Mambo 6 Ya Kuvutia Unayopaswa Kuyajua Kuhusu  Eid Al Fitr

  | 3 min read
0
Comments
1970
eid al-fitr na familia

Moja ya siku muhimu sana katika kalenda ya Kiislamu ni Eid al-Fitr. Husherekewa siku mbili, kuhitimisha  mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao hudumu kwa mwezi mmoja. Tuangalie kwa umakini tamaduni za sikukuu hii, ambazo kwa asili yake husherekewa na familia, na jamii.

1. Eid al-Fitr Inaashiria Mwisho wa Ramadhan

eid al-fitr na familia mwisho wa mwezi wa ramadan

Eid al-Fitr hufanyika siku ya kwanza ya Shawwal, mwezi wa Kiislamu unaokuja moja kwa moja baada ya Ramadan. Wakati wa Ramadhani, Waislamu wanalazimika kuacha kula, kunywa na shughuli nyingine za dhambi.  Ni lazima kuzingatia hili ili kupata wakati wa kutafakari na kuabudu. Ukijulikana kama Mwezi Mtakatifu wa Kiislam, Ramadhan inaashiria wakati ambapo Quran takatifu ilifunuliwa kwa nabii Muhammad (saw).

2. Haiwezi Kuanza Mpaka Mwezi mpya Umeonekana

Kalenda ya Kiislam huongozwa  na kuzama na kuchomoza kwa mwezi. Hii ndio sababu Eid al-Fitr huanguka siku na tarehe tofauti katika kalenda ya kawaida (Gregory) kila mwaka. Kwa mujibu wa tamaduni, Eid al-Fitr haiwezi kusherehekewa  mpaka mwezi mpya umeonekana kwa macho ya kawaida (bila kutumia darubini). Hivyo ni kawaida kabisa kwamba sehemu fulani za ulimwengu zinaweza kusherehekea Eid al-Fitr tarehe tofauti na wengine. Mwaka huu, Eid al-Fitr inatazamiwa kusherekewa kati ya tarehe 4, 5 au 6 ya mwezi Juni.

3. Tafsiri Yake Ni ya Sikukuu Ya Kuvunja Saumu

eid al-fitr na familia kuvunja saumu

Baada ya kujikataza kula chakula na maji wakati wa masaa ya mchana kwa mwezi mzima, Waislamu wengi wanafikia wakati wa kuvunja ibada yao ya kufunga. Inatafsirika kama “Sikukuu ya kuvunja Saumu,” vyakula vina nafasi muhimu sana siku hii ya Eid al-Fitr. Kifungua kinywa cha asubuhi kina umuhimu wake, ikijumuisha vitu vitamu vyenye sukari. Kwa Tanzania, utasikia vitu kama ‘Maadazi ya Eid’ kalimati na chai ya Maziwa. Kisha, familia zinakusanyika kwa chakula cha mchana siku hiyo hiyo baada ya sala ya asubuhi. Vyakula vya kila aina vya kikabila huliwa katika sherehe hii ya ya kufurahisha, huku watu wa dini mbalimbali wakijumuika na familia za Kiislamu kusherekea siku hii.

4. Nguo Mpya na Zawadi ni Utamaduni wa Eid al-Fitr

Pia siku ya Eid al-Fitr ni desturi ya watu kuvaa mavazi ya aina mpya. Katika dini ya Kiislamu, hupewa tafsiri kama sehemu ya kumuheshimu Mwenyezi Mungu na inalenga kuashiria wazo la upya wa nafsi kwa  Muislamu aliyesamehewa dhambi zake mwezi wa Ramadhan. Pia, siku hii hujumuisha zawadi hutolewa kwa watu waote. Kama ilivyo kwa sikukuu ya Krismasi katika ulimwengu wa Kikristo, siku ya Eid al-Fitr ni wakati ambapo Waislamu wanaweza kuwaonyesha upendo wapendwa wao kwa zawadi. Watoto hupata zawadi zaidi, ingawa zawadi hutolewa kati ya marafiki na ndugu na watu wasio na uwezo.

5. Kutoa Hakuangalii Uwezo wa Familia

eid al-fitr na familia zawadi kwa masikini

Waislamu wote wenye uwezo wa kifedha wanapaswa kulipa Zakat al-Fitr, aina ya sadaka maalum ambayo inalenga kuimarisha uhusiano ndani ya jamii ya Kiislamu na hisia za undugu na upendo. Mfumo huu huwawezesha watu masikini kuingizwa katika sherehe za Eid al-Fitr, kwa nia ya kuhimiza  watu wenye uwezo wa kifedha kuwa na ukarimu zaidi mwaka mzima.

6. Ni Sherehe ya Watu Wote na Sio Waislamu Tu

Eid al-Fitr inaadhimishwa kama sherehe ya umma ili kujenga maana zaidi kwa jamii. Maonesho  mazuri huendelea kipindi hiki, viwanja vya michezo ya watoto, mashindao tofauti n.k hufanyika katika maeneo ya umma.. Salamu kuu ya siku hiyo huwa ni “Eid mubarak” (Sikukuu Njema). Sikukuu huendelea vizuri hadi usiku. Pia katika sehemu nyingi za dunia, watu wa dini tofauti wanahimizwa kutembelea nyumba za marafiki zao wa Kiislam na kujiunga katika  sherehe kwa kufurahia mlo wa siku hiyo na kubadilishana zawadi.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media