ONIMAS Shopifier

About Us

ONIMAS - ni program (software) ambayo inamsaidia mfanyabiashara kuchanganua,
kuendesha na kumpa mwongozo katika shughuli zake za kibiashara.
Ni kwa biashara ndogondogo (rejareja) na za maduka ya jumla. Ni programu inayotumia lugha
ya Kiswahili na nyepesi kutumia kwa kila mfanyabiashara.
Kwa kutumia ONIMAS mfanyabiashara anaweza kujua mzunguko wa fedha, bidhaa, faida
iliyopatikana kwa kila bidhaa akiwa mahali popote mfano akiwa nje ya eneo la biashara, nje ya
mkoa au nje ya nchi.
ONIMAS inatumika kwa aina zote za biashara ambapo mtumiaji ana uwezo wa kuitumia kwa
zaidi ya duka au mradi mmoja na kuyaunganishwa kama duka moja.

WATUMIAJI, NI MADUKA YA
i. Vifaa vya ujenzi
ii. Vifaa vya umeme
iii. Vifaa vya mashine (spares)
iv. Vifaa vya nyumbani na shamba
v. Vifaa vya elektroni
vi. Nguo, viatu ,mitumba, n.k
vii. Wauza nafaka, matunda, mboga,
viii. Maduka ya jumla na
supermarket
ix. Wauza mbao, matofali, n.k
x. Wauza vitabu na Stationary
xi. Bidhaa mchanganyiko
xii. Bidhaa za kilimo, mifugo na
madawa
xiii. Vituo vya uzalishaji mikate,
vinywaji, n.k

KAZI ZINAZOFANYWA NA ONIMAS
i. Kusaidia kudhibiti gharama, kukokotoa fedha
taslimu, kutoa mchanganuo wa mapato na
matumizi ya ziada na kutengeneza ripoti za faida
na hasara za (siku, juma, mwezi na mwaka)
ii. Inatengeneza stock ya bidhaa ya kila siku.
iii. Kumbukumbu za madeni, invoisi, orders kwa
wateja na wasambazaji (vendors).
iv. Kutambua bidhaa zikikaribia mwisho wa muda
wa matumizi (to expire).
v. Kuandaa na kuchambua kumbukumbu za
kifedha (Financial/Accounting records)
vi. Ripoti nyingine ni za mzunguko wa bidhaa
(Stock transfer), mauzo na manunuzi, invoisi,
orders, madeni, taarifa za wafanyakazi, n.k

MAHITAJI
Uwe na kompyuta angalau moja hata yenye uwezo wa kawaida. Inaweza kuwa ya mezani
(desktop) au mpakato (laptop). Toleo la simu ya kiganjani nalo litakuwepo hivi punde.

Business Address
Dodoma Mjini Dodoma Bahi Road
Business Id
567301
ONIMAS Shopifier
Member Since 24. Sep '14 0 Active Ads 2 Published Ads
Contact Business
Phone Business
Email Business
Report This Ad
Cancel
Join our Mailshot

Notification for member sales, events and promotions.