Biashara Mpya? Hatua Rahisi za Kuuza Bidhaa 10 za Mwanzo

  | 3 min read
0
Comments
3108
uza bidhaa 10 za mwanzo

Unapoanzisha biashara mpya mtandaoni, mauzo yako ya mwanzo ni muhimu sana. Ni mauzo yatakayokufanya upate moyo, yatakayokusaidia kupata picha ya soko, na kupanga mkakati wako wa mauzo. Kwa kawaida, mauzo ya mwanzo huwa magumu zaidi kuyapata.

Hizi ni njia muhimu unazoweza kuzitumia ili kufanikisha mauzo yako ya mwanzo yatakayokuwezesha kujua soko lako lilipo.

1. Anza na Marafiki Na Familia

biashara mpya marafiki na familia

Mbinu ya kwanza ya kufanya mauzo ya bidhaa yako ya kwanza ni kuwatumia marafiki na wanafamilia wako. Hii haimaanishi umtumie Mama au kaka yako, au rafiki wako wa karibu wanunue bidhaa ambayo hawataitumia. Mfano kama unauza saa za kiume, huwezi ukamtafuta mama anunue kisa tu ni mwanafamilia. Unachotakiwa kufanya ni kufikiria na kumtafuta ndugu au rafiki ambaye anaweza kuihitaji na atafurahia kutumia bidhaa yako. Hawa ni watu muhimu na rahisi kupata maoni yao kuhusu bei na ubora.

2. Fanya Shindano na Toa Zawadi

Tuongelee ukweli. Zawadi mara zote zimekuwa njia nzuri sana ya kufanya watu waone bidhaa yako mpya. Zawadi, mashindano na punguzo la bei vikifanywa kwa usahihi vinaweza kuleta watu wengi sana katika duka lako kwa kutumia maneno ya mdomo, hivyo kusaidia kusambaa kwa uwepo na elimu juu ya duka lako na bidhaa zake. Mfano, unabidhaa mpya unataka kuingiza sokoni.

Unaweza ukafanya shindano la watu ku-share ujumbe fulani kuhusu bidhaa yako kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii na wanaweza wakashinda bidhaa hiyo bure. Watu wengi wakishiriki, itasaidia kuenea uelewa wa uwepo wa bidhaa yako sokoni.

3. Weka Mkakati wa Kuwauzia Marafiki Kupitia Mitandao Ya Kijamii

uza bidhaa 10 za mwanzo tangaza facebook

Sawa, mwanzo tulisema unaweza kuongea na wanafamilia au marafiki wanunue bidhaa kwako. Lakini hawa ni wale wa karibu, uko nao kila siku — au tuseme umewatafuta kwenye shughuli fulani ya kifamilia. Sasa ni wakati wa kutafuta wale marafiki ambao hauko nao kariu sana katika mitandao ya kijamii. Mfano mtandao kama Facebook, wanakuwezesha kuchagua idadi fulani ya marafiki ambao wanaweza kuwa wanavutiwa na bidhaa yako. Facebook wanatambuua hili kutokana na maneno maalum (Keyword) ambayo yanahusiana na bidhaa yako na marafiki zako wamekuwa wakiyatumia kutafuta vitu mbali mbali mtandaoni. Ukiwatambua, sasa unaweza kuwatumia ujumbe moja kwa moja.

4. Tangaza ZoomTanzania au Mitandao Mingine ya Matangazo

biashara mpya

Kuwa mjasiriamali wa mtandaoni inamaanisha unatakiwa uwepo kila mahali mtandaoni. Hii inajumuisha uwepo wako sehemu zote, hasa zile ambazo wateja wako wanaweza kuwepo. Mtandao kama ZoomTanzania unaweza kuwa soko zuri zaidi kwa bidhaa yako, hasa kutokana na idadi kubwa ya wanunuzi na wauzaji wanaotembelea hapo kila siku. Unaweza ukaangalia jinsi ya kutangaza bidhaa zako ZoomTanzania hapa.

5. Fanya Matangazo ya Kulipia Facebook na Instagram

Facebook na mshirika wake Instagram wana vipengele muhimu vinavyowasaidia wafanyabiashara au watangazaji wa bidhaa kufikia kundi maalum la wateja wanaoweza kuvutiwa na bidhaa fulani. Ni mitandao ambayo kila mjasiriamali mpya mtandaoni anatakiwa aijaribu. Kumbuka kuwa, mwanzo unaweza kuingia gharama wakati unatafuta kundi maalum la watumiaji ili kupata wanunuzi sahihi. Cha msingi, ni kufuatilia matokea ya kila kampeni ya matangazo utakayofanya na kuirekebisha kila mara itakapobidi.

Kumbuka kuwa, mauzo yako ya kwanza si lazima yalete faida — unatafuta soko la kudumu, wateja watakaoridhika na bidhaa na mbinu za kuwafikia na kuwafikishia bidhaa hiyo.

Mustapha Mosha
Mustapha Ally is a Community Marketing Manager at Zoom Tanzania and BrighterMonday Tanzania. He loves digital marketing social media