Biashara Mtandaoni: Kwa nini Utangaze Na ZoomTanzania?

  | 4 min read
0
Comments
1310
biashara-zoomtanzania

Mwelekeo wa mafanikio ya biashara za Mtandaoni unaendelea kuonekana na hauonyeshi dalili zozote  za kupunguza Unaweza kuwa bidhaa na ukataka kufikia wateja. Lakini, kama unataka kufikia wateja kwa haraka na kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara yako, basi ni muhimu kutaingaza biashara yako ama kuweka tangazo lako kwenye jukwaa la  ZoomTanzania

Haijalishi unafanya biashara gani.  Hata ikiwa ni ya ya kufyetua tofali.  Biashara yako ikiwa mtandaoni inakuhakikishia urahisi wa kufikia wateja na ukuaji. Hizi ni baadhi ya faida ya kutangaza biashara yako kwenye mtandao wa ZoomTanzania

1. Hakuna Gharama Za Kutangaza 

biashara zoomtanzania

Ukiweka kitu chako kwenye mtandao wa Zoom Tanzania, haichajiwi bei yoyote. Ni bure kabisa. Hii inapunguza gharama za kutangaza biashara yako na badala yake, hiyo hela unaweza kuitumia kukuza biashara yako. Ukishaweka tangazo lako, kazo yako ni kusubiri wateja wakupigie simu. Ni watakupigia simu maana kila siku kuna zaidi ya watu 20,000 wanaotembelea tovuti ya ZoomTanzania. 

2. Unauza Ukiwa Popote Kwa Wateja Wa Sehemu Yoyote

Ukijiunga  na ZoomTanzania huna haja ya kuwa na hofu juu ya mahali ulipo. Kuna wauzaji wengi wako nje ya Dar es Salaam, na wengine hata wako vijijini na wanakuwa na hofu jinsi kutokana na sehemu walipo. ZoomTanzania inakuondelea hofu hiyo. Kampeni ya Uza Hapo Hapo Ulipo inamaanisha kuwa unaweza kuuza kitu chochote ukiwa sehemu yoyote Tanzania. Ni si hilo tu. Bali wateja wako wanaweza kutoka sehemu yoyoe. Yale mambo ya kusema niko Kariakoo na nawauzia wateja wanaokuja Kariakoo hayako ZoomTanzania. Unaweza kuuza kitu chochote kwa mteja aliyepo sehemu yoyote. Embu fukiria unaweza kuuza bidhaa yako kwa mteja wa Chato. Ama wa Makambako. ZoomTanzania inakupa soko lenye upana mkubwa. Kumbuka, kutangaza ZoomTanzania unahitaji simu na internet tu.

3. Biashara Inakua Mara Dufu 

biashara zoomtanzania

Ukitangaza  ZoomTanzania ni rahisi kukuza biashara yako na kupunguza hasara. Kwa nini? Kwanza, ZoomTanzania inakusaidia kujua bidhaa gani inauzika kwa urahisi, ipi inatazamwa na watu wengi lakini hawakupigii, ipi inatazamwa na wateja wanapiga kuiulizia  n.k. Hili linakusaidia kujua uwekeze zaidi wapi ili kuongeza na upunguze wapi. Mfano, labda umeagiza vifaa vya simu lakini baada ya muda unaona Covers na Chargers zinauzika zaidi  ukilinganisha na proctectors ambazo watu wanaziangalia tu lakini hawanunui. Unaweza kufanya maamuzi ya kupunguza bei ili kuvutia wateja, ama hata kuacha kuuza vifaa ambavyo havinunuliwi ili kuongeza mteja na kuboresha biashara yako kwa vitu vinavyotoka. ZoomTanzania inakusaidia hili kupitia dashboard ambayo kila muuzaji anaipata inayomuonesha jinsi biashara yako inavyoenda.  

4. Ukiwa ZoomTanzania ni Kama Hujafunga Biashara Yako

biashara zoomtanzania

Eti kila siku ufungue duka saa kumi na moja asubuhi na kufunga saa nne usiku na kukosa muda wa kuwa na familia yako. Kila siku unaweza foleni na adha nyingine mpaka unakuwa una hamu kabisa na biashara yako. Kwa nini uteseke wakati unaweza kuweka bidhaa zako ZoomTanzania na kuziuza masaa 24 bila hata ya wewe kunyanyua mguu wako? Ni kweli unaweza kuendelea na duka lako, hatusemi ufunge, lakini mtandao wa ZoomTanzania unakusaidia kupata mbadala nafuu wa kuuza bidhaa zako bila ya wewe kushughulika sana. Hata ukifunga duka lako, kuna watu wanaona tangazo lako usiku wa manane. Ukienda kula chakula cha mchana, kuna watu wanaona tangazo lako mtandaoni. Na hata ukienda Kanisani jumapili na kufunga biashara yako, ukiwa ZoomTanzania ni kama hujafunga biashara yako. 

5. Unapata Wateja Wengi

Ukiwa ZoomTanzania unapata wateja wengi. Kwa sababu mbili kubwa. ZoomTanzania inafikia watu wa kila pande ya Tanzania na hivyo basi ni rahisi kwa mtu aliyeko mbali na wewe kutaka kuinunua bidhaa yako hata kama watu wanaokuja kwenye duka lako hawainunui. Huwezi kujua muhitaji atatoka wapi. Pili, kuna wateja wengi ambao hawawezi kuja kwenye duka lako kwa sababu ya mishughuliko ya kila siku. Wafanyakazi wanaochelewa kutoka kazini hawana muda wa kuja dukani kwako Mwenge. Lakini hao hao wanaweza kuingia ZoomTanzania, wakaona  bidhaa unayouza, wakakupigia simu na kesho yake ukawapelekea mzigo.  

6. Ukiwa ZoomTanzania ni Kama Una Maduka Mawili

Ukishaweka matangazo ya bidhaa zako ZoomTanzania, huna haja tena ya kuwekeza muda mwingi kuangalia biashara yako (kama utakavyofanya ukiwa na duka). ZoomTanzania ni mtandao unaotembelewa na watumiaji wengi  kila siku hivyo ukishaweka tangazo lako, wateja wanakufuata wenyewe. Ukiwa ZoomTanzania ni kama una maduka mawili. Hii itakusaidia kuwekeza muda kwenye shughuli nyingine.. Unaweza hata kuanzisha biashara nyingine mbadala. Mfano unaweza hata ukaanza kuendesha Uber huku bidhaa zako zikijiuza ZoomTanzania. Ni wewe tu kupokea simu na kukubaliana na wateja. 

Kumbuka, ZoomTanzania ni suluhisho lako la kibiashara. Nenda na wakati kwa kuweka bidhaa zako ZoomTanzania. Hata kama unavitu ambavyo huvihitaji, basi viuze ZoomTanzania. Piga picha nzuri na weka bei shindani. Anza kuuza sasa. ZoomTanzania ni ya wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara. Pata kipato na furahia maisha kwa kuuza ZoomTanzania.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media