Tangazo Kuhusu COVID-19 kwa Wateja Wetu wa ZoomTanzania

  | 3 min read
0
Comments
2721

Wapendwa Wauzaji na Wanunuzi,

Tunapenda kuwashukuru kwa kuendelea kutuamini kama mtandao namba moja unaowaunganisha wauzaji na wanunuzi tangu mwaka 2009. Tunashukuru na ni lengo letu kuhakikisha tunawaridhisha zaidi ya hapa. 

Kama ilivyo katika maeneo mengine duniani, timu nzima ya ZoomTanzania inatambua uwepo wa janga la COVID-19, kusambaa kwake na jinsi linavyoathiri maeneo mengi, ikiwemo biashara. 

Hivyo, ili kuendelea kuwahudumia watu wengi zaidi iwezekanavyo huku tukiwa makini kuhakikisha tunajikinga na ugonjwa huu, kutakuwa na mabadiliko kidogo ambayo hata hivyo hayataathiri utendaji wa namna matangazo na mauzo yanavyofanyika katika mtandao wetu. 

Hivyo kazi kwetu zinaendelea kama kawaida. Wafanyabiashara wengi wadogo wanaotumia ZoomTanzania wanatutegemea kuhakikisha biashara zao zinaendelea kuwa wazi na wafanyakazi wao kuendelea kufanya kazi. Hii ndio sababu tunawaunga mkono wafanyabiashara wadogo katika hali ya usalama na uwajibikaji. Pia wanunuzi zaidi ya 20,000 wanaotembelea ZoomTanzania kila siku wanategemea kununua bidhaa mtandaoni kwa usalama na hivyo kupunguza hatari ya kuambukizwa/kusambaza COVID-19. Hivyo basi:

Kwa Wauzaji Wanaotangaza Biashara ZoomTanzania

  • Asilimia 100% ya wafanyakazi wa ZoomTanzania watafanya kazi kutokea nyumbani ili kupungua uwezekano wa kuambukizwa / kusambaza virusi vya COVID-19. Hata hivyo, hili halitaathiri kitu chochote kwa watu wanaotangaza bidhaa zao kwani huduma zitakuwepo 100% kama kawaida kwa masaa ya kazi ya kawaida.
  • Pia, kwa sasa tunapitia kila bidhaa zinazotangazwa katika mtandao wetu, zile zinazoendana na janga la virusi vya Corona, kuhakikisha haziongezwi bei na watembeleaji wetu hawauziwi kwa bei zisizofaa, au kutapeliwa.
  • Kwa wauzaji wanaouza bidhaa huu ni wakati wa kuonyesha thamani ya biashara yako kwa wateja. Waonyeshe wateja upendo kwa kutoa huduma ya kufikisha bidhaa (delivery) hadi walipo ili kupunguza hatari ya wao kuambukizwa au kusambaza COVID-19

Kwa Wanunuzi Wanaotafuta Bidhaa ZoomTanzania

  • Matangazo ya bidhaa zote muhimu yataendelea kuwepo ZoomTanzania kwa wakati wote. Timu ya ZoomTanzania itaendelea kuhakikisha bidhaa nyingi zaidi zinapatikana kipindi hiki.
  • Epuka kufunga safari kwenda sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi ili kupata bidhaa. ZoomTanzania inawauzaji wanaoweza kufanya ‘Delivery’ ya bidhaa wanazouza hadi ulipo kwa gharama nafuu. Ukitaka kujua kamaa muuzaji anafanya delivery, bofya kitufe kilichoandikwa Delivery wakati wa kutafuta bidhaa yako kama kiavyoonekana katika picha.

tangazo Covid-19 zoomtanzania

World Health Organisation (WHO) wanashauri kuwa, njia nzuri zaidi za kupunguza kusambaa kwa irusi vya COVID-19 ni pamoja na; kuepuka mikusanyiko ya watu, kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka kushika macho, pua na mdomo; na kuona wataalam wa afya mara tu utakapohisi una dalili za Corona (homa, kukohoa na kupata shida wakati wa kupumua). 

WHO - COVID-19

Ili kujilinda na kulinda afya ya timu nzima ya ZoomTanzania, wafanyakazi wote watafanyia kazi kutokea nyumbani. 

Hata hivyo, tuko na tutaendelea kuwepo kupitia namba za simu, barua pepe na mitandao ya kijamii kwa nyakati za kazi.

Wasiliana nasi kupitia: Huduma kwa Wateja: +255655140602, Mauzo: +255677057375, Barua pepe: info@zoomtanzania.com. Pia tembela kurasa za mitandao yetu ya kijamii: LinkedIn, Twitter, Instagram & Facebook

Tunashukuru kwa uelewa wako na tunakutakia heri katika wiki chache zijazo.

Timu ya ZoomTanzania.

 

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media