Njia 5 za Kupata Pesa Zaidi Wakati wa Kuuza Fanicha Zilizotumika

  | 3 min read
0
Comments
1598
kuuza fanicha

Sababu za kuuza fanicha/samani ulizozitumia ni nyingi. Inaweza kuletwa na sababu tofauti. Inawezekana unataka kununua mpya na nzuri zaidi, una mpango wa kuhamia sehemu ya mbali na hutaki kwenda nayo. Au pia unaweza kuwa tayari una fanicha mpya hivyo hutaki kujaza nafasi kwenye nyumba yako.

Sababu zinaweza kuwa nyingi. Lakini kwa namna yeyote ile, ukiamua kuuza fanicha zako utataka kuuza kwa bei nzuri na kwa haraka zaidi. Ili uweze kuuza kwa haraka na kwa bei nzuri, hizi ni njia muhimu za kufata:

1. Tambua Hali ya Samani Yako

tambua thamani ya fanicha yako wakato wa kuuza fanicha

Jambo la kwanza unapaswa kufanya ni kuangalia hali ya kitu chako. Kama ni kochi au meza, viko katika hali gaini? Je, vina alama za michubuko? Je, mwonekano wake bado mzuri? Ukiweza kuainisha vitu kama hivi itakuwa rahisi kujua kiasi gani unaweza kupunguza ili kupata bei halisi ya samani yako.

Lakini pia unaweza kuangalia kitu kinachoweza kuipa thamani fanicha yako. Mfano unaweza kuangalia vitu kama aina ya mbao au jina (brand) ya fanicha unayotaka kuuza. Vyote hivi vitakusaidia kuthaminisha bei ya fanicha yako. 

Baada ya hapo fikiria ni kiasi gani ulilipia na umetumia muda gani mpaka sasa. Hii itakusaidia kupata bei sahihi ya kuuzia kwa kutoa fedha ya kununulia na thamani iliyopotea kwenye ubora au mwonekano wa bidhaa yako.

2. Amua ikiwa Unataka Kuuza Kwa Haraka au La!

Watu wengi hawajui kuwa muda una nafasi kubwa katika mchakato wa kuuza fanicha iliyotumika. Ikiwa unahitaji kuuza fanicha yako kwa haraka, inashauriwa kupunguza bei ya bidhaa yako. Hii inaongeza nafasi za kuuza fanicha yako kwa haraka. Kwa nini? Mara zote watu wanatafuta bei rahisi.

Kwa upande mwingine, ikiwa huna haraka, unaweza kuuza bidhaa yako kwa bei ya juu na kusubiri kuanzia hapo. Ikiwa thamani ni sawa na bidhaa, mnunuzi sahihi atakuja tu!

3. Jifunze Jinsi ya Kujadili Bei

jifunze jinsi ya kujadiliana bei wakati wa kuuza fanicha zako

Kwa kawaida, wakati wa kuuza mtafikia muda wa kujadiliana bei na mnunuzi wa fanicha unayouza. Wewe unataka upate bei nzuri kwenye fanicha yako na wakati huo huo mnunuzi nae anataka anunue kitu cha bei rahisi. Wote mnakuwa kwenye hali mbili tofauti kabisa, lakini mara zote kuna mahali pa mkutano: mahali ambapo wot mnapata thamani katika ununuzi huo.

Usisite kuhusu kutaja bei yako hata kama muuzaji atataja bei ya chini sana. Kama tulivyoona hapo juu, muuzaji unaweza kutaja bei kwa kuangalia uhitaji wake wa pesa. Kama unadhani bei aliotaja ni ndogo sana kukupa faida au kufikia bei uliyoiweka. Lakini pia kama huna muda mwingi, basi usisite kumfanya apande dau na kama hatafika basi angalau awe ameikaribia. Wakati mwingine bei hiyo inaweza kuwa bora ukilinganisha na gharama za kurekebisha, kusafirisha au kupotea ikiwa utaamua kuiacha iendelee kuozea ndani.

4. Kuwa Muwazi Juu ya Uzima wa Fanicha Yako

kuwa muwazi wakati wa kuuza fanicha zako

Ni kawaida kwa fanicha kupata uharibifu kidogo wakati wa matumizi. Wewe unalijua hili na wanunuzi wanalijua pia. Kuwa mkweli na toa maelezo ya kutosha ukiambatanisha picha za fanicha zioneshazo mikwaruzo, michaniko, sehemu uliyorekebisha n.k. 

Wanunuzi wanapenda kujua wananunua nini mapema. Wengi huwa hawajali kuhusiana na uharibifu mdogo (ili mradi uendane na thamani) na ni bora tu wajue mapema. Kumbuka kwamba soko la bidhaa zilizotumika linategemea kuaminiana. Mnunuzi kumuamini muuzaji na hii ndio inayowahimiza watu kununua vitu vilivyotumika kwa mtu ambaye hawajawahi kukutana naye.

5. Jiongeze

Mwisho, hakikisha unatambua sehemu sahihi ya kuwafikia wateja wako na kwa bei sahihi. Orodhesha bidhaa zako kwenye mtandao wa ZoomTanzania ili kufikia jamii kubwa ya wanunuzi katika mtandao huu. Njia ya kujiunga ni rahisi, hakuna gharama yeyote na ni rahisi kupata wateja wengi kutoka kwenye bidhaa yako. Ukitaka kujua jinsi ya kuuza bidhaa yako kwa haraka na usalama unaweza kusoma makala hii tuliyoandika siku za nyuma kuhusiana na jinsi ya kuuza bidhaa zako katika mtandao wetu

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media