ZoomTanzania Kuwazawadia Madalali Kupitia Dalali Bomba

  | 2 min read
0
Comments
2577
dalali

ZoomTanzania imeendelea kuwanufaisha Madalali wa nyumba, viwanja na magari kwa kuanzisha shindano litakalojulikana kama Dalali Bomba Awards. Sindano hilo lenye lengo la kuongeza idadi ya madalali wa nyumba, viwanja na magari mtandaoni, litafanyika kwa mwezi mmoja na litakuwa na mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu.

Ili kushiriki, madalali waliopo katika mtandao wa ZoomTanzania wanatakiwa kutambulisha madalali wapya kwenye Mtandao huo  ambao watatakiwa kuweka matangazo ya nyumba, viwanja au magari ili ili kuwafikia zaidi ya watembeleaji 20,000 kwa siku wanaotembela mtandao wa Zoomtanzania. 

Washindi Wanashinda Nini?

Washindi watajinyakulia vocha zenye thamani ya shilingi 340,000/- (Mshindi wa Kwanza), Shilingi 230,000/- (Mshindi wa Pili) na Shilingi 115,000/- (Mshindi wa Tatu)  ambayo ataweza kuitumia kununua kitu chochote atakachokitaka katika mtandao wa ZoomTanzania

“Lengo letu ni kuhakikisha kila Mtanzania anaweza kupata nyumba, kiwanja au gari akitembelea ZoomTanzania. Hivyo ili kutimiza, ni lazima kuwe na wigo mpana wa madalali kutoka kila kona. Hii itawezesha mtu yeyote akitaka nyumba, gari au kiwanja popote akikute ZoomTanzania.” Alifafanua Hawa Mwakatundu, Meneja Mauzo ya Biashara kwa Biashara, ZoomTanzania.

Elimu ya Ujasiriamali

Kwa madalali wapya watakaotambulishwa, watapatiwa elimu ya ujasiriamali kupitia mtandao na namna wanaweza kuwafikia wateja wengi zaidi. 

“ZoomTanzania imekuwa ikikutana na madalali mara kwa mara ili kujadili na kuwaelimisha madalali hao namna wanaweza kutumia mtandao; kwa lengo la kuwafikia maelfu ya wateja wapya kila siku.” Erca Uisso, Meneja wa Kampeni za ZoomTanzania alifafanua. “Hili ni zoezi endelevu na litakuwa linafanika kila mwezi kuhakikisha madalali wanapata urahisi wa kuwafikia wateja kupitia mtandao” Erca aliongeza

Dalali Meet & Greet

Katika kikao cha mwisho kilichofanyika ofisi za ZoomTanzania, Masaki Dar es Salaam – Madalali walielimishwa namna ya kuwa salama mtandaoni. Pia walifundishwa namna ya kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia mtandao. 

Pia, elimu kuhusu mtandao na matumizi yake kwa madalali inaendelea kutolewa kwa madalali tofauti kupitia kikundi maalum cha App ya Whatsaap  kilichoanzishwa kwa ajili ya madalali wote waliopo na ambao hawapo ZoomTanzania. Dalali anaweza kujiunga katika ‘group’ hili kwa kubofya link hii: https://chat.whatsapp.com/Dq0MgvEvenlEGEF1PEZGx0

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media