Hatua 5 za Kuwavutia Wateja Kutoka kwa Washindani Wako

  | 3 min read
0
Comments
4724
kuwavutia wateja kwenye biashara

Moja ya mafanikio makubwa katika kuboresha biashara yako ni kufanikiwa kuwavutia wateja wa mshindani wako kwenye biashara yako. Wateja wanahama. Lakini watafanya hivyo endapo tu wanaweza kuona thamani halisi ya pesa zao. Hivyo ni lazima uwape sababu nzuri ya kuchagua biashara yako na kuacha ya washindani wako.

Hivyo basi, unafanya nini kushindana na kukuza kapu lako la wateja katika soko lenye ushindani mkali?

1. Tafiti Kuhusu Washindani Wako

vuta wateja kwenye biashara

Bila kujali aina ya bidhaa unayouza — kama inatengeneza pesa, lazima iwe na washindani wako katika soko. Hivyo bila kung’ang’ania kwenye kuuza bidhaa yako moja, ni muhimu kutafiti mambo kadhaa kuhusu mshindani wako. Tafiti bidhaa na huduma za mshindani wako kujua nini wanatoa na nini hawatoi. Baada ya kujua hayo, sasa utaweza kutoa huduma nzuri ambayo wengine hawaitoi. 

Mfano, unaweza ukaangalia kama mpinzani wako anatoa au hatoi huduma kama vile kupeleka mzigo kwa mteja (delivery), kuwa na namba maalum ya huduma kwa wateja, huduma ya kumwekea bidhaa mteja (Install) n.k. 

2. Kuwa na Watu wanaopendekeza Bidhaa Yako

Moja ya njia nzenye nguvu zaidi za kuvutia wateja kutoka kwa mshindani wako ni maneno ya mdomo kutoka kwa watu wenye ushawishi. Mara nyingi huwa ni katika mitandao ya kijamii. Hawa wanaweza kufanya wateja wakuamini sana au wasikuamini kabisa. Kwa tafiti iliyofanywa, hakuna aina ya matangazo yanaweza kuwa na matokeo chanya kama mapendekezo mazuri kutoka kwa watu wenye ushawishi. Hivyo ili kufanikiwa, angalia watu wenye ushawishi wanaoweza kuendana na biashara yako, kisha watumie. Kwa wafanyabiashara wadogo, njia hii oia inaweza kuwa nzuri zaidi kwani mara nyingi haihitaji gharama kubwa sana. 

3. Cheza na Bei Pamoja na Ofa

vuta wateja kwenye biashara

Wateja ndivyo walivyo. Mara nyingi wanaangalia wauzaji wanaouza vitu nafuu zaidi. Kwa kuuza bidhaa zenye bei nafuu ukilinganisha na wapinzani wako unaweza kuvutia wateja wengi. Cha kuzingatia ni kuhakikisha ubora wa bidhaa unazowauzia. Wateja wanapendelea kununua bidhaa bora lakini kwa bei nafuu na si bidhaa mbou kwa bei nafuu. Hivyo, kama unauza bidhaa zinazofanana na za wapinazi wako, basi angalia namna ya kutoa vitu kama ofa, au kuounguza bei kidogo kwa idad fulani ya bidhaa zitakazonunuliwa. Ili kuwatoa wateja kutoka kwa mshindani wako ni wazi kuna gharama zake ambazo huna budi kuzikubali. 

4. Tafuta Mianya na Mapungufu

Pia ni muhimu kuumiza kichwa sana kuhusiana na soko la biashara yako ilipo. Ni lazima uwe unatafuta, kuvumbua na kuziba mapengo yaliyopo kwa bidhaa na huduma mpya. Moja ya njia nzuri zaidi ya kuwavutia wateja wapya si tu kutoa huduma ya kipekee, bali kutoa huduma ambayo inakosekana katika soko. 

Tumia mitandao ya kijamii kifikia soko lako. Uliza maswali kuhusiana na bidhaa na huduma ambazo wateja wangependa kuziona zinapatikana. Sawa, mshindani wako anaweza kuja na bidhaa mpya utakayoiingiza sokoni, lakini wewe ndio wa kwanza na mara nyingi wa kwanza huwa wanapata wateja waaminifu. 

5. Wape Kipaumbele na Kuwasaidia Wateja

vuta wateja kwenye biashara

Utafiti uliofanywa na Oracleunaonyesha kuwa, 89% ya wateja wanaweza kuhama kampuni kama kukiwa na huduma mbovu kwa wateja. Kwa miaka ya sasa, shukrani nyingi ziende kwenye mitandao ya kijamii, huduma kwa wateja imekuwa rahisi na la moja kwa moja. Mtandao kama Twitter umewawezesha wateja kupata msaada moja kwa moja huku wateja wengine wakiona namna kampuni zinavyowasaidia. 

Ni muhimu kujenga uhusiano binafsi na wateja wako, hasa kwenye mitandao ya kijamii na barua pepe. Mtandao wa SpotOn unaonyesha kuwa 41% ya wateja wako radhi kununua kutoka kwenye makampuni yanayowatumia email za ofa/bidhaa zilizo maalum tu kwa ajili yao.

Haihitaji kufikiria sana: Ukitoa huduma nzuri kwa wateja — ndivyo utavutia wateja wengi zaidi — na muhimu zaidi utaweza kuwafanya wateja wengi zaidi waamini biashara yako

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media