Hatua 5 Muhimu za Kuzingatia Wakati wa Kuuza Kiwanja

  | 4 min read
0
Comments
5424
kuuza kiwanja

Mchakato wa kufanya mauzo ya kiwanja unaweza kuwa mgumu kama utashindwa kulenga wateja sahihi. Uuzaji wa kiwanja ni  moja ya mauzo yanayohitaji mbinu yakinifu. Kuna sababu tofauti zinazoweza kukufanya uamue kuuza kiwanja chako. Labda umerithi kiwanja ambacho hakiko kwenye mipango yako ya kukiendeleza, au umeamua kwenda kuishi sehemu nyingine, ama umepata changamoto za kifedha na unahitaji kujipatia kipato cha kukukwamua. Sababu ziko nyingi.  

Kabla ya kuuza kiwanja, hasa ambacho hakijaendelezwa, muuzaji lazima atafakari  kwa makini ni kitu gani kinakipa thamani kiwanja hicho. Hii inamaanisha kuwa bei uliyo iweka lazima iakisi vitu thamani ya kiwanja.

1. Thaminisha Ardhi Kutoka kwa Jicho la Mnunuzi

kuuza kiwanja mteja

Hatua ya kwanza kabla ya kuuza kiwanja ni kupanga bei. Unaweza kukosea kwa namna mbili, aidha kwa kuweka bei ndogo sana au bei ya juu sana. Kinachotakiwa ni kuweka bei sahihi itakayochochea mauzo ya haraka. Ili kujua thamani halisi unaweza kulinganisha bei ya viwanja vya eneo hilo. Kama si mjuzi, unaweza ukaajiri dalali  wa viwanja ili akusaidie kukithaminisha. Unaweza kujua thamani halisi kulingana na bei ya soko la wakati huo. Mfano, bei ya kiwanja heka moja kipindi cha nyuma itakuwa tofauti na bei ya kiwanja hicho hicho kwa leo. Pia itakua rahisi kwani dalali atasaidia kutoa taarifa kwa madalali wenzake ambao watasaidia upatikanaji wa wanunuzi.

2. Andaa Kiwanja Chako

Baada ya kuthaminisha kiwanja chako, inatakiwa ukifanye kiwanja chako kionekane kina thamani hiyo. Majani yasiyoeleweka, mashimo au miinuko inaweza kufanya mnunuzi asione uzuri na thamani ya kiwanja hiko. Ukishindwa kuonyesha thamani ya kiwanja, utakuja kulazimisha kushusha bei chini ya  kiwango ulichojiwekea. 

Hivyo ili kuepuka hili fanya kiwanja chako kionekane chenye thamani na kizuri. Weka alama za mipaka vizuri, majani na miti punguza, magugu ondoa, vichake vifyeke na tengeneza njia za kutembea kwenye kiwanja. Hakikisha mnunuzi anaweza kusimama katika pande yeyote na kuona kiwanja vizuri. 

3. Weka Matangazo 

kuuza kiwanja weka tangazo zoomtanzania

Ukishakiweka  kiwanja chako kwenye hali nzuri na kukipa bei sahihi, basi  ni wakati wa kuwajulisha wanunuzi. Cha kwanza utakachohitaji ni sehemu ya kukitangazia. Kwa sasa watu wanauza kila kitu mtandaoni, viwanja vikiwa  ni mojawapo.

Inachotakiwa ni kuhakikisha una kila taarifa inayotoa maelezo ya kutosha kuhusu kiwanja chako. Hakikisha unaweka malezo ya kiwanja (eneo, ukubwa n.k) picha tofauti za kiwanja, na ramani ya jinsi ya kufika kwenye kiwanja n.k. Kitangaze kiwanja chako kwenye mtandao wa ZoomTanzania ambapo unaweza kuweka tangazo lako bila malipo yoyote

4. Tengeneza Mfumo wa Malipo wenye Tija

Sio kila mnunuzi wa kiwanja atakuwa tayari kufanya malipo ya fedha zote kwa wakati mmoja. Kuna baadhi ya wateja ambao wanafanya malipo kwa awamu Kama hautakua na uhitaji wa fedha yote kwa mkupuo, unaweza kuruhusu mfumo ambao mnunuzi wa kiwanja anaweza kulipa kwa nyakati tofauti kwa riba kidogo.  Kumbuka kuanisha hili katika tangazo lako kunaweza kuwavutia watu wengi zaidi.

Lakini kwa upande mwingine, unaweza kujiweka  katika hatari pale mnunuzi atakapokuwa msumbufu kwenye kumalizia malipo yaliyobaki. Ili kuepuka hili, hakikisha unaajiri mwanasheria atakaesimamia mkataba wa malipo kati yako na mnunuzi kwa kufuata sheria za nchi. Pia hakikisha kiasi cha kutosha kinatangulizwa na kinachobaki kinakuwa na tarehe maalum ya kumaliziwa. 

5. Kufanya  Mauzo

kuuza kiwanja mkataba wa kufanya mauzo

Sasa Umepata mnunuzi ambaye yuko tayari kufanya malipo. Hapo utakuwa umefika hatua muhimu. Hapa kuna  makubaliano baina yako, mwanasheria na mnunuzi. Kwa kawaida hatua hii hujumuisha vitu vifuatavyo:

  • Mkataba wa uuzaji
  • Hati ya uhamisho wa ardhi inayoonyesha kuna uhamisho wa umiliki kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi
  • Malipo na makabidhiano ya hati muhimu kama vile:
    • Risiti kinachoonyesha malipo ya kodi ya kiwanja ya kila mwaka. Hii inamaanisha kuwa, muuzaji anatakiwa  kufanya malipo yote ya kodi ya kiwanja kabla ya kukiuza ili mnunuzi asipate deni.
    • Usajili wa uamisho wa ardhi baada ya malipo yote muhimuunaofanyika kwa Msajili wa Hifadhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Watu. 

Njia bora na rahisi ni kumtafuta mwanasheria pamoja na wataalam watakaosimamia uhamishaji wa hati za umiliki kutoka kwako kwenda kwa mnunuzi. Kufanya mauzo ya kiwanja yanahitaji umakini mkubwa katika hatua ya mwisho. Na njia bora ya kupata vitu hivi vyote ni kuajiri mwnasheria atakaesimamia vyote kwapamoja.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media