Pata Pesa Kwa Kuuza Vitu Usivyovitumia Nyumbani Kwako

  | 3 min read
0
Comments
2725
kuuza vitu usivyovitumia

Wakati mwisho wa mwaka unakaribia, unaweza kuwa na shida ya fedha za haraka, au unataka kupunguza baadhi ya vitu nyumbani. Unaweza kutengeneza pesa nzuri kwa kuuza vitu vingi ambavyo huvihitaji nyumbani kwako. 

Watu wengi wanapuuzia thamani ya vitu ambavyo hawavitumii majumbani mwao, au wanadhani  ni vigumu sana kuviuza, lakini si kweli. Wewe unaweza kuona kitu fulani kina thamani ndogo sana kukiuza baada ya kukitumia. Lakini, kuna mtu anatamani sana kitu hicho hicho.

Na ukweli mwingine ni kwamba, watu wengi wana vitu majumbani mwao ambavyo viko katika hali nzuri lakini hawavitumii tena. Inaweza kuwa simu ya zamani, viti, fremu za picha, magodoro, nguo za watoto, viatu, vitabu, n.k. Sasa, badala ya kuviacha viharibikie stoo, au vimalize nafasi katika nyumba yako, kwanini usiuzie watu wengi wanaovitaka?

Unaweza Vipi Kuuza Vitu Usivyovitumia Mtandaoni? 

Ni muhimu sana kujua sehemu sahihi ya kwenda kuuza bidhaa zako. Kuna sehemu nyingi za kuuzia bidhaa. Unaweza kuzitangaza Facebook, Instagram au Twitter. Lakini kwa uhalisia, mitandao hii sio rafiki sana kwa kuuza na kununua kutokana na kuongezeka kwa akaunti feki, utapeli n.k. Hivyo inakuwa ngumu mtu kukuamini na kuja kununua kwako. Lakini, mtandao kama ZoomTanzania ambao umekuwa kwenye biashara kwa zaidi ya miaka 10, ni njia rahisi na inayoaminiwa na watu wengi kununua na kuuza vitu vilivyotumika. Hii ni kwa sababu ya wauzaji wanaouza bidhaa zao ZoomTanzania kuhakikiwa kabla ya kuuza bidhaa zao. 

Hivyo basi, unapofikiria kuhusu sehemu za kuuza vitu vyako mtandaoni, unapaswa kuzingatia vitu kama:

Sifa: Je, wanunuzi wanachukulia vipi tovuti hii kuwa ya kuaminika?

  • Tovuti unayotaka kutangazia, je ni rafiki kwa watumiaji? Je! Itakuwa rahisi kwa watu wanaotafuta bidhaa mkondoni kupata vitu vyako?
  • Kuna gharama yoyote ya wewe kuuza vitu vyako?

Baada ya kuamua hivi, sasa unahitaji kujua nini cha kufanya ili kuhakikisha kwamba vitu vyako vinavutia wateja wengi na kuuza haraka.

1. Piga Picha Nzuri

Picha inazungumza mengi. Wateja wengi sana wanavutiwa na bidhaa, si tu kwa sababu walikua wanaitaka bidhaa hiyo, bali kwa namna ilivopigwa picha na inavyoonekana.. Jambo zuri ni kwamba  hauhitaji kuwa na kamera ya bei ghali ili kupata picha nzuri. Unaweza kutumia simu kwa urahisi na haraka zaidi. Cha kuzingatia:

  • Piga picha ya bidhaa zako kutoka pembe tofauti.
  • Hakikisha hakuna vitu vingi vinavyoweza kuharibu mwonekano wa picha yako. Hivyo unaweza kupiga sehemu yanye rangi moja, mfano juu ya kitambaa cha rangi nyeupe kama inawezekana.
  • Pia hakikisha picha inaonekana vizuri na umepiga sehemu yenye mwanga wa kutosha. 
  • Hakikisha picha haitingishiki. 

2. Weka Kichwa cha Habari Kinachovutia

Mbali na picha, kitu cha kwanza ambacho kitawafanya wanunuzi wagundue  bidhaa yako ni kichwa unachotumia kuielezea. Hakikisha kinaeleweka kirahisi na kwa ufupi. Kwa mfano, kama unauza Televisheni, kichwa cha habari kirahisi kueleweka kingekuwa: TV ya Samsung HD 

Pia unaweza kutumia maneno mazuri ya kuvutia kama vile kubwa, nzuri, ya kisasa, maridadi ili kumvutia mnunuzi. Cha msingi ni kuzingatia ni kutumia sifa zinazoakisi kweli wa bidhaa yako.

3. Andika Maelezo Muhimu

Haya ni muhimu sana kwani ukiona mtu amefikia kuyasoma basi ujue uliandika kichwa kizuri cha habari na msomaji amevutiwa na anataka kujua zaidi. Hivyo zingatia: 

  • Kuwa mwaminifu kwa kuzingatia sifa na ubora halisia  wa bidhaa hiyo.
  • Andika kwa lugha rahisi, ambayo mtu yeyote akiona ataelewa.. Mfanye msomaji atamani kuimiliki bidhaa hiyo.

Hiyo ndivyo watu wengi wanaweza kuuza bidhaa zao kirahisi. Unaweza pia ukasoma zaidi juu ya kutangaza bidhaa yako Zoomtanzania au namna ya kuboresha tangazo lako. Kazi ni kwako. Anza kwa kuweka siku ya kupunguza vitu nyumbani kwako kwa kuvipiga picha na kuviuza ZoomTanzania.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media