Hatua 5 Muhimu za Kufanya Masoko Kipindi Cha COVID19

  | 4 min read
0
Comments
2305
biashara kipindi covid19

Kila biashara imeathirika na inaendelea kuathirika na janga la COVID-19. Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Afrika na dunia kwa ujumla zimeweka vikwazo kwa raia wake kukaa ndani ili kuzuia uwezekano wa maambukizi kusambaa. Kwa biashara kubwa, athari za janga hili zinaweza kuchukua muda kuonekana, lakini kwa biashara ndogo, hali ni tete mwanzoni kabisa. 

Watu wengi sasa wanajifungia majumbani kwa hofu ya maambukizi, hivyo kupungua au kupotea kabisa kwa wateja si jambo la kushangaa

Kama wewe ni mfanyabiashara mdogo na biashara yako imeshapata athari za mwanzo za janga hili, hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kuzifata kipindi hiki cha janga la Covid-10.

1. Usipotee Kabisa

biashara kipindi covid19

Ikiwa umefikia hatua kufunga kabisa biashara yako kutokana na kutokuwa kwa wateja au kuhofia maambukizi, huu sio mwisho. Jaribu kutenga muda kujadiliana na wafabiashara wenzako pamoja na wateja wako ili kujua nini kinafanya kazi na nini hakifanyi kazi wakati huu. 

Ni muhimu sana kuwasiliana na wafanyabishara wenzako na wateja wako. Unaweza kuamua: 

  • Wape taarifa. Haijalishi una biashara ya aina gani — labda ni saluni ya nywele, duka la nguo, au duka la vifaa vya elektroniki, ni lazima wateja wako na watu wako wa karibu wasikie kutoka kwako. Unaweza kutumia njia ya message, barua pepe au mitandao ya kijamii kuhakikisha kuwa wanajua bado uko. Sio kwamba tu njia hii itasaidia wao kujua kama una bidhaa au unafanya vipi kazi, bali pia ni njia nzuri ya kuwaelezea namna wanaweza kusaidia biashara yako katika kipindi hiki. 

2. Badilika Kutokana na Jamii Yako. 

Kuwa mbunifu. Kwa sasa, watu wengi wanaanza kutengeneza utaratibu mpya wa kila siku. Kuna ambao wanaanza kujitengenezea mazoa ya kufanya kazi kutokea nyumbani, kufanyia mazoezi nyumbani na wengine kulea watoto kutokea nyumbani. Wote hawa wanahitajiwatoa huduma wao kama wewe wabadilike kutokana na mazingira na hali ilivyo. Hivyo, unaweza kutafuta namna ambavyo unaweza kuwa msaada wao muhimu kipindi hiki. 

3. Rekebisha Namna Unavyouza Mtandaoni na Huduma Kwa Wateja

biashara kipindi covid19

Kama una duka la mtandaoni na unauza bidhaa za kawaida kama nguo, vifaa vya nyumbani n.k,jiandae kuzidiwa na oda, hasa wa watu wanaouza bidhaa za vyakula na majumbani. Maduka mengi makubwa ambayo yana huduma za mtandaoni yenye bidhaa hizi  yanaweza kuzidiwa na idadi ya wanunuzi hivyo watu wengi wanaanza kutafuta bidhaa kwa maduka mengine ya kawaida. Kama ukiwa na kitengo kizuri cha huduma kwa wateja, huu ndio wkati mzuri wa kuhakikisha kila bidhaa uliyo nayo inapata mnunuaji. 

4. Sikiliza Wateja Wanataka Nini

biashara kipindi covid19

Ni ukweli wa kawaida na muhimu kuwa kwa kipindi kama hiki kuwasikiliza wateja katika kipindi kama hiki kutakusaidia wewe kupata picha ya wateja wanataka bidhaa na huduma gani kutoka katika biashara yako. 

Kama janga hili litandelea kukua, maduka mengi yatafungwa. Lakini, yale yenye biashara za mtandaoni (Mfano yenye tovuti zao, Kurasa za mitandao ya kijamii n.k)  yataendelea kung’ara. Na inatazamiwa biashara nyingi sana zitaamia mtandaoni katika kipindi cha miaka 10 inayokuja. Hivyo, ili kuwa miongoni mwa kimbilio a wateja, ni muhimu kujua wanataka nini. Unaweza kufanya tafiti ndogo kwa kuuliza maswali rahisi kwa wateja sahihi. Mfano unawezakutumia

  • Tafiti Fupi za Mtandaoni (Online Surveys)
  • Tafiti Fupi katika Mitandao ya Kijamii
  • Maoni ya wateja Baada ya kununua Bidhaa yako au Huduma

5. Jiandae Kufanyia Kazi Nyumbani

COVID-19 ni janga lililobadilisha mengi sana katika soko. Watu wemgi wamelazimika kubadili utaratibu wao wa kawaida wa maisha. Kufanyia kazi nyumbani ndio trendi kubwa zaidi kwa sasa. Hivyo kama bado hujaanza, basi andaa mazingira mapema ya biashara yako kuhamia nyumbani kwako. Hii itakusaidia kama ikitokea amri ya watu kukaa nyumbani imewekwa, basi hautatetereka sana. Hivi ni vitu unaweza kufanya kujiandaa:

  • Andaa ofisi yako ndogo nyumbani
  • Usiwe na Muda maalum wa kUfanya kazi kama kawaida
  • Hakikisha una usalama wa Data 

 

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media