Makosa 5 Ya Kuepuka Wakati wa Kuuza Bidhaa Mtandaoni

  | 4 min read
0
Comments
2735
makosa ya biashara mtandaoni

Kufanya mauzo mtandaoni kunajumuisha mafunzo mengi ambayo unaweza kujifunza endapo tu utafanya biashara. Idadi ya wafanyabiashara mtandaoni inaongezeka kila siku. Baadhi wanafanikiwa sana na wengi wanaishia njiani. Miongoni mwa sababu ni kushindwa kujifunza kwa wafanyabiashara juu ya nini kinafanya kazi, na nini hakifanyi. Kama ukiepuka makosa haya, unaweza kuingia katika kundi la wafanyabiashara wa mtandaoni waliofanikiwa zaidi

Haya ni makosa 5 ambayo wengi wanayafanya wakati wakijaribu kuuza vitu mtandaoni

1. Kutegemea Kupata Wateja Kwa Haraka

makosa ya biashara ya mtandaoni

Kufanya mauzo mtandaoni ni  zaidi ya kupiga picha na kuziweka mtandaoni tu. Watu wengi wanaamini kwamba, ukiwa na bidhaa ukaiweka mtandaoni basi wateja watamiminika. Inaweza kuonekanai ni kazi rahisi sana. Lakini kwa uhalisia inahitaji “sadaka” kubwa zaidi.

Badala yake, unatakiwa kuzingatia kutengeneza na kukuza jamii ya wanunuzi wako kwanza. Waoneshe  thamani ya kuwa katika kurasa za mitandao yako ya kijamii. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaonesha a video au kuwaandikia makala zinazowaelimisha na zenye thamani kwao. Mfano, kama unafanya biashara ya nguo, unaweza kuandaa video au kuandika makala kuhusiana na mitindo iliyoko kwenye chati, njia mbalimbali za kuwaa  mrembo n.k. Kwa kufanya hivi, unatengeneza jamii inayokuamini na itakuwa rahisi kwao kununua bidhaa kutoka kwako. 

2. Kuwauzia Watu Ambao Hawapo

Kama hujui watu unaowauzia/kuwatangazia bidhaa yako, ni kama unawauzia wateja ambao hawapo. Na kujaribu kuwauzia wateja ambao hawapo, si tu unapoteza muda, bali ni kigezo kikubwa cha kutofanikiwa.

Kama unauza bidhaa maalum, anza kwa kujifunza wateja wako walipo. Mitandao ya kijamii imegawanyika. Watumiaji wa mitandao hiyo wamegawanyika vile vile. Ni kama soko la Kariakoo, kuna upande utakua unauza nguo sana, kuna upande unauza vitu vya elektroniki, na kuna upande unauza vifaa vya ofisini tu. Peruzi Twitter, Instagram, magrupu ya Facebook ili kujua.Kama unauza magari, kuna magrupu Facebook ya wauzaji na wanunuzi wa magari. Jiunge na magrupu ili kujifunza jinsi watu wanavyouliza maswali katika mitandao tofauti, vitu wanavyopenda n.k. Hii itakuwezesha kujua jinsi unavyoweza kuingiza biashara yako katika maisha yao ya kila siku.

3. Kutoelewa Msaada Unaohitaji ili Kuendesha Biashara Yako

makosa ya biashara ya mtandaoni

Biashara ya mtandaoni ni kubwa. Na kama unaamua kuingia kuifanya, basi ni vema kujua ni msaada . Kama unaamua kufungua tovuti na mitandao ya kijamii kwa ajili ya biashara yako, tafuta mtaalamu wa kukusaidia. Kama unaona hautaweza kuendesha mitandao ya kijamii peke yako, tafuta mtu wa kukusaidia.  Ni vigumu kufanya kila kitu kuanzia kuhudumia wateja (wanaopiga simu na wanaotuma meseji kwenye mitandao ya kijamii), kufanya mauzo na matangazo n.k

Kama umeamua kuwekeza katika biashara ya mtandaoni, basi ni vyema pia kutenga bajeti kwa ajili ya rasilimali watu. Unaweza kuandaa fungu kwa ajili ya watu watakaokusaidia katika kuunda na kuendesha mitandao yako. Kufanya hivi kunaweza kukusaidia kushughulikia mambo yale ambayo yanaweza kukuza biashara yako

4. Kushindwa Kutoa Kipaumbele kwa Huduma kwa Wateja

Kosa kubwa linalofanywa wakati wa kuanzisha biashara ya mtandaoni ni kuweka bidhaa bila kujali  huduma kwa wateja.. Kwa mazingira ya Kitanzania ambapo bado wateja wengi wana wasiwasi na masoko ya mtandaoni kwa ukionyesha dalili yeyote ya kushindwa kumridhisha basi unaweza kumkosa.

Kama unauza vitu mtandaoni, ni muhimu kujua nje ndani juu ya bidhaa yako. Unaweza ukawauzia watu kitu au huduma na maswali yakawa mengi juu ya matumizi. Kama utashindwa kujibu  utaonekana mbabaishaji. Jifunze kila kitu kuhusu bidhaa yako, maswali wanayoweza kukuuliza, changamoto n.k. Itakuwa rahisi sana wakipiga simu kuuliza maswali utaweza kuwasaidia. Hii itawatengenezea moyo wa kukuamini na kukutegemea. Mara nyingine wakitaka kitu/huduma, lazima wagonge mlango wako

5. Kutokuwa Na Mkakati wa Kutangaza Biashara

makosa ya biashara ya mtandaoni

Kama mmiliki wa biashara, kuwa na mkakati madhubuti wa kuitangaza na kuuza bia shara. Haijalishi unauza nini, ni lazima ujifunze na ujue namna na mahala pa kupata wanunuzi wa bidhaa yako. Mfano, ZoomTanzania inaruhusu mtu/kampuni kutangaza bidhaa na kufikia wanunuzi zaidi ya 20,000 wanaotembelea mtandao huo kila siku. Cha kuzingatia ni kujua tu jinsi ya kutangaza na jinsi ya kuwa na tangazo imara mtandaoni hapo.

Pia wauzaji wengi hawapuzii vitu kama punguzo la bei, nafasi ya kujifunza kutokana na takwimu za mitandao ya kijamii. Pia, kuwa na tovuti inayowezesha wanunuzi kukufikia au kufanya malipo kwa urahisi ili kupata bidhaa wanazotaka ni moja ya njia nzuri ya kuongeza wateja

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media