Siri 5 za Kufanikiwa Katika Biashara ya Nguo Mtandaoni

  | 3 min read
0
Comments
15751
biashara-ya-nguo-mtandaoni

Kuna maelfu ya mataganzo ya  nguo na viatu kwenye mtandaoni wa  ZoomTanzania. Hiyo inamaanisha kuwa kuna ushindani mkubwa katika biashara hii . Ili uwe muuzaji mwenye mafanikio ni lazima ujiongeze na kutoa huduma inayoridhisha, nguo nzuri na tangazo lililojieleza kwa umakini.

Wauzaji wengi wanaofanikiwa  katika biashara ya nguo mtandaoni ni wale ambao nguo zao zinaendana na wakati, na ambazo haziuzwi na kila muuzaji, Hizi ni siri 6 muhimu zitakazokuwezesha kuwa mfanyabiashara wa nguo mwenye kufanikiwa mtandaoni

1. Mara zote weka Vipimo vya Nguo Unazouza

Hakikisha kuwa hauweki tangazo lako la nguo bila ya vipimo vya nguo hizo. Vipimo vya nguo ni muhimu kwa wanunuzi kwa maana itawaonesha kama una nguo za vipimo vyao. Wengi hawatajisumbua kuchukua namba yako ya simu na kukupigia ili kukuuliza vipimo vya  Jeans uliyoitangaza. Watakachofanya watanunua kutoka kwa muuzaji mwingine ambae ameweka vipimo vya nguo anazouza. Moja ya lengo la kwenda kununua nguo mtandaoni ni kuokoa muda, sasa kama muuzaji utashindwa kuwapunguzia wanunuzi wako muda wa kufanya manunuzi basi utawakosa. 

2. Tumia Sanamu (Mannequin) Kuonyesha Mwonekano wa Nguo

Uwezekano wa kuuza nguo zako unaongezeka kama utaonyesha namna nguo hiyo inavyokaa kwenye mwili. Tumia sanamu (mannequin) ama tafuta mtu azivae ili kuonesha jinsi zinavyokaa mwilini.  Hii inawasaidia wanunuzi kuweza kupata picha ya nguo unayouza, urefu wake, au mwonekano wa cheni shingoni, kiatu mguuni n.k. Unaweza kuanza na mdoli unaoonyesha sehemu tu mwili unayotaka kuonyesha nguo au kama mtaji wako unaruhusu basi unaweza kununua mdoli mzima anayeonyesha ngo zote zinavyokaa mwilini. Kama unaweza, tumia mtu azivae. 

3. Hakikisha Picha ya Nguo Inaonekana Pande Zote (Nyuzi 360)

Kwa mara nyingine, hakikisha unamsaidia mnunuzi wa nguo kupata picha jinsi  atakavyoonekana akiivaa hiyo nguo. Kama ni gauni, suruali au T-shirt, hakikisha picha unazozipiga zinaonesha pande zote za nguo hiyo, yaanimbele, nyuma na pembeni. Pia onesha kwa umakini maeneo muhimu ya nguo, mfano zipu, vifungo vinavyovutia, nembo n.k. Yani hakikisha tangazo linamfanya mteja akutafute. Kama utakuwa hujaweka maelezo ya kutosha, basi wacha picha zijielezee zenyewe. 

4. Weka Wazi Aina Ya Kitambaa Kwenye Maelezo 

Pia, wanunuzi wanataka kujua nguo wanayonua imetengenezwa kwa malighafi gani. Mfano, baadhi ya wanunuzi wanaweza kupendelea nguo zilizotengenezwa kwa pamba ikilinganishwa na silikoni. Malighafi zinazotengenezea nguo zinaweza kuwa kikwazo kwa baadhi ya wanunuzi hasa wale wenye matatizo ya kiafya (allergies) kwa baadhi ya aina ya malighafi . Kuna watu wanashauriwa kuvaa nguo za pamba tu kutokana na asili ya ngozi zao. Ni muhimu  kupiga picha lebo ya nguo inayoonyesha aina ya kitambaa kilichotumia ili kusiwe na maswali zaidi.

5. Weka Jina, Rangi na Aina ya Nguo Kwenye  Tangazo Lako

Katika ulimwengu wa teknolojia, mitandao ya kutafutia data mfano Google imeboreshwa kufanya watafutaji kupata vitu kwa urahisi sana. Wanachotakiwa kufanya ni kuandika kitu wanachotafuta na bidhaa wanayoitaka ionekane. Ndio maana, ni muhimu sana kuandika jina la nguo unayouza, watengenezaji wake na rangi ili kuwezesha mtandao kama Google kuonyesha bidhaa yako iwe ya kwanza pale tu mnunuzi atakapoitafuta akitumia moja ya neno lililo katika tangazo lako. Mfano, mtu akiwa anataka nguo fulani, akienda Google akiandika ‘fulana nyeupe’, au kiatu cha Converse, Suruali ya Jeans, basi tangazo la nguo zako litatokea endapo tu maneno hayo yako katika tangazo lako. Pia ni muhimu kujua wanunuzi wako wanatumia maneno gani  gani wakati wanatafuta bidhaa kama unayouza., Tumia maneno hayo (keywords) katika maelezo ya bidhaa yako. Ili kufanikiwa katika hili, fanya utafiti kidogo.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media