazo langu liwe kwenye Ukurasa wa Punguzo (Deals)?

Kila muuzaji anaweza akafanya bidhaa yake ionekane kwenye ukurasa wa Deals. Ili bidhaa yako iweze kuonekana kwenye ukurasa huo, bonyeza kitufe kimeandikwa Actions kwenye tangazo husika, kisha bofya sehemu imeandikwa Submit a Deal. Baada ya hapo weka bei ya punguzo unayotoa na hakikisha itakuwa ndogo kuliko bei ya kwanzoni. Kisha onyesha  ikiwa unataka punguzo lako likae kwa muda gani. 

Baada ya hapo, timu yetu ya wahakiki watalipitia na kuliruhusu. Page ya deals inapatikana hapa

7. ZoomTanzania Inasaidiaje Wauzaji na Wanunuzi?

ZoomTanzania inatoa hela muhimu juu ya biashara za kimitandao ili kuwasadia wauzaji wapate wateja wengi zaidi na wanunuzi kupata bidhaa bora. Pia, ZoomTanzania inatoa elimu juu ya ulinzi wakati wa kufanya mauzo na manunuzi mitandaoni ili kuwalinda wateja wake. Haya yote yanatolewa kupitia blogu yake inayopatikana kupitia www.zoomtanzania.com/blog

  1. Ninawasiliana Vipi na ZoomTanzania? 

Kama ungependa kuwasiliana na ZoomTanzania kuna namna tofuati unazoweza kuzitumia kulingana na mahitaji yako. Unaweza kutupigia simu kupitia namba hii 0655 140 602. Pia unaweza kutuandikia barua pepe kupitia info@zoomtanzania.com. Tuko kwenye mitandao ya kijamii ili kuwa karibu kabisa na wateja wetu. Huko unaweza kutu-follow kwa kutafuta ZoomTanzania kwenye mitandao ya kijamii na kutuuliza swali lolote. Na kama ukihitaji, unaweza kututembelea ofisini kwenye Masaki kwenye jengo la Renaissance Plaza. Tuko ghorofa ya kwanza. 

  1. Nani Anaweza Kuuza ZoomTanzania?

uza bidhaa mtandaoni hakikisha bidhaa zinamfikia mnunuzi

Kila mtu anaweza kuuza ZoomTanzania kama yuko nchini Tanzania. Unaweza kuwa mfanyabiashara mwenye duka ama unaweza kuwa muuzaji binafsi ambaye unataka kuuza vitu usivyovihitaji. ZoomTanzania haitozi gharama yoyote kuweka tangazo lako. Haijalishi uko wapi nchini Tanzania. Ingia kwenye website ya ZoomTanzania na anza kuuza leo. 

  1. Kuna Gharama Zozote za Kuweka Tangazo ZoomTanzania?

Hakuna gharama zozote za kuweka tangazo lako kwenye ZoomTanzania. Lakini, kama utapendelea kufanya tangazo lako lionekane mwanzoni kabisa wa kurasa, utahitaji kulipia ili kupata huduma hiyo. Lakini kuweka tangazo la kawaida hakuna gharama zozote zinazotozwa.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media