Mambo 5 Ya Kuzingatia Ukitaka Kutoka na Familia Kula Ftari

  | 3 min read
0
Comments
833
Familia Kula Ftari

Kupata muda wa kufurahi na familia yako wakati wa Ramadhan inaweza kuwa changamoto. Ukifikiria muda kazi, muda wa kufuturu,  muda wa ibada za usiku kucha, unaweza kudhani kuwa hauna muda kabisa kwa ajili ya familia. Lakini, mwezi huu ndio mwezi ambao ni muhimu sana kupata  muda nao., Ni muda ambao unaunganisha familia na Mungu wao.

Katika kufurahia mwezi huu na familia, unaweza kuamua kuwatoa nje kwa ajili ya kubadilisha mazingira na kula mlo wa ftari tofauti na waliouzoea. Pia ni wasaa mzuri wa kuwapumzisha  wanaoandaa ftari kila siku. Ikiwa ungependa hili, basi ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Chagua Eneo/Mgahawa Wenye Mandhari Rafiki Kwa Kifamilia

Familia Kula Ftari

Wakati wa kuchagua sehemu ya kwenda kupata ftari na familia, ni muhimu kuzingatia uwezo wa mgahawa kuhudumia familia familia nzima. Zingatia vitu kama umbali wa eneo, kelele, huduma, usafi, wapishi n.k. Pia baadhi ya sehemu zinaweza kuwa na meza zenye uwezo wa kuwahudumia watu wachache tu kwa wakati mmoja, hivyo ni muhimu kujua kabla ya kufika ili kuepusha usumbufu.. Unaweza kushirikisha  familia yako wakati wa kuamua eneo la kwenda ili kila mtu afurahi.

2. Fanya Hifadhi (Booking) ya Meza ya Familia Mapema

Baada tu ya kuamua sehemu mnayotaka kwenda, piga simu kwenye mgahawa huo na kufanya hifadhi (booking) kwa ajili ya familia. Unaweza kupata namba za simu za mgahawa unaoutaka kwenye orodha ya namba za migahawa katika mtandao wa ZoomTanzania.  Wasiliana nao kuwajulisha idadi ya wanafamilia mtakaokuwepo, na pia kuwajulisha kama kuna aina ya mkao mtakaochagua kuandaliwa. Mfano, kuna baadhi ya migahawa ina meza ndogo na haiwezi kuhudumia meza ya watu 10 kwa wakati mmoja. Lakini kuna baadhi ya migahawa inaweza kuunganisha meza au kuwekwa meza zinazokaribiana. Ukiwasiliana na wahudumu mapema na mkaelewana basi ni rahisi kufanya hifadhi.

3. Jua Orodha na Bei za Vyakula Vinavyoandaliwa

Familia Kula Ftari

Tofauti na baadhi ya migahawa ambayo huwa inauza aina fulani ya vyakula tu, mfano Pizza, Kuku n.k, baadhi ya Migahawa na Hoteli huwa na mlo maalum mwezi huu wa Ramadhani. Wengi huwa na menu za kujichagulia (Buffet) kwa ajili ya ftari.  Menyu ya buffet hiyo kwa kawaida huwa na vianzio mfano uji, chai, maziwa — kisha milo kama biriani, viazi, mihogo, kababu, kuku wa kuungwa n.k. Unaweza kuwapigia kuulizia menyu ya mwezi huu wa Ramadhan au kuangalia katika orodha mbali mbali katika mtandao.

4. Hakikisha Mnafika Kwa Wakati

Kwa kawaida kukutanisha  wanafamilia, ndugu na jamaa sio kitu  rahisi. Katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhan, kila mwanafamilia anaweza akawa anatokea upande wake, au kunaweza kuwa na mpango wa kukutana nyumbani na kuondoka kwa pamoja. Kama ni hivi,  ni vema kufika eneo la tukio kwa wakati na kwa pamoja. Fikiria, kama mmeweka oda ya chakula cha watu 8, kisha watu 6 wakawahi kufika wakati wa kufuturu, kuna usumbufu mkubwa wa kusubiri. Ni muhimu kama unapanga kuitoa  familia yako kuhakikisha watu wote wanafika kwa wakati. Pia kama mnatoka pamoja, basi ni vema kuzingatia bugdha kama foleni, kwa miji mikubwa mfano Dar es Salaam.

5. Kuwa Na Uvumilivu

Familia Kula Ftari

Msimu huu wa Ramadhani, migahawa na sehemu nyingi za chakula zinakuwa na watu wengi sana hasa wakati wa kufuturu. Hii inapelekea wakati mwingine vyakula kupungua au kuchelewa kidogo kutokana na wingi na ukubwa wa oda. Ni muhimu sana kuzingatia hili hasa unapotoka na familia yako kula ftari. Kubali kuwa mwelewa ikitokea umeagiza kichwaji au chakula na kikachelewa kidogo.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media